Ruto awataka Viongozi wa Upinzani kuacha Kelele, asema Seriakli ina Imani na IEBC

No comments
Saturday, May 28, 2016 By danielmjema.blogspot.com

Makamu wa Rais, William Ruto, amewataka wakenya kupuuza 'kelele' za Upinzani, kwa Serikali ya Jubilee haitotishika na kuongeza kuwa Viongozi wa Upinzani wanatumia maandamano 'sideshows' hayo kujiweka katika chati kuelekea uchaguzi mkuu ujao utakaofanyika mwaka 2017. 
 “Viongozi wa upinzani wanapiga kelele kwa sababu wameshitukia kushindwa katika uchaguzi mkuu ujao," alisema Ruto
Akizungumza katika sherehe ya kutoa zawadi, iliyofanyika jana, katika shule ya Sekondari ya wasichana ya Kahuhia, Kaunti ya Muranga, Ruto alisema Serikali ina imani na IEBC na kusisitiza kuwa tume hiyo itaendesha uchaguzi wa huru na haki.
  “Hamuwezi kuwadanganya Wakenya kuwa hauna imani na IEBC, Bunge na Serikali, kwani nyinyi huwa mna imani na kitu chochote? Sio kile anachokisema Rais wala Naibu wake, ni kile ambacho sheria inachoelekeza," alisema Ruto.
Chanzo: Daily Nation

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .