Pallegrini aeleza sababu za kushindwa kutwaa Ubingwa
Posted in
Michezo
No comments
Tuesday, May 17, 2016
By
danielmjema.blogspot.com
Baada ya klabu ya Manchester City kumaliza msimu ikiwa nafasi ya nne katika msimamo wa Ligi Kuu Uingereza, kocha ambaye alikuwa anafundisha klabu hiyo Manuel Pellegriniameweka wazi tatizo lililoifanya klabu hiyo kufanya vibaya msimu huu tofauti na msimu uliopita.
Manuel ameweka wazi kuwa kitendo cha uongozi wa Man City kuweka wazi kuwa klabu hiyo itakuwa na kocha mpya msimu ujao, kimechangia kudhoofisha timu, Guardiola alitangazwa na Man City kuwa atamrithi Pellegrini mwezi February, kitu ambacho kilifanya timu kupoteza morali katikati ya msimu.
“Nilitaka kuchukua Ubingwa wa Ligi Kuu Uingereza msimu huu, lakini uongozi wa klabu ulipoamua kutangaza hadharani ujio wa kocha mpya, mambo yote yalibadilika ikiwemo morali kwa wachezaji, tulipoteza mechi mbili muhimu tukiwa nyumbani, wakati ambao tulikuwa tuna tofauti ya point tatu na anae ongoza” alisema Pellegrini
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :