Balala: Maandamano ya kupinga IEBC zinaweza kuathiri Sekta ya Utalii

No comments
Saturday, May 28, 2016 By danielmjema.blogspot.com


Waziri wa Utalii, Najib Balala ametahadharisha kuwa maandamano yanayofanywa na Muungano wa Upinzani nchini Kenya (CORD), dhidi ya Tume huru ya Uchaguzi (IEBC), yanaweza yakaathiri sekta ya utalii ambayo inaanza kujiimarisha kutokana na anguko la miaka miwili.
Balala alisema matukio ya wafuasi wa CORD kuvamia maduka, kuharibu magari na ubebaji wa silaha, ni baadhi ya mambo ambayo yanaichafua taswira ya Kenya, katika uso wa kimataifa na soko la Utalii duniani.
Waziri huyo alisema binafsi hana tatizo na kile kinachofanywa na CORD, lakini viongozi wa Upinzani wanapaswa kuendesha maandamano ya amani badala ya kuwachochea wafuasi wao kufanya vurugu.
“Katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, Sekta ya Utalii nchini imekuwa katika hali ya kujikongoja huku hoteli nyingi katika pwani ya Kenya yakiathirika pakubwa huku wahudumu wa hoteli wapatao 30,000 wakikosa ajira," Alisema Balala na kuongeza
“Serikali imefanya kazi kubwa kufufua sekta ya Utalii, lakini vurugu vinavyotokana na maandamano ya kuipinga IEBC, vinaweza vikatuathiri na kurudisha nyuma juhudi hizi, Ni ulimbukeni kwa watu kutumia vurugu, hatuwezi kuvumilia hali hii iendelee kutokea na viongozi wa Upinzani wanaohusika katika vurugu hizi wanapaswa kuchukuliwa hatua za kisheria," alionya
Waziri Balala alitoa kauli hiyo, siku ya jana, Ijumaa, Mei 27, 2016, katika eneo la Diani, baada ya kushuhudia uzinduzi wa Hillpark Amare Resort, iliyojengwa kwa gaharama ya zaidi ya shilingi milioni 200.

Chanzo:Daily Nation

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .