Prezzo akanusha kujihusisha na madawa ya kulevya

Posted in
No comments
Saturday, May 28, 2016 By danielmjema.blogspot.com

Rapper mkali wa humu nchini, Jackson Makini, 'Prezzo' amekanusha kutumia madawa ya kulevya kama ambavyo kumekuwepo na minong’ono hiyo kwa muda mrefu.

Prezzo ambaye yupo katika ziara za kikazi nchini Tanzania, ameyasema hayo katika mahojiano na kituo kimoja cha Redio nchini humo kuwa hajihusishi na madawa ya kulevya na kukonda kwake kumetokana na yeye mwenyewe kutaka awe hivyo.

Prezzo yuko Tanzania kwa ajili kufanya collabo na hitmaker wa ‘Siwezi’ Barakah Da Prince katika studio za Fish Crub chini ya producer Lamar. Amesafiri na producer na mshkaji wake, Sappy.
Akiongea na huku akionesha dhahiri akiwa amekula chupa mbili tatu za ulabu (kitu ambacho anadai ni uchovu na usingizi kutokana na kuwa busy kwenye tour), Prezzo alisema kuwa binadamu watamsema vyovyote atakavyokuwa awe mwembamba au mnene.
Siku za hivi karibuni rapper huyo maarufu kwa pamba, ambaye aliwahi kuliteka soko la muziki Afrika mashariki na nyimbo kama vile 'Naleta Action' na 'Mahewa' ameonekana kutulia zaidi huku akimtambulisha mpenzi wake Michelle.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .