Ruto: Sihusiki na kifo cha Jacob Juma, niko tayari kuhojiwa

No comments
Wednesday, June 8, 2016 By danielmjema.blogspot.com

KUFUATIA kuwepo kwa taarifa zinazomhusisha Naibu wa Rais, William Ruto na kifo cha Mfanyabiashara maarufu nchini, Jacob Juma, aliyeuwawa na watu wasiojulikana, Ruto ameibuka na kuvunja ukimya kwa kusema kuwa hahusiki na kifo hicho na kusisitiza kuwa yuko tayari kuhojiwa na maafosa wa usalama.
Jacob Juma aliuwawa kwa kumiminiwa Risasi Saba na kisha mwili wake kukutwa kwenye gari lake, Mnamo May 6, mwaka huu. Akizungumza katika mahojiano maalum na 'The Big Question' ya 'Citizen TV',  Ruto alisema hahusiki kwa lolote na kifo cha Juma na kuongeza kuwa yuko tayari kuhojiwa katika ofisi ya Mpelelezi mkuu wa Serikali (DCI) endapo atatakiwa kufanya hivyo.
Jina la Naibu la Naibu wa Rais limekuwa likitajwa mara kwa mara ambapo kuna taarifa ambazo bado hazijathibitshwa kwamba siku chache kabla ya Kifo chake, Juma aliandika ujumbe kwenye ukurasa wa mtandao wa Twitter, akisema kuwa Ruto alikuwa anamtishia maisha yake.


Marehemu Jacob Juma enzi za uhai wake
 Aidha kuhusu madai ya Cyrus Jirongo kuhusu uhusika wake katika kifo hicho, Ruto alisema madai hayo hayana msingi wowote na kumtaka Jirongo kutoa ushahidi huku akiongeza kuwa hizo ni mbinu za kambi ya upinzani za kutaka kuchafua jina lake
"Hivi karibuni kumekuwa na tabia ya kunigeuza 'Punching Bag' upinzani wanatumia jina langu kama fimbo ya kujiweka sawa kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2017, siasa zao ni za kuchafuana na sio siasa za kujadili maswala ya kitaifa," alisema

Gari la Marehemu Jacob Juma

Ruto alisema uchunguzi kuhusu chanzo cha Kifo cha Juma zinaendelea na wote waliohusika lazima watakamatwa.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .