Buriani Makongoro Oging wa Global Publishers, Kuzikwa Rorya, mkoani Mara, nchini Tanzania
Posted in
Tanzia
No comments
Monday, May 23, 2016
By
danielmjema.blogspot.com
Makongoro Oging' enzi za uhai wake.
Makongoro Oging’ enzi za uhai wake akimkabidhi msaada wa fedha Kundi Luhende (kushoto) katika Hospitali kuu ya magonjwa ya Saratani ya Ocean Road jijini Dar.
WAFANYAKAZI wa Kampuni ya Global Publishers Ltd, watayarishaji wa magazeti ya Ijumaa Wikienda, Uwazi, Risasi, Amani, Ijumaa na Championi, wamepata pigo kwa kuondokewa na mfanyakazi mwenzao, aliyekuwa Mwandishi Mwandamizi wa Gazeti la Uwazi, Makongoro Oging' aliyefariki jana jioni (Jumamosi) Mei 21, 2016 baada ya kuugua kwa muda mfupi.
Marehemu alikuwa akiendelea kwa matibabu akiwa nyumbani kwake Tabata jijini Dar es Salaam ambapo mauti yalimfika.
Makongoro Oging' enzi za uhai wake akiwa na wakili Mabere Nyaucho Marando (kushoto).
Mwili wa marehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Amana kusubiri taratibu za mazishi na msiba upo nyumbani kwake Tabata- Magengeni jijini Dar es Salaam.
Mwili wa marehemu unatarajiwa kusafirishwa kwenda kijijini kwao Wilaya ya Rorya mkoani Mara kwa ajili ya maziko.
Bwana alitoa na Bwana ametwaa, jina lake lihimidiwe.
Mungu ailaze roho ya marehemu Makongoro mahali pema peponi-Amina.
Makongoro Oging’ akiongea na baadhi ya wanafunzi wa mwaka wa kwanza wa Chuo Kikuu cha Ualimu Chang' ombe, jijini Dar es Salaam walikuwa katika mgomo.
Habari Zingine
- Obama kutohudhuria mazishi ya Mohammad Ali, Yatafanyika Ijumaa hii
- Kocha wa zamani wa Nigeria, Stephen Keshi amefariki Dunia
- Mbunge wa chama cha Leba Uingereza auawa
- Hivi ndivyo Mohammad Ali alivyopumzishwa, watu 14,000 walihudhuria
- Matukio katika Picha: Ziara ya Marehemu Mohammad Ali alipotembelea Afrika
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :