Serikali ya Kenya yaingia kandarasi ya ujenzi/ukarabati wa kilomita 435.5 za Barabara kote nchini

No comments
Saturday, May 28, 2016 By danielmjema.blogspot.com

Serikali ya Kenya, jana (Ijumaa, Mei 27, 2016) ilisaini kandarasi ya kujenga takribani kilomita 435.5 za  barabara kwa kiwango cha lami, ikiwa ni sehemu ya programu ya kupandisha hadhi za barabara zake katika kipindi cha miaka miwili.
Kajiado, Kwale, Isiolo, Wajir, Taita Taveta, Nakuru, Nyandarua, Samburu, Narok, Kericho na Bomet ni baadhi ya maeneo yatakayonufaika na mpengo huo uliopitishwa na Waziri wa Ujenzi, Mwezi machi, mwaka huu chini ya ushirikiano kati ya Serikali na sekta binafsi (PPPP).
Waziri wa Usafiri na Ujenzi, James Macharia tayari ameshakabidhi awamu ya kwanza ya kandarasi hiyo kwa Mwenyekiti wa kampuni ya Intex Construction, Kishan Gilot huku akisisitiza kwamba Serikali haitavumilia uzembe wowote katika utekelezaji wa Programu hiyo na kuongeza kwamba vigezo vyote lazima vizingatiwe ili kuwawezesha Wakenya kunufaika na uwekezaji huo.
Kampuni hiyo (Intex Construction Company), inatarajia kuanza ujenzi na ukarabati wa jumla ya kilomita 91.5 za barabara ya Ngong – Kiserian – Isinya na barabara ya Kajiado - Imaroro, katika kaunti ya Kajiado, katika kipindi cha miaka miwili na kuzikarabati kwa kipindi cha mwongo mmoja.
Barabara nyingine ambazo nazo zipo katika mpango wa ujenzi/ukarabati ni pamoja na barabara ya Lamu - Garsen, Kakamega – Ingotse - Namukoye - Nzoia River - Musikoma, Kimaeti - Malakisi – Lwakakha, Shikhendu-Endebess na Barabara ya Ugunja - Ukwala hadi Ruambwa.
Mamlaka inayosimamia barabara vijijini, pia itasimamia ukarabati wa Modogashe-Habaswein-Wajir (Kilomita 143) na Barabara ya Illasit-Njukini-Taveta(Kilomita 67) huku ile inayosimamia Ujenzi/ukarabati wa Barabara mijini (KURA), ikiwa na jukumu la kusimamia ujenzi na ukarabati wa barabara zote katika miji ya Nakuru,Maralal,Ol Kalou,Kericho,Bomet na Narok.

Chanzo: Daily Nation

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .