Hii ndio taarifa ya Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania kuhusu uzimaji wa Simu feki kesho.
Posted in
afrika mashariki
No comments
Wednesday, June 15, 2016
By
danielmjema.blogspot.com
Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) yenye dhamana ya kusimamia shughuli za Mawasiliano ya Kielektroniki wametoa tamko la mwisho kwa wananchi wanaoendelea kutumia simu bandia ambazo matumizi ya simu hizo hazijakizi kiwango maalumu.
Akizungumza na Waandishi wa Habari, Meneja Mawasiliano wa TCRA, Innocent Mungi alisema ifikapo kesho (JUni 16) simu zote feki hazitafanya kazi na kwamba Mamlaka hiyo imejipanga kwa ajili ya zoezi hilo.
"Siku ya tarehe 16 ya mwezi huu simu zote bandia hazitafanya kazi katika Network za Tanzania, kuna maswali kwamba zitazimwa vipi kiujumla ni kwamba kila simu imetengenezwa na kupewa namba maalum kila kifaa chochote cha mawasiliano ambayo inaitambulisha simu ni aina gani," Innocent Mungi na kuongeza
‘Kwahiyo cha kimsingi kuanzia saa sita usiku kuamkia tarehe 16 mwezi huu kitakachotokea simu zote zile ambazo hazijakidhi kiwango basi hazitaweza kufanya kazi kwa muda huo kwasababu ni bandia," alisema
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :