Mahakama yawastaafisha Kalpana Rawal na Philip Tunoi

Posted in
No comments
Friday, May 27, 2016 By danielmjema.blogspot.com

Naibu wa Jaji mkuu,  nchini Kenya, Kalpana Rawal na Jaji wa mahakama ya juu, Philip Tunoi ambao walifungua kesi mahakamani kuweka zuio la amri ya kuwataka kustaafu baada ya kufikisha umri wa kustaafu kisheria (70), kwa lengo la kuendelea kukaa ofisini wamepoteza kesi hiyo na sasa wameamriwa kuachia ngazi.
Kwa mujibu wa hukumu iliyotolewa leo na mahakama ya Rufaa, jijini Nairobi, ikiwa ni rufaa dhidi ya hukumu iliyotolewa miezi kadhaa iliyopita ikiwapa majaji hao haki ya kuendelea kuwepo ofisini. Wakili wa Rawal, Waweru Gatonge amesema hata hivyo kwamba wanafanya utaratibu wa kukata rufaa nyingine.
Tunoi aliamua kwenda mahakamani akipinga kustaafu katika umri wa miaka 70 na kudai kuwa anapaswa kustaafu akiwa umri wa miaka 74,kwa madai kwamba aliteuliwa kushika wadhifa alionao wakati ambapo Katiba iliyoelekeza hivyo tayari imeshafanyiwa masahihisho.
Kwa upande Rawal yeye tayari ameshafikisha umri stahiki ya kustaafu na kulikuwa na taarifa kwamba alikuwa anafikiria kumkaimu Jaji Mkuu Dr. Willy Mutunga anayestaafu mwezi ujao. Mwishoni mwa mwezi Januari mwaka huu, Mahakama kuu ilizuaia jaribio la kamisheni ya wanasheria, Judicial Service Commission (JSC), kumzuia Rawal katika harakati zake za kukata rufaa.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .