Meli kubwa zaidi duniani yakamilika, ina ukubwa wa viwanja vinne vya mpira
Posted in
Jukwaa la Habari
No comments
Thursday, May 19, 2016
By
danielmjema.blogspot.com
Meli kubwa zaidi duniani imekamilika ikiwa na ukubwa wa viwanja vinne vya mpira wa miguu. Meli hiyo iliyopewa jina la ‘Harmony Of The Seas’ imechukua miezi 32 mpaka kumaliza kutengenezwa. Ina vyumba 2747, mabwawa 23 ya kuogelea, hoteli na bar, sehemu za michezo, viwanja vya helkopta lakini pia ina uwezo wa kuchukua abiria 6780.
Aidha gharama za kusafiri na meli hiyo ni £900 lakini kuingia mpaka sehemu za starehe inagharimu £2,760 kwa mtu mmoja. Watengenezaji wa meli hiyo wamesema ‘Harmony Of The Seas’ ni meli yao ya 25 kwenye kampuni Royal Caribbean International fleet.
Tazama picha zaidi.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :