Kocha wa zamani wa Nigeria, Stephen Keshi amefariki Dunia

Posted in
No comments
Wednesday, June 8, 2016 By danielmjema.blogspot.com

Kocha wa zamani wa Nigeria, Stephen Keshi enzi za uhai wake
Nahodha wa zamani na aliyekuwa kocha wa timu ya taifa ya Nigeria Super Eagles, Stephen Keshi amefariki dunia, taarifa za Keshi kufariki dunia zimeingia kwenye headlines kuanzia asubuhi ya June 8, habari ambazo mwanzo ilionekana kama tetesi ila baadae mitandao mikubwa kama The Mirror wa Uingereza ulithibitisha taarifa hizo.
Stephen Keshi na Mkewe Kate (wote Marehemu)
Keshi mwenye umri wa miaka 54 amefariki ikiwa ni miezi michache imepita toka ampoteze mke wake December 2015 Kate aliyekuwa na umri wa miaka 35 kwa ugonjwa wa kansa, taarifa zinazoripotiwa kutoka ndani  ya familia kuwa Keshi hakuwa na dalili zozote za kuumwa ila inaonekana ni kama mtu aliyekuwa na msongo wa mawazo kwa kumpoteza mkewe.
Afrika itamkumbuka Stephen Keshi kwa rekodi yake ya kuwa mwafrika wa pili kufanikiwa kutwaa taji la mataifa ya Afrika akiwa kama mchezaji na baadae kama kocha, wa kwanza kufanya hivyo alikuwa ni Mahmoud El-Gohary wa MisriNigeria pia itamkumbukaStephen Keshi kama kocha pekee mzawa aliyefanikiwa kuwapa Kombe la Mataifa ya Afrika 2013.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .