Bondia wa zamani, Mohammed ALLY amefariki Dunia

No comments
Saturday, June 4, 2016 By danielmjema.blogspot.com

Bondia wa zamani Mohammed Ali ‘The Greatest’ ambaye ni miongoni mwa watu maarufu na wenye wapenzi wengi duniani, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 74. Mohammed Ali alikutwa na umauti mapema leo, kutokana na kupata tatizo katika mfumo wa upumuaji.

Bingwa huyo wa dunia wa uzani wa juu wa zamani alilazwa hospitalini toka siku ya alhamisi June 02 2016 kufuatia tatizo kwenye mapafu. Mbali na kupatwa na tatizo hilo, 'The Legendary' Mohammed Ali alikuwa akiugua kiharusi. Itakumbukwa pia kuwa akiwa katika ubora wake wa hali ya juu katika masumbwi, Ali alilazimika kustaafu ngumi za kulipwa baada ya kupatikana na ugonjwa wa Parkinson mwaka wa 1984.


Hali ya Mohammed Ali ambaye alikuwa akiishi katika Jimbo la Arizona, nchini Marekani, ilibadilika ghafla juzi (Juni 02) na kulazimka kukimbizwa Hopitali ambapo kwa mujibu wa maelezo ya msemaji wa Familia, Bob Gunnell, Bondia huyo alitarajiwa kupata matibabu na kurejea lakini hali haikuwa hivyo.



“He is being treated by his team of doctors and is in fair condition. A brief hospital stay is expected. At this time, the Muhammad Ali family respectfully requests privacy,” yalisema maelezo yake.

"Mungu Ailaze roho ya Bingwa 'The greatest' Mohammed Ali pema Peponi"



Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .