Rais Uhuru Kenyatta na Kiongozi wa Upinzani, Raila Odinga wamlilia Mohammed Ali

No comments
Saturday, June 4, 2016 By danielmjema.blogspot.com

Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya na Waziri mkuu wa zamani, Raila Odinga ambaye pia ni kiongozi wa kambi ya Upinzani wamemlilia Bondia wa zamani na Bingwa wa zamani wa uzani wa juu, Mohammad Ali, aliyefariki dunia leo kutokana na tatizo katika mfumo wa upumuaji.
Rais Kenyatta alimtaja 'Lejindari huyo ambaye amewahi kutwaa ubingwa wa juu wa ngumi wa Dunia mara tatu, kama mmoja wa wanamichezo wenye kipaji cha aina yake ambayo ulimwengu wa Michezo umewahi kuwashuhudia.
Katika Taarifa yake, Rais Kenyatta alisema Marehemu Mohammad Ali alikuwa na hali ya kujituma akiwa michezo jambo ambayo imemfanya kuwa wa kipekee na kuongeza kuwa mwanamasumbwi kamwe hatosaha na kuongeza kuwa ataendelea kuwa kivutio kikubwa kwa mabondia wachanga wanaoazimia kufika mbali katika mchezo wa Ngumi.
“Napenda kutuma salamu zangu za rambirambi kwa familia ya Mohammad Ali pamoja, marafiki zake pamoja na ulimwengu wa mchezo wa ngumi,  kwa hakika Dunia imempoteza mwanamichezo mahiri ambaye mchango wake, namna alivyokuwa akijituma na kuwaburudisha mashabiki hautosahaulika," alisema Rais Kenyatta
Kwa upande wake, Waziri mkuu wa zamani ambaye pia ni Kiongozi wa muungano wa Upinzai nchini (CORD) Raila Odinga, aliungana na dunia kuomboleza kifo cha Mwanamichezo huyo ambapo alisema Dunia imempoteza Shujaa wa kweli na mpambanaji wa haki na ubinadamu.
“Kama Bondia, alifanikiwa kuutangaza mchezo wa ngumi, na baada ya hapo alitumia umaarufu huo kuutumia mchezo wa ngumi kuwa chombo cha kupigania haki na usawa, inatia moyo kwamba Ali aliweza kuishi maisha marefu hadi umauti umnamkuta chini ya utawala wa Rais Mwafrika," Alisema Raila.
Bondia huyo mwenye umri wa miaka 74, alifariki dunia katika Hospitali ya Phoenix, mjini Arizona, siku ya Ijumaa kwa mujibu wa Msemaji wa Familia, Bob Gunnell. Ali ambaye amekuwa akisumbuliwa na maradhi ya kutetemeka (Parkinson) kwa zaidi ya miaka 32, alilazwa hopitalini Juni 02, mwaka huu kutokana na tatizo katika mfumo wa upumuaji.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .