Mke wa Rais, Mama Margaret Kenyatta, azindua Kampeni Okoa Tembo (Ivory belongs to Elephant)

No comments
Saturday, June 4, 2016 By danielmjema.blogspot.com

Mke wa Rais wa Kenya, Mama Margaret Kenyatta, amezindua Kampeni kabambe ya kupambana na yenye lengo la kuokoa Tembo. Kampeni hiyo iliyopewa jina la Ivory belongs to Elephant' inaendeshwa na taasisi ya The East Africa Grass-Root Elephant Education Campaign, itahusisha matembezi ya hiari kwa lengo la kupaza sauti dhidi ya uwindaji Haramu ya Tembo.
Akizungumza kabla ya kuzindua matembezi hayo katika sherehe iliyofanyika kwenye ukumbi wa mikutano ya Kenyatta International Convention Centre (KICC), Mama Margaret alipongeza juhudi zinazofanyika kwa lengo la kuokoa Tembo.
Alisema inatia moyo kuona watu binafsi na mwananchi wa kawaida wakichukua jukumu la kupambana na uwindaji haramu wa meno ya Tembo.
Mke wa Rais alitumia fursa hiyo kumpongeza Mkurugenzi mtendaji wa Kituo cha Elephant Neighbours, Jim Nyamu, ambaye anaongoza harakati ya kuwalinda Ndovu na Faru.
Alisema kuihusisha jamii katika ngazi za chini zauhifadhi wa wanyama pori kutasaidia kuleta amani na mshikamano kati ya jamii hizo na wanyama na hivyo kupunguza migogoro kati ya bianadamu na wanyama pori.
Kwa habari zaidi Tembelea: citizentv.co.ke

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .