Wetangula awatuhumu Wabunge wa Jubilee kupanga kuvuruga maandamano ya Leo

Posted in
No comments
Monday, May 23, 2016 By danielmjema.blogspot.com

Kiongozi mwenza wa mrengo wa CORD, Moses Wetangula amewahusisha Wabunge watatu kutoka mrengo wa Jubilee na jaribio la kuvuruga maandamano ya amani yanayofanyika leo, mjini Jijini Nairobi kupinga uwepo wa maafisa wa IEBC ofisini.
Kiongozi huyo wa Ford Kenya, alisema maandamano yao yamekuwa ya amani ukiacha matukio machache ya vijana waliokodiwa kuingilia maandamano na kusababisha vurugu.
"Kesho (Leo), kutakuwa na maandamano ya aina hiyo katika miji ya Mombasa, Kakamega na Bungoma kuonesha uzito wa madai yao dhidi ya IEBC, tumewajulisha Polisikabla ya kuanza kuwa tutakuwa na maandamano kila Jumatatu kwa hiyo wanapaswa kutulinda na sio kutupiga na Teargas," alisema Wetangula.  
Wetangula alimtuhumu Mbunge wa Starehe, Maina Kamanda, Moses Kuria (Gatundu South) na Mbunge wa Dagoretti kusini, Dennis Waweru ambao wanafanya kazi chini ya mwavuli wa GEMA, akidai wamekuwa wakiuhamasisha umma na vijana wakorofi kuvuruga maandamano yao.
Wetangula alisema kuwa Wabunge hao pia wamekuwa wakiwatumia vijana hao (Hooligans), kuwarushia mawe ambapo katika maandamano yaliyopita ni wao waliohusiska kusababisha vurugu.
“Hatujihusishi na Siasa za ukabila ambayo kwa sasa zinatumiwa na watu wa Jubilee, ambao wanajiita GEMA, tunahisi kuwa serikali inahusika pia katika mipango ya hawa watu (wabunge) kuvuruga maandamano yetu ili tuonekana tunapenda fujo," alisema
Aidha kiongozi huyo wa CORD, alisema wanapanga kuwafungulia kesi wabunge hao endapo wataendelea kuwavurugia maandamano yao huku akiwaonya Polisi kutotumia nguvu wakati wa maandamano hayo ya kupinga IEBC.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .