Real Madrid watwaa Uefa Champions kwa mara ya 11, waipiga Athletico 5-3

Posted in
No comments
Sunday, May 29, 2016 By danielmjema.blogspot.com

Cristiano Ronaldo amefunga penalti ya mwisho na kuisaidia Real Madrid kuendelea rekodi ya kutwaa taji la Uefa Champions League mara nyingi zaidi ikiwa ni mara ya 11, baada ya kuwafunga Mahasimu wao Athletico Madrid kwa mikwaju 5-3 katika mechi ngumu ya fainali, iliyopigwa kwenye dimba la San Siro, mjini Milan, nchini Italy.



Mechi hiyo ililazimika kuingia dakika za nyongeza (120) baada ya dakika 90 kumalizika timu zote zikiwa zimefungana 1-1. Real ndio walikuwa wa kwanza kupata bao kunako kipindi cha kwanza, dakika ya 17, kupitia kwa nahodha wake, Sergio Ramos kabla ya Yannick Carrasco, aliyeingia akitokea benchi hajaisawazishia Athletico, katika dakika ya 79, kipindi cha pili.

Ushindi huu unamfanya Kocha Zinedine Zidane kuwa mtu wa saba kutwaa taji hili akiwa kama Kocha na kama Mchezaji. 

Tutaendelea kukuletea taarifa na picha zaidi kuhusu fainali hii. endelea kutembelea Sauti Kuu kwa habari za siasa, Biashara, michezo na burudani kutoka kila pembe la Dunia.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .