Rais Kenyatta azindua mpango wa kuunganisha Stima katika Nyumba 18,290 Vijijini, ifikapo Juni

Posted in
No comments
Saturday, May 28, 2016 By danielmjema.blogspot.com

Katika juhudi za kuhakikisha kuwa Taifa la Kenya linakuwa na Mwanga, Rais Uhuru Kenyatta, Alasiri ya leo (28.5.2016) amezindua mpango wa kusambaza nishati ya Umeme (Stima) kwa wananchi wanaoishi katika maeneo ya vijijini, The Last Mile Connectivity Project.

Akizungumza na wananchi wa kaunti ya Kiambu, Rais Kenyatta amesema Seriakli yake inajizatiti kuhakikisha takribani familia zipatazo 18,290, zinafikiwa na huduma ya stima kufikia mwezi Juni mwaka huu. Tizama matukio katika picha hapa chini.

Rais Kenyatta akiwasha Stima katika moja ya Nyumba ya wakazi wa Kiambu walionufaika na mpango huo.
Rais Akisalimiana na akina Mama
Rais Kenyatta akionesha kweli yeye ni mtu wa watu. hapa anafurahia jambo na mtoto wa moja ya familia iliyonufaika na mpango wa stima vijijini.
Wananchi wenye furaha katika kaunti ya Kiambu, wakimuaga Rais Kenyatta kwa kumpa zawadi ya mua, baada ya kukamilisha zoezi ya kuwapa nuru ya stima.


Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .