Ni ngumu kuamini ila huu ndio ukweli wenyewe

Posted in
No comments
Saturday, May 14, 2016 By danielmjema.blogspot.com

Kuna vitu vinatokea kwenye ulimwengu wa soka ambavyo wakati mwingine ni vigumu sana kwa mtu kuamini kama kweli yanatokea. mengine ukiambiwa unaweza ukadhani ni ndoto au stori za abunuasi lakini ukweli ni kwamba yametokea na bado yanaendelea kuwaumiza watu vichwa.


Katika kujaribu kukujuza na kukuondolea mfadhaiko, SAUTI KUU inakuletea mambo kumi ambayo ni vigumu kuamini kama yametokea katika ulimwengu huu wa soka.

  1. Thierry Henry hajawahi kunyakua tuzo ya Ballon Do’r.
  1. Arsenal hawajawahi kunyakua taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya.
  1. Uholanzi hawajawahi kubeba Kombe la Dunia pamoja na kuingia fainali mara tatu.
  1. Kocha Arsene Wenger amemfunga Jose Mourinho mara moja katika mechi 14.
  1. Liverpool ndiyo timu iliyofanikiwa sana kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya zaidi ya PSG, Chelsea na Manchester City kwa pamoja ambapo Liverpool wametwaa taji hilo mara tano na Chelsea moja, City na PSG hawajawahi kunyakua taji hilo.
  1. Mshambuliaji wa PSG, Zlatan Ibrahimovic na mlinda mlango wa Juventus, Gianlugi Buffon, hawajawahi kunyakua taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya, lakini mlinda mlango, Jose Manuel Pinto, ametwaa taji hilo. Pinto alibeba taji hilo mara mbili akiwa Barcelona msimu wa 2008–09 na 2010–11.
  1. Kiungo Ricardo Kaka ana tuzo ya Ballon Dor lakini gwiji wa Argentina, Diego Maradona hana. Kaka alinyakua tuzo hiyo mwaka 2007.
  1. Real Madrid wamenyakua mataji 10 ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, lakini wamebeba taji la La Liga na hilo la Ulaya mara moja ndani ya miaka 10.
  1. Arsenal ndiyo timu pekee kubwa Ulaya yenye taji la ligi la dhahabu (Ligi Kuu England), walinyakua taji hilo baada ya kumaliza msimu mzima bila ya 2003/2004 bila ya kufungwa.
10. Aston Villa wana mataji mengi ya Ligi Kuu England zaidi ya Manchester City, ambapo wamenyakua mataji matano msimu wa 1960–61, 1974–75, 1976–77, 1993–94 na 1995–96. Wakati City wamefanya hivyo mara nne msimu wa 1969–70, 1975–76, 2013–14 na 2015–16.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .