Hakuna Bifu!! Ali Kiba amuombea kura Diamond
Posted in
Burudani
No comments
Tuesday, May 24, 2016
By
danielmjema.blogspot.com
Msanii Alikiba amefunguka na kusema kwa mafanikio aliyopata toka amerudi kwenye muziki tena ndani ya muda mfupi ni sawa na kuchana msamba kwake maana siyo hatua za kawaida.
Mkali huyo wa 'AJe' alisema haya kwenye kipindi cha Planet bongo ya East Africa Radio na kusisitiza kuwa yeye kusaini mkataba na kampuni ya ‘Sony Music’ jambo kubwa sana katika maisha yake ya muziki.
“Kiukweli toka nimerudi rasmi kwenye game na kutoa wimbo wa Mwana mashabiki walipokea vizuri sana Africa Mashariki, na kadili nilivyokuja kutoa wimbo mwingine wa Chekecha walizidi kuongezeka mashabiki na kujiona nina mashabiki wengi, hivyo kuja kusaini mkataba na ‘Sony Music’ ndani ya muda mfupi hivi kwangu mimi najiona ni kama nimepiga msamba maana siyo hatua za kawaida” alisema Alikiba.
Mbali na hilo Alikiba alimuombea msanii Diamond Platnum kwa watanzania na Afrika Mashariki kwa ujumla ili wampigie kura kwenye tuzo anazoshiriki sasa na kusema kuwa yeye ndiye msanii pekee anayeiwakilisha Afrika Mashariki kwenye mashindano hayo hivyo watanzania wampigie kura ili aweze kushinda.
eatv.tv
Habari Zingine
- Timbulo: SIjarejea kwenye ualimu
- Vijana wazidi kujitokeza usaili wa Maisha Plus East Africa, Dar es salaam yatia fora
- RAPPER WA CAMEROON, NGOMA AACHIA VIDEO YA WIMBO MPYA ‘ALL LES DAY’, AIELEZEA COLLABO YAKE NA RAY VANNY
- New Hit: Lady Jay Dee – Sawa Na Wao
- Madonna atembelea makazi duni ya Kibera, Nairobi
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :