Rais Uhuru Kenyatta amesisitiza kuwa atazingatia sheria katika kutatua swala la IEBC

No comments
Friday, June 3, 2016 By danielmjema.blogspot.com

Rais Uhuru Kenyatta amesisitiza kuwa erikali yake itazingatia Sheria dhidi ya msukumo wa Upinzani unaomtaka kutengua uteuzi wa Makamishna wa Tume huru ya Uchaguzi nchini (IEBC).
Rais Kenyatta alisema hatounga mkono hoja yoyote inaylenga kuvunja Katiba ya nchi. "Niliapa kulinda Katiba yetu na nitafanya hivyo, sio swala la lipi ni zuri kwako bali ni kuhusu swala la kitaifa," alisema Rais Kenyatta.
Rais Kenyatta aliyasema hayo mapema leo katika hafla ya kuliombea taifa, lililofanyika katika Hoteli ya Safari Park. Ibada ya kuliombea Taifa huandaliwa na Bunge kila mwaka na hii ni mara ya 14 kuandaliwa.
Rais Kenyatta alisema nguvu nyingi ilitumika kupigania Katiba hii, kwa hiyo itaendelea kuwa na manufaa kwa wote bila kubagua na kuongeza swala la msingi ni kutafuta namna ya kuboresha maisha ya Wakenya lakini sio kuwekeza nguvu nyingi katika mambo ambayo tayari Katiba imeshayatolea ufafanuzi.
Kwa upande Naibu wa Rais, William Ruto alisema Seriakli itaangalia njia nzuri ya kushughulikia swala la IEBC, lakini akaongeza kuwa anaimani uchaguzi mkuu ujao utakuwa wa huru, haki na wa Amani.
Naye Spika wa Bunge la Taifa, Justin Muturi alitoa wito kwa Wakenya kuwa 'vyombo vya amani, umoja kwa ajili ya maendeleo ya Taifa'

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .