Wajumbe waidhinisha ushindi wa Donald Trump
Posted in
Jukwaa la Habari
No comments
Tuesday, December 20, 2016
By
danielmjema.blogspot.com
Wajumbe wa Jopo la Kuamua Mshindi wa Urais nchini Marekani wamemuidhinisha Donald Trump kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika Novemba.
Hii ni licha ya juhudi za dakika za mwisho za kutaka kumzuia kuingia ikulu ya White House mwezi Januari.
Wiki sita baada ya uchaguzi mkuu kufanyika tarehe 8 Novemba, mwanachama huyo wa Republican amepata zaidi ya kura 270 za wajumbe ambazo alikuwa anahitaji kufanya rasmi ushindi wake.
Baada ya ushindi huo, Bw Trump ameahidi "kufanya kazi kuunganisha nchi yetu na kuwa rais wa Wamarekani wote". Wajumbe walikuwa wametumia ujumbe mwingi kupitia barua pepe na pia kupigiwa simu wakihimizwa kutomuunga mkono bilionea huyo kabla yao kukutana kupiga kura.
Shughuli yao ya kupiga kura kwa kawaida huwa kama shughuli ya kutimiza wajibu tu, ambapo huwa wanamuidhinisha mshindi, lakini mwaka huu uchaguzi umegubikwa na tuhuma za kuingiliwa na wadukuzi kutoka Urusi.
Jimbo la Texas hatimaye lilimuwezesha kufikisha idadi ya kura 270 za wajumbe alizohitaji,, licha ya wajumbe wawili wake kugeuka na kupiga kura kumpinga.
Gazeti la New York Times pia linaripoti kwamba kuna wajumbe wanne wa chama cha Democratic, chake Hillary Clinton, ambao walimpigia kura mgombea mwingine lakini Bi Clinton. Matokeo ya kura hiyo yatatangazwa rasmi tarehe 6 Januari kwneye kikao maalum cha pamoja cha bunge la Congress.
"Nawashukuru Wamarekani kwa kunipigia kura kwa wingi kuwa rais wa Marekani," Bw Trump alisema kupitia taarifa baada ya matokeo kutangazwa.
"Kwa hatua hii ya kihistoria, tunaweza sasa kutazama mbele na kutarajia maisha ya kufana siku za usoni. Nitafanya kazi kwa bidii kuunganisha nchi yetu na kuwa rais wa Wamarekani wote," alisema.
BBC
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :