Nyani Azima Umeme nchini Kenya kwa masaa Manne
Posted in
afrika mashariki
No comments
Wednesday, June 8, 2016
By
danielmjema.blogspot.com
Kampuni ya kuzalisha umeme nchini Kenya, KENGEN imetuma taarifa kwa vyombo vya habari ikiomba radhi kwa ukosefu wa umeme Kwa hapo jana.
Mara kwa mara umeme hupotea nchini Kenya kwa sababu moja au nyengine, sawa tu na mataifa yote barani Afrika
Hata hivyo sababu walioitoa KENGEN kwa ukosefu huo wa umeme Kwa takriban saa nne kote nchini humo ndio imewaacha wengi wamepigwa na butwaa !
Amini usiamini, KENGEN imempata nyani mmoja katika eneo maalum lenye 'swichi' hiyo katika mtambo wa kuzalisha umeme ulioko kwenye bwawa kuu la Gitaru Mashariki mwa Kenya. Sasa kampuni hiyo inasema huenda nyani huyo ndiye aliyezima umeme kote nchini Kenya!
Kengen inasema kuwa huenda nyani huyo aliangukia mashine hiyo ndogo na ''kusababisha hitilafu ya takriban megawati 180 za umeme ambao ndio uliosababisha ukosefu wa umeme kote nchini Kenya.''
Kwa takriban saa nne taarifa hiyo ilielezea.Tumbili huyo alinusurika na sasa amechukuliwa na shirika la huduma kwa wanyama pori KWS ilikupokea matibabu.
"mitambo ya kuzalisha umeme kote nchini Kenya huwa imezingirwa na nyaya za umeme ilikuwazuia wanyama wa porini kuingia humo na kusababisha madhara kama hayo ya jana , taarifa hiyo ilisema.
''Tunaomba radhi kwa tukio hilo la kipekee la hapo jana na sasa tumeanza kuweka mikakati dhabiti ya kuzuia marudioa ya ajali hiyo'' taarifa hiyo ya KenGen ilielezea.
Mashirika mengi pamoja na wawekezaji wa kibinafsi walilazimika kufunga biashara zao hapo jana huku wale waliokuwa na nitambo binafsi za kuzalisha umeme wakiingia gharama zaidi ya kununua mafuta .
Wakenya wengi waliopokea habari hizo waliikejeli kampuni hiyo ya kuzalisha umeme wengi wakiwatania katika mitandao ya kijamii.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :