Mapema leo, Kikosi cha timu ya Taifa ya Tanzania, ikifanya mazoezi katika uwanja wa Kasarani, kuelekea mechi ya kirafiki na Harambee Stars

Posted in
No comments
Saturday, May 28, 2016 By danielmjema.blogspot.com


Kikosi cha timu ya taifa ya Tanzania kikifanya mazoezi jijini Nairobi kuelekea mchezo wake wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya timu ya taifa ya Kenya Harambee Stars kwa ajili ya kujipima nguvu kabla ya kukabiliana na Misri kuwania kufuzu kucheza fainali za mataifa ya Afrika mwaka 2017.

Balozi wa Tanzania nchini Kenya, Dk. John Haule akipiga picha ya pamoja na wachezaji na viongozi wa timu ya soka ya Tanzania baada ya kuzungumza nao na kuwatoa hofu ya maisha na usalama wakiwa Nairobi, Kenya. Taifa Stars inayodhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro, ipo Nairobi kwa ajili ya mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Harambee Stars ya Kenya utakaofanyoka kesho Jumapili kwenye Uwanja wa Moi Kasarani. 
Kikosi cha timu ya soka ya Tanzania-Taifa Stars, kikikifanya dua kwenye Uwanja wa Camp Toyoyo uliopo Jericho, nje kidogo ya jiji la Nairobi. Taifa Stars inayodhaminiwa na Bia ya Kilimanjaro, ipo Nairobi kwa ajili ya mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Harambee Stars ya Kenya utakaofanyoka kesho Jumapili kwenye Uwanja wa Moi Kasarani. (Picha zote zimepigwa na Alfred Lucas, Ofisa habari wa TFF)

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .