Showing posts with label Tanzia. Show all posts
Showing posts with label Tanzia. Show all posts

Mbunge wa chama cha Leba Uingereza auawa

Mbunge wa chama cha Leba Uingereza auawa

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com
Mbunge wa chama cha Leba nchini Ungereza Jo Cox amefariki dunia baada ya kupigwa risasi mara tatu na kuchomwa kisu akiwa katika eneo la bunge kaskazini mwa uingereza.
Cox ndiye mbunge wa kwanza kuuawa nchini Uingereza tangu Ian Gow auawe mwaka 1990, Mwanamme mmoja mwenye umri wa miaka 52 aliyetajwa na majirani kama mtu asiye na marafiki amekamatwa na silaha kupatikana.

Hivi ndivyo Mohammad Ali alivyopumzishwa, watu 14,000 walihudhuria

Hivi ndivyo Mohammad Ali alivyopumzishwa, watu 14,000 walihudhuria

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com
Familia ya hayati Muhammad Ali ilikusanyika pamoja na umati wa watu unaotajwa kufikia 14000 na kufanya ibada ya pamoja ya saa moja, kwa ajili ya kumuombea Muhammad Ali, ibada ambayo ilihudhuriwa na wake zake pia Khalilah Camacho-Ali na Veronica Porche-Ali.
10
Bondia wa zamani Lennox Lewis
15
Bondia Sugar Ray alikuwepo pia
2-1
Mke wa tatu wa Muhammad Ali ‘Veronica Porche’
1-1
Mke wa pili wa Muhammad Ali ‘Khalilah Camacho’
20
18
13
16
4-1
5-1
6
7
8 (2)
9
12
11
0
3-1

Matukio katika Picha: Ziara ya Marehemu Mohammad Ali alipotembelea Afrika

Matukio katika Picha: Ziara ya Marehemu Mohammad Ali alipotembelea Afrika

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com
Moja ya nukuu zake kuhusu Afrika ni hii >>> ‘Nataka kuiona Afrika na kukutana na Kaka na dada zangu
m2
Nukuu nyingine ya Muhammad Ali baada ya kuja Afrika >>> ‘Nafuraha kuwaambia watu wangu kwamba kuna vitu vingi vya kujionea Afrika zaidi ya Simba na Tembo, hawakuwahi kutuambua kuhusu vitu vizuri vya Afrika kama Vyuo, Hospitali, Maua mazuri’
m3
Nigeria
m6
Muhammad Ali alipoitembelea Misri.
m4
m7
Alipoitembelea tena Misri mwaka 1986 akiwa tayari amebadili dini na kuwa Muislamu.
m9
Kiongozi wa Zaire enzi hizo Mobutu Sese Seko akiwa kwenye picha na watu wengine akiwemo Muhammad Ali ambapo kiongozi huyu aliandaa pambano na kukubali kumlipa kila mpambanaji kwenye pambano aliloandaa kiasi cha Dola za Kimarekani Milioni 5 kila mmoja.
m11
Pambano lililoandaliwa Congo DRC enzi hizo Zaire
m12
Alipoitembelea Sudan mwaka 1988
m10
m13
Mwaka 2005 Muhammad alikutana kwa mara ya kwanza na rais wa zamani wa Afrika Kusini Nelson Mandela
m8
Kinshasa mwaka 1974

Obama kutohudhuria mazishi ya Mohammad Ali, Yatafanyika Ijumaa hii

Obama kutohudhuria mazishi ya Mohammad Ali, Yatafanyika Ijumaa hii

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com

Rais wa Marekani Barrack Obama hatohudhuria mazishi ya marehemu Muhammad Ali siku ya Ijumaa,kulingana na Ikulu ya rais. Ali alifariki Ijumaa iliopita akiwa na umri wa miaka 74 katika hospitali moja huko Phoenix, Arizona.




Viongozi duniani watakuwa miongoni mwa maelfu watakaohudhuria mazishi hayo yatakayofanyika katika eneo la Louisville,Kentucky ambapo Ali alizaliwa.Ikulu ya White House imesema bw Obama na mkewe Ali, Lonnie walizungumza kwa njia ya simu.
Kwa mujibu wa Taarifa zilizoripotiwa na BBC Swahili, miongoni mwa wale watakaohudhuria ni rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan na mfalme Abdullah wa Jordan.
Aliyekuwa bingwa wa ndondi katika uzani mzito duniani Lennox Lewis na muigizaji Will Smith ambaye aliigiza kama Ali ni miongoni mwa wale watakaobeba jeneza lake.

Kocha wa zamani wa Nigeria, Stephen Keshi amefariki Dunia

Kocha wa zamani wa Nigeria, Stephen Keshi amefariki Dunia

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com
Kocha wa zamani wa Nigeria, Stephen Keshi enzi za uhai wake
Nahodha wa zamani na aliyekuwa kocha wa timu ya taifa ya Nigeria Super Eagles, Stephen Keshi amefariki dunia, taarifa za Keshi kufariki dunia zimeingia kwenye headlines kuanzia asubuhi ya June 8, habari ambazo mwanzo ilionekana kama tetesi ila baadae mitandao mikubwa kama The Mirror wa Uingereza ulithibitisha taarifa hizo.
Stephen Keshi na Mkewe Kate (wote Marehemu)
Keshi mwenye umri wa miaka 54 amefariki ikiwa ni miezi michache imepita toka ampoteze mke wake December 2015 Kate aliyekuwa na umri wa miaka 35 kwa ugonjwa wa kansa, taarifa zinazoripotiwa kutoka ndani  ya familia kuwa Keshi hakuwa na dalili zozote za kuumwa ila inaonekana ni kama mtu aliyekuwa na msongo wa mawazo kwa kumpoteza mkewe.
Afrika itamkumbuka Stephen Keshi kwa rekodi yake ya kuwa mwafrika wa pili kufanikiwa kutwaa taji la mataifa ya Afrika akiwa kama mchezaji na baadae kama kocha, wa kwanza kufanya hivyo alikuwa ni Mahmoud El-Gohary wa MisriNigeria pia itamkumbukaStephen Keshi kama kocha pekee mzawa aliyefanikiwa kuwapa Kombe la Mataifa ya Afrika 2013.

Rais Uhuru Kenyatta na Kiongozi wa Upinzani, Raila Odinga wamlilia Mohammed Ali

Rais Uhuru Kenyatta na Kiongozi wa Upinzani, Raila Odinga wamlilia Mohammed Ali

No comments
By danielmjema.blogspot.com
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya na Waziri mkuu wa zamani, Raila Odinga ambaye pia ni kiongozi wa kambi ya Upinzani wamemlilia Bondia wa zamani na Bingwa wa zamani wa uzani wa juu, Mohammad Ali, aliyefariki dunia leo kutokana na tatizo katika mfumo wa upumuaji.
Rais Kenyatta alimtaja 'Lejindari huyo ambaye amewahi kutwaa ubingwa wa juu wa ngumi wa Dunia mara tatu, kama mmoja wa wanamichezo wenye kipaji cha aina yake ambayo ulimwengu wa Michezo umewahi kuwashuhudia.
Katika Taarifa yake, Rais Kenyatta alisema Marehemu Mohammad Ali alikuwa na hali ya kujituma akiwa michezo jambo ambayo imemfanya kuwa wa kipekee na kuongeza kuwa mwanamasumbwi kamwe hatosaha na kuongeza kuwa ataendelea kuwa kivutio kikubwa kwa mabondia wachanga wanaoazimia kufika mbali katika mchezo wa Ngumi.
“Napenda kutuma salamu zangu za rambirambi kwa familia ya Mohammad Ali pamoja, marafiki zake pamoja na ulimwengu wa mchezo wa ngumi,  kwa hakika Dunia imempoteza mwanamichezo mahiri ambaye mchango wake, namna alivyokuwa akijituma na kuwaburudisha mashabiki hautosahaulika," alisema Rais Kenyatta
Kwa upande wake, Waziri mkuu wa zamani ambaye pia ni Kiongozi wa muungano wa Upinzai nchini (CORD) Raila Odinga, aliungana na dunia kuomboleza kifo cha Mwanamichezo huyo ambapo alisema Dunia imempoteza Shujaa wa kweli na mpambanaji wa haki na ubinadamu.
“Kama Bondia, alifanikiwa kuutangaza mchezo wa ngumi, na baada ya hapo alitumia umaarufu huo kuutumia mchezo wa ngumi kuwa chombo cha kupigania haki na usawa, inatia moyo kwamba Ali aliweza kuishi maisha marefu hadi umauti umnamkuta chini ya utawala wa Rais Mwafrika," Alisema Raila.
Bondia huyo mwenye umri wa miaka 74, alifariki dunia katika Hospitali ya Phoenix, mjini Arizona, siku ya Ijumaa kwa mujibu wa Msemaji wa Familia, Bob Gunnell. Ali ambaye amekuwa akisumbuliwa na maradhi ya kutetemeka (Parkinson) kwa zaidi ya miaka 32, alilazwa hopitalini Juni 02, mwaka huu kutokana na tatizo katika mfumo wa upumuaji.

Bondia wa zamani, Mohammed ALLY amefariki Dunia

Bondia wa zamani, Mohammed ALLY amefariki Dunia

No comments
By danielmjema.blogspot.com
Bondia wa zamani Mohammed Ali ‘The Greatest’ ambaye ni miongoni mwa watu maarufu na wenye wapenzi wengi duniani, amefariki dunia akiwa na umri wa miaka 74. Mohammed Ali alikutwa na umauti mapema leo, kutokana na kupata tatizo katika mfumo wa upumuaji.

Bingwa huyo wa dunia wa uzani wa juu wa zamani alilazwa hospitalini toka siku ya alhamisi June 02 2016 kufuatia tatizo kwenye mapafu. Mbali na kupatwa na tatizo hilo, 'The Legendary' Mohammed Ali alikuwa akiugua kiharusi. Itakumbukwa pia kuwa akiwa katika ubora wake wa hali ya juu katika masumbwi, Ali alilazimika kustaafu ngumi za kulipwa baada ya kupatikana na ugonjwa wa Parkinson mwaka wa 1984.


Hali ya Mohammed Ali ambaye alikuwa akiishi katika Jimbo la Arizona, nchini Marekani, ilibadilika ghafla juzi (Juni 02) na kulazimka kukimbizwa Hopitali ambapo kwa mujibu wa maelezo ya msemaji wa Familia, Bob Gunnell, Bondia huyo alitarajiwa kupata matibabu na kurejea lakini hali haikuwa hivyo.



“He is being treated by his team of doctors and is in fair condition. A brief hospital stay is expected. At this time, the Muhammad Ali family respectfully requests privacy,” yalisema maelezo yake.

"Mungu Ailaze roho ya Bingwa 'The greatest' Mohammed Ali pema Peponi"



Ratiba ya shughuli ya kuuaga mwili wa Makongoro Oging

Ratiba ya shughuli ya kuuaga mwili wa Makongoro Oging

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com
Hii ndiyo ratiba ya Shughuli ya kuuaga kwa mwili wa aliyekuwa Mwandishi Mwandamizi wa Gazeti la Uwazi, Makongoro Oging' aliyefariki Mei 21, 2016 baada ya kuugua kwa muda mfupi. Marehemu alikuwa akiendelea kwa matibabu akiwa nyumbani kwake Tabata jijini Dar es Salaam ambapo mauti yalimfika.


Breaking New: Soita Shitanda amefariki Dunia

Breaking New: Soita Shitanda amefariki Dunia

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com
Waziri Mstaafu ambaye aliwahi kuhudumu kama Mbunge wa jimbo la Malava, Soita Shitanda (pichani), amefariki dunia, katika Hospitali ya Nairobi alikokuwa anapatiwa matibabu.

Buriani Makongoro Oging wa Global Publishers, Kuzikwa Rorya, mkoani Mara, nchini Tanzania

Buriani Makongoro Oging wa Global Publishers, Kuzikwa Rorya, mkoani Mara, nchini Tanzania

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com

Makongoro Oging' enzi za uhai wake.
Makongoro (2)
Makongoro Oging’ enzi za uhai wake akimkabidhi msaada wa fedha Kundi Luhende (kushoto) katika Hospitali kuu ya magonjwa ya Saratani ya Ocean Road jijini Dar.
WAFANYAKAZI wa Kampuni ya Global Publishers Ltd, watayarishaji wa magazeti ya Ijumaa Wikienda, Uwazi, Risasi, Amani, Ijumaa na Championi, wamepata pigo kwa kuondokewa na mfanyakazi mwenzao, aliyekuwa Mwandishi Mwandamizi wa Gazeti la Uwazi, Makongoro Oging' aliyefariki jana jioni (Jumamosi) Mei 21, 2016 baada ya kuugua kwa muda mfupi. Marehemu alikuwa akiendelea kwa matibabu akiwa nyumbani kwake Tabata jijini Dar es Salaam ambapo mauti yalimfika. Makongoro (1)
Makongoro Oging' enzi za uhai wake akiwa na wakili Mabere Nyaucho Marando (kushoto).
Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Amana kusubiri taratibu za mazishi na msiba upo nyumbani kwake Tabata- Magengeni jijini Dar es Salaam. Mwili wa marehemu unatarajiwa kusafirishwa kwenda kijijini kwao Wilaya ya Rorya mkoani Mara kwa ajili ya maziko. Bwana alitoa na Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe. Mungu ailaze roho ya marehemu Makongoro mahali pema peponi-Amina. Makongoro (3)
Makongoro Oging’ akiongea na baadhi ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Chuo Kikuu cha Ualimu Chang' ombe, jijini Dar es Salaam walikuwa katika mgomo.

Gwiji wa masuala ya mtangamano EAC afariki

Gwiji wa masuala ya mtangamano EAC afariki

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com
Balozi Ndayiziga katika mojawapo ya warsha ya EAC hivi karibuni. Kulia ni mtaalamu wa habari na mratibu wa mafunzo ya wandishi wa habari EAC, Bw. Sukhdev Chhatbar.

Mkufunzi katika Mafunzo hayo, Balozi  Jeremy Ndayiziga (kushoto enzi za uhai wake) akimkabidhi cheti Mroki Mroki, kutoka Father Kidevu Blog ambaye pia ni Mpigapicha wa Masuala ya Mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki,  kwa kushiriki kikamilifu mafunzo hayo ya masuala ya Mtengamano wa EAC. Anaeshuhudia Katikati ni Elizabeth Wanyoike wa GIZ ambao walifadhili mafunzo hayo na Jumuia ya Afrika Mashariki.
**********
 Na Mtua Salira, EANA
Mshauri Mtaalamu wa muda mrefu wa Masuala ya Mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) Balozi Jeremy Ndayiziga (54) amefariki dunia baada ya kuugua kwa muda mfupi ugonjwa wa kisukari mjini Bujumbura,Burundi.
Balozi huyo raia wa Burundi kwa mujibu wa marafiki wa karibu na ndugu zake alifariki Jumatano wiki iliyopita na anatarajiwa kuzikwa nchini Burundi Jumanne ijayo, Shirika Huru la Habari la Afrika Mashariki (EANA) limeripoti.
Kutokana na hali yake ya afya kuendelea kudorora, Balozi Ndayiziga alilazimika kukatwa mguu wake wa kulia  katika Hopsitali ya Nairobi kutokana kuzidiwa na ugonjwa wa kisukari na hivyo kubaki hospitalini kwa miezi ipatayo minne. Afya yake ilionekana kuimarika kidogo na alikuwa anakaribia kupona.
Mara ya mwisho alionekana makao makuu ya EAC mjini Arusha, Tanzania katikati ya Novemba mwaka huu katika mkutano wa Maofisa Mawasiliano wa EAC.
Jina la Balozi Ndayiziga ni maarufu kwa watendaji wa EAC kutokana na umahiri wake wa uchapaji kazi,uongozi wa busara na kuwa muumini wa itikadi ya Shirikisho la EAC. Ndiye aliyeiongoza nchi yake katika harakati za kujiunga na EAC 2007.

‘’Marehemu Balozi Ndayiziga alikuwa mtu maarufu, mchapakazi mwenzangu na kwa kweli, zaidi ya yote alikuwa rafiki yangu wa karibu sana,’’ alisema Jean Rigi,Katibu Mkuu wa Wizara ya Afrika Mashariki  nchini Burundi na kuongeza kuwa wengi watamkosa na ni pigo kubwa kwa wote wanaopigania kujenga Afrika Mashariki na raia wake.

Mkongwe wa masuala ya habari nchini Tanzania Jenerali Ulimwengu kufuatia taarifa ya kifo hicho alisema: ‘’Nimepata mshtuko mkubwa! Nilijua kwamba alikuwa anaugua lakini nilifikiri kwamba ni jambo la kawaida tu linaloweza kudhibitiwa.

Nimesikitishwa sana kwa sababu alikuwa ni mtu makini na mwalimu mwenye uelewa wa hali ya juu na alikuwa mwakilishi mzuri wa masuala ya mtangamano wa Jumuiya ya Afrika Mashariki.Nilifanya naye kazi kwa karibu sana kwa kipindi cha zaidi ya miaka mitano.’’
Naye mmoja kati wafanyakazi aliokuwa anafanya nao kazi kwa karibu ni Sukhdev  Chhatbar, Mtaalamu wa Masuala ya Habari, ambaye alielezea kusitishwa na kifo Balozi Ndayiziga.

’Tulikuwa tunawasiliana vyema katika uekelezaji wa miradi mbalimbali.Alikuwa mtu maarufu, mwenye msimamo thabiti,mwenye busara na alikuwa tayari kufanya lolote kuimarisha mchakato wa mtangamano wa kikanda,’’ alisema Chhatbar, mwandishi wa habari maarufu aliyekuwa anasafiri na kusimamia miradi ya pamoja ya EAC na marehemu Balozi huyo katika nchi wananchama wa jumuiya.
Marehemu ameacha mjane na watoto wanne.

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .