China yarejesha chombo cha Marekani
Posted in
Kimataifa
No comments
Tuesday, December 20, 2016
By
danielmjema.blogspot.com
Marekani imethibitisha kwamba China imerejesha chombo cha baharini ambacho kilikuwa kimetwaliwa kutoka kwenye bahari ya South China Sea.
Kutwaliwa kwa chombo hicho kulikuwa kumetishia kuvuruga uhusiano kati ya Marekani na Uchina. Chombo hicho ni cha kufanya utafiti baharini.
Maafisa wa Pentagon wanasema chombo hicho kisicho na nahodha kilisalimishwa kwa maafisa wa Marekani karibu na pahala ambapo kilitwaliwa, kilomita 92 kaskazini magharibi mwa Ghuba ya Subic.
Taarifa ya Marekani imesema maafisa wake wataendelea "kupaa, kuendesha vyombo vya baharini, na kuhudumu katika bahari ya South China Sea" maeneo yanayoruhusiwa na sheria za kimataifa.
Baada ya kutwaliwa kwa chombo hicho, Rais Mteule wa Marekani Donald Trump aliituhumu China kwa kutekeleza wizi. Baadaye, alipendekeza China waruhusiwe kukaa na chombo hicho.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :