Showing posts with label Jukwaa la Habari. Show all posts
Showing posts with label Jukwaa la Habari. Show all posts

Wajumbe waidhinisha ushindi wa Donald Trump

Wajumbe waidhinisha ushindi wa Donald Trump

No comments
By danielmjema.blogspot.com
Wajumbe wa Jopo la Kuamua Mshindi wa Urais nchini Marekani wamemuidhinisha Donald Trump kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika Novemba.
Hii ni licha ya juhudi za dakika za mwisho za kutaka kumzuia kuingia ikulu ya White House mwezi Januari.
Wiki sita baada ya uchaguzi mkuu kufanyika tarehe 8 Novemba, mwanachama huyo wa Republican amepata zaidi ya kura 270 za wajumbe ambazo alikuwa anahitaji kufanya rasmi ushindi wake.
Baada ya ushindi huo, Bw Trump ameahidi "kufanya kazi kuunganisha nchi yetu na kuwa rais wa Wamarekani wote". Wajumbe walikuwa wametumia ujumbe mwingi kupitia barua pepe na pia kupigiwa simu wakihimizwa kutomuunga mkono bilionea huyo kabla yao kukutana kupiga kura.
Shughuli yao ya kupiga kura kwa kawaida huwa kama shughuli ya kutimiza wajibu tu, ambapo huwa wanamuidhinisha mshindi, lakini mwaka huu uchaguzi umegubikwa na tuhuma za kuingiliwa na wadukuzi kutoka Urusi.
Jimbo la Texas hatimaye lilimuwezesha kufikisha idadi ya kura 270 za wajumbe alizohitaji,, licha ya wajumbe wawili wake kugeuka na kupiga kura kumpinga.
Gazeti la New York Times pia linaripoti kwamba kuna wajumbe wanne wa chama cha Democratic, chake Hillary Clinton, ambao walimpigia kura mgombea mwingine lakini Bi Clinton. Matokeo ya kura hiyo yatatangazwa rasmi tarehe 6 Januari kwneye kikao maalum cha pamoja cha bunge la Congress.
"Nawashukuru Wamarekani kwa kunipigia kura kwa wingi kuwa rais wa Marekani," Bw Trump alisema kupitia taarifa baada ya matokeo kutangazwa.

"Kwa hatua hii ya kihistoria, tunaweza sasa kutazama mbele na kutarajia maisha ya kufana siku za usoni. Nitafanya kazi kwa bidii kuunganisha nchi yetu na kuwa rais wa Wamarekani wote," alisema.

BBC

Meli kubwa zaidi duniani yakamilika, ina ukubwa wa viwanja vinne vya mpira

Meli kubwa zaidi duniani yakamilika, ina ukubwa wa viwanja vinne vya mpira

No comments
By danielmjema.blogspot.com
34475E0400000578-3593741-image-a-3_1463470551324
Meli kubwa zaidi duniani imekamilika ikiwa na ukubwa wa viwanja vinne vya mpira wa miguu. Meli hiyo iliyopewa jina la ‘Harmony Of The Seas’ imechukua miezi 32 mpaka kumaliza kutengenezwa. Ina vyumba 2747, mabwawa 23 ya kuogelea, hoteli na bar, sehemu za michezo, viwanja vya helkopta lakini pia ina uwezo wa kuchukua abiria 6780.
344847EC00000578-3593741-image-a-25_1463476641104meli
Aidha gharama za kusafiri na meli hiyo ni £900 lakini kuingia mpaka sehemu za starehe inagharimu £2,760 kwa mtu mmoja. Watengenezaji wa meli hiyo wamesema ‘Harmony Of The Seas’ ni meli yao ya 25 kwenye kampuni Royal Caribbean International fleet.
Tazama picha zaidi.
34484AB100000578-3593741-image-a-24_146347656657134476E9100000578-3593741-image-a-1_1463470492113
Meli 04
344763AA00000578-3593741-image-a-20_1463470952693
3445EDE100000578-3593741-image-a-7_1463470650433

Usithubutu kufanya vitu hivi ukiwa Dubai

Usithubutu kufanya vitu hivi ukiwa Dubai

No comments
By danielmjema.blogspot.com
Dubai ni moja ya miji ambayo kwa sasa watanzania wengi wanaenda kwa ajili ya kufanya biashara mbalimbali, sasa mtu wangu nimekutana na hivi vitu kumi na moja ambavyo hutakiwi kuvifanya ukiwa Dubai.
1. Kutojihusisha na shughuli za Madawa ya kulevya, inasemeka Dubai wako makini kwenye suala ya kupinga matumizi na uuzaji wa madawa ya kulevya huenda kuliko mji wowote.
2. Hutakiwi kunywa pombe kwenye maeneo ya Public.
3. Hutakiwi kuvaa bila Kujistiri, wanawake wanatakiwa kujiepusha na kutembea nusu uchi kwenye maeneo kama beach na hata wanaume wanatakiwa Kujistiri wakati wakitembea kwenye mitaa ya mji huo.
4. Hutakiwa kupiga muziki kwa sauti ya juu wala kucheza mpaka uwe katika maeneo ambayo ni maalum kwa shughuli hizo kama vile klabu.
5. Hauruhusiwi kukiss ukiwa public, wanandoa waingereza walifungwa kwa kufanya mapenzi beach lakini hata kiss inaweza kukuweka matatani.
6. Epuka maneno ya kufuru dhidi ya Uislamu.,wageni wengi wamekuwa matatani kwa sababu walikuwa wanajaribu kutoa maoni yao.
7. Kuwa mwangalifu na kamera yako, hauruhusiwi kupiga picha mtu picha bila idhini yake. 
 9. Kuwa mwangalifu na Wallet yako . Dubai imeelezwa kuwa na kiwango kidogo sana cha uhalifu lakini uhalifu mdogomdogo unajitokeza kama sehemu zingine.
10. Usile hadharani kipindi cha Ramadhani, hutakiwi kula, kunywa au kuvuta sigara wakati wa mfungo hata kutafuna Big G.
 11. Usitumie mkono wa kushoto kwa sababu mkono huo hutumika kwa ajili ya usafi wa mwili, usimsalimie yeyote kwa mkono wa kushoto, kufungua mlango wala usimpe mtu chakula kwa mkono wa kushoto.
Unaweza kuiangalia video hii hapa chini

VIWANJA 10 BORA VYA NDEGE DUNIANI HADI KUFIKIA MACHI 2016 HIVI HAPA

VIWANJA 10 BORA VYA NDEGE DUNIANI HADI KUFIKIA MACHI 2016 HIVI HAPA

No comments
By danielmjema.blogspot.com

Kwa mwaka wa nne mfululizo uwanja wa Ndege wa Singapore Changi  umekuwa ndio uwanja wa ndege bora zaidi duniani ukishika nafasi ya kwanza na ulichukua tuzo za SkyTrax World Airport Awards 2016 ambapo ulitangazwa huko Gologne Germany, Tuzo za Skytrax zinategemea kura zinazokusanywa kutoka kwa mamillioni ya abiria.

1. Singapore Changi Airport
1
2. Incheon International Airport (South Korea)
2
3. Munich Airport (Germany)
OLYMPUS DIGITAL CAMERA
4. Tokyo International Airport Haneda
4
5. Hong Kong International Airport
5
6. Chubu Centrair International Airport (Nagoya, Japan)
6
7. Zurich Airport (Switzerland)
7
8. London Heathrow Airport
8
9. Kansai International Airport (Osaka, Japan)
9
10. Hamad International Airport (Doha, Qatar)

YALIYOJIRI: TRUMP AMSHUKIA PAPA FRANCIS

YALIYOJIRI: TRUMP AMSHUKIA PAPA FRANCIS

No comments
By danielmjema.blogspot.com

BILIONEA anayewania kuteuliwa na Chama cha Republican kuwania urais nchini Marekani, Donald Trump, amemkosoa kiongozi wa Kanisa Katoliki duniani, Papa Francis na kusema ni aibu kwa kiongozi huyo wa dini kuhoji imani yake.

Kauli ya Trump imekuja siku chache baada ya Papa kukosoa kauli yake ya kwamba atajenga ukuta kutenganisha Marekani na Mexico na kusema kuwa “mtu anayeweza kujenga ukuta kutenganisha watu badala ya kujenga daraja si Mkristo.”
Papa alitoa kauli hiyo wakati akimalizia ziara yake nchini Mexico ambako alisema kauli yake hailengi kuwashawishi watu wasimpigie au kumpigia kura mgombea huyo ambaye amekuwa na kauli zinazozua gumzo mara kwa mara.
Trump alimjibu Papa na kudai kuwa; “Kiongozi hususani wa dini ni aibu kuhoji imani ya mtu,” alisema na kuongeza kuwa pamoja na kauli hiyo yeye hajali na kwamba haikuwa ya Papa binafsi bali ilichagizwa na Serikali ya Mexico.
Pia watu kadhaa wakiwemo mahasimu wa kisiasa wa Trump wameonyesha kupinga kauli ya Papa huku wengine wakiwa hawaamini kama Papa anaweza kutoa kauli hiyo.
Mpinzani wake katika kinyang’anyiro cha awali Seneta Marco Rubio, alisema hataki kuzungumzia suala hilo hadi atakaposoma maoni yote ya Papa.
Hata hivyo, aliongeza kuwa Marekani ina haki na wajibu wa kutekeleza sheria zake za uhamiaji.
“Hili ni taifa huru na tuna haki ya kudhibiti anayekuja, muda anaokuja na namna anavyokuja,” The Guardian ilimnukuu Rubio akiwa South Carolina.
“Mji wa Vatican unadhibiti wanaoingia, muda wanaoingia na namna wanavyoingia na kwa hivyo Marekani nayo ina haki ya kufanya hivyo.”
Hata hivyo, Rubio ambaye ni Mkatoliki alisema anaamini na kumheshimu Papa kama mrithi wa Mtume Petro.
Mpinzani mwingine wa Trump ambaye alibadili dhehebu na kuwa Mkatoliki na aliyekuwa Gavana wa Florida, Jeb Bush, alimwambia mwandishi wa Guardian kuwa: “Ukristo ni kati yake na muumba wake.”
Akizungumzia kauli ya Papa alisema haelewi inamaanisha nini lakini yeye binafsi anaunga mkono suala la kujenga ukuta na fensi pale panapohitajika.
“Nafikiri ni sahihi nikiwa kama Mkatoliki nipewe maelekezo ya Ukatoliki kutoka kwa Papa, lakini si kwenye mambo ya uchumi au mazingira,” alisema Bush.

MKE WA WAZIRI MKUU AZINDUA TAASISI YA MANJANO FOUNDATION

MKE WA WAZIRI MKUU AZINDUA TAASISI YA MANJANO FOUNDATION

No comments
By danielmjema.blogspot.com

Mgeni Rasmi kwenye halfa ua Uzinduzi wa Taasisi ya Manjano Foundation Pamoja na Vipodozi Pendwa Vijulikanavyo kama Luv Touch Manjano Mke wa Waziri Mkuu Mh Tunu Pinda Akitoa Hotuba yake katika Uzinduzi huo .Katika Hotuba yake Mh Mama Pinda Alisema amefurahishwa sana Kwa Mwanamke wa Kitanzania Kuanzisha Bidhaa amabyo imeweza kushindana na Bidhaa kama hizo kutoka mataifa Mengine.
 
Halfa hiyo iliyofanyika kwenye Ukumbi wa Diamond Jubilee.Hafla hiyo ya uzinduzi ilifunguliwa na mke wa Waziri Mkuu wa Tanzania mama Tunu Pinda. Alizindua rasmi kwa soko la Tanzania poda ya luvtouch Manjano, rangi ya awali (foundation), na rangi ya mdomo (lipstick) na walio hudhuria hafla hiyo walipata nafashi ya kushuhudia thamani ya bidhaa hizo, aina ya urembo na viwango vya ubora vinvyoshinda hoja zote na kuthibitisha kuwa bidhaa za hapa nchini zinaweza kushindana na bidhaa za kimataifa. Wanawake wengi walipata fursa ya kujaribu moja ya bidhaa hizo na waliweza kununua bidhaa za LuvTouch Manjano ukumbini.

Mtoa Mada kwenye Halfa hiyo Mh Balozi Mwanaidi Majaar Akisisitiza Jambo kwenye Halfa Hiyo.Mh Balozi Majaar Alisisitiza Umuhimu wa Kumsomesha Mtoto wa Kike Pamoja na Kuwawezesha Kiuchumi.Balozi Majari alisiistiza Jamii ya Kitanzania Kuachana na Kasumba ya Kuwanyanyapaa Watoto wa Kila pia Kutokuwawezesha na Akasema mtoto wa Kike akipewa Fursa ya Kupata Elimu na Kuwezeshwa Wanawake Wanaweza.
 
Hafla hiyo pia ilihusisha kuzindua Taasisi ya Manjano Foundation, ambayo imeanzisha jukwaa kwa ajili ya kuandaa miradi na programu ambazo zitamuinua mwanamke wa Kitanzania kwa kumwondolea umasikini wa kipato na ambayo itakuwa ni chachu ya kubadili yale yote yaliyoyazunguka maisha yake. Shirika hili limekwishazindua mradi wenye kubeba bendera yake, Manjano Dream-Makers, mradi unaokusudia kuzaa kizazi kipya cha wajasiriamali wanawake kwa kutumia kipodozi cha LuvTouch Manjano tu.
 
Shear illusions ilikusanya wanawake takriban 450 wa Kitanzania kusherehekea miaka 10 ya safari ya kumfurahisha kila mwanamke, pamoja na kuzindua kipodozi pendwa cha LuvTouch Manjano iliyobuniwa na Shekha Nasser, mmiliki wa Shear illusions. Pamoja na uzinduzi huo, alizundua pia kitabu cha muongoza kwa kina mama kuonyesha jinsi ya kujipodoa kitaalam kwa kutumia nyenzo na vipodozi sahihi.
 
Afisa Mtendaji Mkuu wa Shear illusions Ltd. Mama Shekha Nasser Katikati akiongea Mgeni Rasmi a Mke wa Waziri Mkuu Mh Mama Tunu Pinda (Kulia) Pamoja na Mtoa Mada kwenye Halfa hiyo Mh Balozi Mwanaidi Majaar
Balozi wa Manjano Foundation Irene Paul Wakati wa Uzinduzi wa Taasisi ya Manjano Foundation Pamoja na Uzinduzi wa Vipodozi Pendwa vya Luv Touch.
Balozi wa Manjano Foundation Irene Paul (Kulia) Akiwa n Mtoa Mada katika Halfa hiyo Mama Rehema Kasule Kutoka Uganda
Msanii aliyetumbuiza Kwenye Halfa Hiyo Brian Mugenyi akitoa Burudani ya aina yake kwenye Halfa hiyo iliambatana na Uzinduzi wa Vipodozi vya Luv Touch 
Wageni waalikwa walioshiriki katika halfa ya Uzinduzi wa Taasisi ya Manjano Foundation.
 
SOURCE:MICHUZI BLOG

IMETOSHA YATEMBELEA KITUO CHA BUHANGIJA, MKOANI SHINYANGA

IMETOSHA YATEMBELEA KITUO CHA BUHANGIJA, MKOANI SHINYANGA

No comments
By danielmjema.blogspot.com
Ilikua mishale ya saa kumi kamili jioni ujumbe wa harakati za Imetosha ulipowasili katika kituo cha Buhangija cha kulea watoto wenye mahitaji maalumu mjini Shinyanga. Sauti za furaha za watoto zilisikika zikiimba nyimbo za kukaribisha ujumbe wa wana harakati hao ambao wako Mwanza kutambulisha harakati za Imetosha ambazo ni kupambana na kupinga unyanyapaa, ukatili na mauaji kwa watu wenye Ulemavu wa ngozi.

Balozi wa Imetosha Henry Mdimu akinunua mahitaji ya watoto waliopo kituoni hapo kabla ya kufika kituoni hapo.

Huyu ni Irene wa NHIF Shinyanga
 

Wajumbe wa Imetosha

 Akiongea na watoto kituoni hapo Mwenyekiti wa harakati za Imetosha Masoud Ali (Kipanya) alisema Imetosha inatambua umuhimu wa haki ya kuishi kwa kila binadamu ndio maana Imetosha imeanzisha harakati za kutokomeza mauaji na unyanyapaa kwa watu wenye ulemavu wa ngozi.  “Tunatambua hapa kati yenu kuna vipaji vya aina mbalimbali hivyo pamoja na kupambana na harakati za kupinga na kutokomeza mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi tupo hapa kuwatia moyo kuwa mna uwezo mkubwa ndani yenu hivyo msijidharau” alisema Masoud.


Kipanya akimuimbisha mtoto wa kituoni hapo


Mwl Peter Alali Francis akisisitiza jambo wakati akiongea na ujumbe wa Imetosha


 Alisema“Pamoja na uhaba wa mabweni kituo kinakabiliwa na uhaba wa chakula. Muda mwingine watoto hawa hushindia mlo mmoja. Chakula mlichofikisha leo hapa kitatusogeza maana tulikua tumeishiwa chakula kabisa” alisema Francis. Ujumbe huo wa Imetosha uliwasilisha kambini hapo unga kilo 50, mchele kilo 50, chumvi kilo 5 na mafuta ya kupikia lita 10. 


Mwalimu Mkuu wa Kituo hicho Peter Ajali Francis alishukuru ujio wa wanaharakati wa Imetosha kituoni hapo na kusema kituo hicho kilianzishwa mwaka 1960 kikiwa chini ya Kanisa katoliki.
Kituo hicho kilikua maalumu kwa ajli ya watoto wasiiona na viziwi lakini kutokana na mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi kuongezeka mwaka 2006 kituo hicho kilianza kupokea watoto wenye ulemavu wa ngozi kutoka sehemu mbalimbali toka kanda ya Ziwa. Kituo kina jumla ya watoto 388 kati ta hao 284 wana ulemavu wa ngozi. Kituo hicho kinakabiliwa na uhaba wa mabweni ambapo chumba chenye uwezo wa kuchukua watoto 50 kinachukua watoto zaidi ya 100 na chenye uwezo wa kuchukua watoto 40 kinachukua watoto zaidi ya 80.


 Zaytun Biboze akiwa amebeba mmoja wa watototo wanaoishi katika ktuo hicho



Masoud Kipanya na Jhikoman wakiwaimbisha watototo wimbo waupenda wa Clap your hands!

Isaya Mwakilasa aka Wakuvwanga akiwachekesha watoto kiuoni Buhangija, Shinyanga



Magunia haya ya unga, mafuta na mchele ndio msaada wa chakula ambao Imetosha ilitoa kwa kituo hicho



Katibu wa Imetosha amabaye ki taaluma ni mwandishi wa habari akimhoji mwalimu Francis Ajali

Wanaharakati wa Imetosha wamepanga kurudi tena mjini Shinyanga mwezi Mei na kukifanya kituo hicho kuwa ngome ya kuanzishia mapambano dhidi ya unyanyapaa, ukatili na mauaji kwa albino.
Picha na Mkala Fundikira habari na Salome Gregoy/ Mkala Fundikira 

KUELEKEA SIKU YA HEDHI DUNIANI, MTANDAO WA HEDHI SALAMA WAENDESHA SEMINA SHULE YA SEKONDARI ST. ANTHONY

KUELEKEA SIKU YA HEDHI DUNIANI, MTANDAO WA HEDHI SALAMA WAENDESHA SEMINA SHULE YA SEKONDARI ST. ANTHONY

No comments
By danielmjema.blogspot.com

 Kutoka kushoto ni Mkurugenzi mtendaji wa Kasole Secrets Hyasintha Ntuyeko ambao pia ni watengenezaji wa Pads za Glory, Katikati ni Mlezi wa wanafunzi Hilda Minja na Sara Mugele ambaye ni Dean of students  Shule ya Sekondari ya St. Anthony.
 Daktari Edna Kiogwe akieleza juu ya umuhimu wa elimu ya Hedhi kwa jamii nzima wakati wa semina na wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya St. Anthony.
Mkurugenzi mtendaji wa Kasole Secrets Hyasintha Ntuyeko ambeye pia ni muandaaji wa siku ya Hedhi Duniani kwa Tanzania akielezea umuhimu wa kutunza Mazingira wanapokuwa Hedhi na kuithamini miundombinu.
 Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya St. Anthony wakiwa wanafuatilia kwa makini Semina hiyo.
 Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya St. Anthony wakifurahia Pads za Glory walizopewa ikiwa ni ishara ya kusherehekea sikukuu ya Hedhi Duniani.
Baadhi ya wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya St.Anthony wakifurahia zawadi za Glory Pads baada ya Semina.

Kufahamu zaidi juu ya Hedhi salama Bofya www.hedhisalama.com


Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .