Showing posts with label Kimataifa. Show all posts
Showing posts with label Kimataifa. Show all posts

Ujerumani yamtafuta mshukiwa raia wa Tunisia

Ujerumani yamtafuta mshukiwa raia wa Tunisia

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com
Rais wa Ujerumani, Joachim Gauck
Polisi wanamtafuta raia wa Tunisia anayeshukiwa kuhusika katika shambulizi kwenye soko la Krismasi mjini Berlin. Mshukiwa huyo anafahamika kwa vyombo vya usalama kama gaidi ambaye ombi lake la uhamiaji lilicheleweshwa.

Shirika la habari la Ujerumani, dpa, limemtaja mshukiwa huyo kuwa ni Anis A, likizinukuu duru za usalama. Mshukiwa huyo anachukuliwa na idara ya ujasusi ya Ujerumani kama mtu hatari ambaye yuko tayari kufanya vitendo vya kigaidi wakati wowote.
Gazeti la Allgemeine Zeitung limeripoti kuwa hati za uhamiaji za raia huyo wa Tunisia mwenye umri wa miaka 21 zilipatikana ndani ya lori lililotumika kufanyia shambulizi hilo na anafahamika na maafisa wa usalama kwa kuhusika katika makosa mengine matatu.
Duru nyingine ya usalama imeliambia shirika la dpa kwamba polisi wameanza operesheni inayohusiana na shambulizi hilo katika jimbo la North Rhine Westphalia, magharibi ya Ujerumani. Gazeti la Ujerumani, Bild, limeripoti kwamba mtu huyo amesajiliwa katika mji wa Cleves, mji mdogo katika jimbo hilo katika mpaka na Uholanzi. Waziri wa mambo ya ndani wa jimbo la North Rhine Westphalia amesema mshukiwa aliishi Berlin kuanzia Februari mwaka huu.
Serikali yathibitisha
Waziri wa mambo ya ndani wa Ujerumani, Thomas de Maiziere, alithibitisha kuwepo kwa mshukiwa mpya. "Kuna mshukiwa mpya na anatafutwa. Ningependa kusema, kama wengine wote walivyosema: Huyu ni mshukiwa tu na sio lazima awe muhusika aliyefanya shambulizi. Uchunguzi ungali unaendelea katika kila upande. Kila kitu kinachunguzwa na mshukiwa huyu amekuwa katika orodha ya watu wanaotafutwa tangu usiku wa kuamkia leo."
Hata hivyo waziri de Maiziere amekataa kuthibitisha mara moja taarifa kadhaa za vyombo vya habari kwamba mshukiwa huyo ni mhamiaji kutoka Tunisia mwenye mafungamano na makundi yenye misimamo mikali ya kidini.  De Maiziere na mkuu wa idara ya ujasusi Hans-Georg Maassen wamefanya mazungumzo kuhusu hatua za kiusalama kufuatia shambulizi hilo katika kikao cha dharura cha kamati ya bunge inayoshughulikia masuala ya ndani.
Wakati haya yakiarifiwa, rais wa Ujerumani Joachim Gauck aliwatembelea baadhi ya wahanga wa shambulizi la Jumatatu katika hospitali ya Charite mjini Berlin. Gauck alisema amefaulu kukutana na mwanamume aliyeangukiwa na mlingoti alipokuwa akimsaidia mtu mwingine aliyejeruhiwa.
Rais Gauck alisema, "Ziara yangu ni ishara kwamba mamilioni ya watu nchini kote wanafuatilia kujua hatma ya wahanga na wale walio katika hali mahututi, pamoja na wale wenye nafasi nzuri ya kupona kabisa. Wasihisi wako peke yao na kwamba mbali na madaktari hapa, watu kote Ujerumani wana matumaini na wanawasubiri wapone."
Soko la Krismasi lililoshambuliwa linatarajiwa kufunguliwa LEO Alhamisi.

Msichana aliyetengwa kwa kuwa na hedhi nchini Nepal afariki

Msichana aliyetengwa kwa kuwa na hedhi nchini Nepal afariki

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com
Maafisa wa polisi huko Nepal wanachunguza kifo cha msichana wa miaka 15 aliyefukuzwa hadi katika mtaa wa mabanda kwa kutokwa na hedhi. Wanasema kuwa msichana huyo alikosa hewa na kufariki baada ya kuwasha moto ili kupata joto. 
Chini ya tamaduni za Hindu kwa jina Chhaupadi, wanawake walio na hedhi ama ambao wamejifungua huonekana kuwa wachafu. Tamaduni hiyo ilipigwa marufuku na serikali ya Napoli mwaka 2005, lakini bado inaendelea kutekelezwa katika maeneo ya mashambani yaliopo magharibi.
Mwili wa Roshani Tiruwa ulipatikana na babake wikendi iliopita katika jiwe na nyumba moja ya matope katika kijiji cha Gajra, Wilayani Accham yapata kilomita 440 magharibi mwa Kathmandu.
Baadhi ya jamii katika maeneo ya mashambani zinaamini kwamba watakabiliwa na janga baya iwapo wanawake walio katika hedhi hawatatengwa. Huku wakiwa wametengwa hunyimwa chakula chao cha kila siku na hawaruhusiwi kunywa maziwa.

Mchele wa plastiki wakamatwa nchini Nigeria

Mchele wa plastiki wakamatwa nchini Nigeria

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com
Nigeria imekamata magunia 102 ya ''mchele wa plastiki'' yaliyokuwa yanaingizwa nchini humo na wafanyabiashara haramu ambao walitaka kuuza katika msimu huu wa sherehe, kulingana na afisa wa forodha katika mji mkuu wa nchi hiyo , Lagos.
Uchunguzi wa awali ulibaini kuwa mchele huo ulikuwa ni wa "plastiki'' ,baada ya kuuchemshwa, na kuoneka kuwa mkubwa zaidi ya mchele wa kawaida na ni Mungu tu anajua ni nini ambacho kingetokea kama ungeliwa na binadamu ", Haruna Mamudu aliongeza katika kauli yake juu ya tukio hilo.
Aliwawaonya wahujumu wa uchumi ambao wanangalia kipindi hiki cha sherehe kama njia za kupata mapato kwa udanganyifu kuwa watakabiliwa na mkono wa sheria. Bwana Mamudu hakuelezea ni vipi mchele huo wa plastiki ulitengenezwa lakini ulikua na nembo iliyoandikwa "Best Tomato Rice".
Uchunguzi unaendelea kutambua ni kiwango gani cha mchele huo kimekuwa kikiuzwa na ni vipi unaweza kuondolewa sokoni ili kulinda afya za raia wa Nigeria waliokwisha utumia na kuwapeleka wahusika wa biashara hiyo haramu mbele ya sheria".
Nchini Uchina, kuliwahi kuwa na sakata ya chakula mwaka jana baada ya kubainika kuwa kuwepo kwa mchele uliotengenezwa kwa plastiki.
BBC

Rais wa Gambia agoma kung'ooka madarakani

Rais wa Gambia agoma kung'ooka madarakani

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com
Rais wa gambia Yahya Jammeh ameonya kuwa atakataa jaribio lolote la viongozi wa kieneo kumlazimisha kuondoka madarakani licha ya kushindwa katika uchaguzi na mfanyibiashara Adama Barrow. Akihutubia wanachama wa muungano wa Bar Afrika nchini humo Bw Jammeh alisema:
 ''Waje wajaribu kuniondoa.wanasubiri nini? mimi ni mtu mpenda amani lakini haimaanishi kwamba sitalitetea taifa langu, kwa ujasiri na uzalendo na kuibuka mshindi''. Amesema kuwa alikataa wito wa muungano wa viongozi wa mataifa ya Magharibi ECOWAS akiwemo rais Muhammadu Buhari wa Nigeria na Ellen Johnson Sirleaf wa Liberia kuondoka nchini Gambia. Akiongezea:
 ''Wao ni kina nani wa kuniambia mimi niondoke nchini mwangu. Amewashtumu viongozi hao kwa kuingilia a ya ndani ya Gambia. ECOWAS tayari imesema kuwa inamtambua bw Barrow kama rais wa taifa hilo na kwamba litachukua hatua zozote kuhakikisha kuwa matokeo ya uchaguzi yanaheshimiwa.
Viongozi wa kieneo watahudhuria kuapishwa kwa Bw Barrow mnamo mwezi Januari 18 kulingana na taarifa ya Ecowas. Rais Jammeh awali alikuwa amekubali matokeo ya uchaguzi huo manamo tarehe mosi mwezi Disemba ,lakini baadaye akaitisha uchaguzi mpya utakaoandaliwa na tume ya uchaguzi inayomcha mungu. Alisema kwamba matokeo hayo uchaguzi yaligubikwa na dosari.
BBC

utulivu warejea DR Congo

utulivu warejea DR Congo

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com
Hali ya utulivu imerejea katika barabara za mji mkuu wa Kinshasa pamoja na zile za miji mingine muhimu nchini DR Congo kufuatia maandamano. Kiongozi wa upinzini nchini humo Etienne Tshisekedi , amewataka wafuasi wake kuipinga serikali ya rais Joseph Kabila .
Zaidi ya watu 20 wameuawa katika ghasia baada ya muhula wa Kabila kukamilika siku ya Jumatatu usiku huku uchaguzi ukiwa umeahirishwa hadi 2018. Kanisa katoliki linatarajiwa kuendeleza mazungumzo kati ya upinzani na muungano wa kitaifa.
Mwandishi wa BBC mjini Kinshasa anasema kuwa kanisa linaheshimiwa sana nchini humo kwa miongo kadhaa na kwamba mazungumzo hayo huenda yakatuliza hali ya wasiwasi iliopo iwapo upinzani na serikali hawataafikiana
BBC

Idadi ya waliofarika kwa kunywa sabuni Urusi yafikia 58

Idadi ya waliofarika kwa kunywa sabuni Urusi yafikia 58

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com
Idadi ya watu waliofariki baada ya kunywa sabuni wakidhania ni pombe imefikia watu 58 kutoka 49 kulinga na vyombo vya habari nchini Urusi. Wengi wa watu 37 walioathirika bado wanaendelea kutibiwa huku wengine wakiwa katika hali mahututi. 
Raia hao walikunywa maji ya sabuni yaliokuwa na sumu kali wakidhania ilikuwa pombe kulingana na kamati ya uchunguzi ya Urusi. Lakini maji hayo yalikuwa na kemikali ya Ethanol inayoweza kusababisha upofu.

Mlipuko wauwa watu 26 Mexico

Mlipuko wauwa watu 26 Mexico

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com
Takribani watu 26 wamekufa na wengine kadhaa kujeruhiwa kutokana na mlipuko mkubwa wa moto uliotokea katika Soko la fataki San Pablito kilomita 36 nje kidogo ya mji wa Mexco city.
Wingu zito la moto kutokana na mlipuko huo katika soko la fataki la San Pabito, Umesababisha watu kuchanganyikiwa na kukimbia huku na kule kwa lengo la kujiokoa.
Picha za video zilizorushwa katika televishen nchini humo zimeonyesha anga la soko hilo likiwa limeunikiwa na wingu refu la moto. Makundi ya uokoaji yamefika katika eneo la tukio kutoa msaada,na watu wametahadhalishwa kutosogea katika eneo hilo na barabara kuachwa wazi.
Gavana wa eneo hilo Eruviel Avila amesema kuwa kwa sasa nguvu kubwa imeelekezwa kusaiia majeruhi na watoa huduma wa serikali wamepelekwa katika eneo hilo. Mashuhuda wa tukio hilo wanasema kuwa idadi ya milipuko iliendelea ada ya mlipuko wa kwanza na hatimaye oshi mkubwa na moto ukafunika anga.
Rais wa Mexico, Enrique Pena Nieto,kupitia ukurasa wake wa weeter ametoa pole kwa familia zilizopoteza wapendwa wao kutokana na mlipuko huo na majeruhi
Soko hilo la fataki la San Pablito mwaka 2005 lilikumbwa kasa kama huo,pale mfulilizo wa milipuko na moto mkubwa ulipozuka wakati taifa ilo liijiandaa kwa sherehe za uhuru.

China yarejesha chombo cha Marekani

China yarejesha chombo cha Marekani

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com
Marekani imethibitisha kwamba China imerejesha chombo cha baharini ambacho kilikuwa kimetwaliwa kutoka kwenye bahari ya South China Sea.
Kutwaliwa kwa chombo hicho kulikuwa kumetishia kuvuruga uhusiano kati ya Marekani na Uchina. Chombo hicho ni cha kufanya utafiti baharini.
Maafisa wa Pentagon wanasema chombo hicho kisicho na nahodha kilisalimishwa kwa maafisa wa Marekani karibu na pahala ambapo kilitwaliwa, kilomita 92 kaskazini magharibi mwa Ghuba ya Subic.
Taarifa ya Marekani imesema maafisa wake wataendelea "kupaa, kuendesha vyombo vya baharini, na kuhudumu katika bahari ya South China Sea" maeneo yanayoruhusiwa na sheria za kimataifa.
Baada ya kutwaliwa kwa chombo hicho, Rais Mteule wa Marekani Donald Trump aliituhumu China kwa kutekeleza wizi. Baadaye, alipendekeza China waruhusiwe kukaa na chombo hicho.

Watu 12 wafa katika shambulio la lori

Watu 12 wafa katika shambulio la lori

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com
Wakati wakristo kote Duniani wakijiandaa na sikukuu ya Krisimasi, huko nchini Ujerumani watu 12 wamefariki dunia baada ya lori kuacha njia na kuelekea katika soko maarufu kwa maandalizi ya Krisimasi katikati ya mji wa Berlin.
Taarifa za awali za serikali ya Ujerumani zimeeleza kuwa tukio hilo ni la makusudi. Pamoja na kusababisha vifo vya watu tisa,lakini Lori hilo pia limejeruhi watu 50 baada ya kuingia katika soko hilo lenye mkusanyiko mkubwa wa watu.
Waziri wa mambo ya ndani wa Ujerumani Thomas de Maiziere, amesema kuna kila dalili kwamba tukio hilo huenda ni la kupangwa na kwamba Polisi wanaendelea na uchunguzi.
Hata hivyo Polisi wamesema kuwa wanachunguza kufuatia gari lililosababisha maafa hayo kudaiwa kuwa lilikuwa na namba za usajili za polisi na kwamba lilibiwa katika jengo ambalo kulikuwa na kazi ya ujnezi huko Poland.
Msemaji wa idara ya zima moto mjini Berlin, Sven Gerling, amesema walishtushwa na kile walicho kiona katika eneo la tukio. Nao Mashuhuda wa tukio hilo wamesema kuwa waliliona lori hilo likielekea katika viunga vya soko hilo kwa kasi karibu na kanisa la kumbukumbu ya Kaisari Wilhelmo.
Polisi wamefanikiwa kumkamata mtu wanayedhani alikuwa akiendesha gari hilo ambapo abiria aliyekuwa ndani ya gari hilo na ambaye hajafahamika mara moja alikufa katika ajali hiyo.
BBC

Trump aahidi Marekani kujitoa kwenye biashara na Pasifiki

Trump aahidi Marekani kujitoa kwenye biashara na Pasifiki

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com

Rais mteule wa Marekani Donald Trump amesema kuwa siku yake ya kwanza madarakani atatoa tamko la kujiondoa katika mpango wa biashara ya ubia ya nchi za Pasifiki.
Katika ujumbe wa video Ufupisho mipango yake kwa ajili ya siku yake ya kwanza ,alisema ingekuwa badala yake kujadili mikataba ya biashara ya pande mbili ili kuleta ajira na viwanda kurudi Marekani.
Trump amesema atajikita kwenye kukatisha vizuizi vya makaa ya mawe na kuendeleza mpango wa kulinda miundombinu muhimu. Ushirikiano wa nchi za Pasifiki ulisainiwa mwezi Februari baada ya miaka saba ya mazungumzo na ilikuwa msingi wa sera ya biashara ya Rais Obama.
Chanzo: BBC

Tetemeko lasababisha kimbunga Fukushima, Japan

Tetemeko lasababisha kimbunga Fukushima, Japan

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com
Tetemeko la ardhi la nguvu ya 7.4 kwenye vipimo vya Richter limekumba maeneo ya Fukushima na Miyagi nchini Japan na kusababisha kimbunga chenye mawimbi ya urefu wa zaidi ya mita moja.
Tetemeko hilo limetokea mwendo wa saa kumi na mbili asubuhi saa za Japan (21:00 GMT Jumatatu), idara ya utabiri wa hali ya hewa ya Japan (JMA) imesema. Wakazi walishauriwa kukimbilia maeneo yaliyo juu upesi, huku mawimbi yakihofiwa kufikia urefu wa mita 3.
Kulikuwa na taarifa za watu kadha kupata majeraha madogo pamoja na uharibifu kutokea. Tetemeko jingine lilitokea eneo hilo mwaka 2011 na kusababisha kimbunga ambapo watu zaidi ya 18,000 walifariki.
Tetemeko hilo, moja ya mitetemeko mikubwa zaidi kuwahi kushuhudiwa, liliharibu kinu cha nyuklia cha Fukushima. Hadi sasa, shughuli kubwa ya kuondoa taka za nyuklia imekuwa ikiendelea. Maafisa wa serikali wanasema hakujakuwa na dalili zozote za uharibifu kwenye kinu hicho wakati huu.
Maafisa wa Jiolojia wa Marekani awali walikuwa wamekadiria nguvu ya tetemeko hilo kuwa 7.3 lakini baadaye wakapunguza hadi 6.9, kipimo ambacho ni cha chini kuliko kile kilichotolewa na wenzao wa Japan.
Idara ya utabiri wa hali ya hewa ya Japan inasema tetemeko la sasa linauhusiano na tetemeko la mwaka 2011. Msemaji mmoja aliyenukuliwa na Japan Times amesema eneo hilo limekuwa likipokea tetemeko la 7.0 angalau mara moja kila mwaka.
Kina cha tetemeko la Jumanne kinakadiriwa kuwa kilomita 30 chini ya ardhi (maili 18.6), JMA imesema. Mitetemeko mikubwa imesikika maeneo ya mbali yakiwemo mji mkuu New York ulio maili 100 kusini mwa Fukushima. Nyumba katika mji huo zilitikisika kwa karibu sekunde 30.
Japan huwa eneo linaloathiriwa sana na mitetemeko ya ardhi ambapo asilimia 20 ya mitetemeko ya ardhi ya nguvu ya 6.0 kwenda juu duniani hutokea eneo hilo. Japan huwa eneo linaloathiriwa sana na mitetemeko ya ardhi ambapo asilimia 20 ya mitetemeko ya ardhi ya nguvu ya 6.0 kwenda juu duniani hutokea eneo hilo.

PAPA FRANCIS ASOGEZA MBELE SWALA LA KUSOMEHEWA KWA WAAVYA MIMBA

PAPA FRANCIS ASOGEZA MBELE SWALA LA KUSOMEHEWA KWA WAAVYA MIMBA

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com
Kiongozi wa kanisa katoliki duniani Papa Francis amesogeza mbele kwa muda usiojulikana suala la mapadre wa kikatoliki duniani kusamehe wanawake walitoa mimba.
Mwaka jana aliwaruhusu mapadre kufanya hivyo kwa kipindi ambacho kilitajwa kama mwaka wa huruma ya Mungu kilichoisha Jumapili iliyopita.
Hapo awali maaskofu peke yao ndio waliokuwa na uwezo wa kuwasamehe wanawake waliotoa mimba.
Baba mtakatafu amesisitiza kwamba mafundisho ya kikatoliki yanaonyesha kwamba utoaji mimba ni kosa kubwa, lakini kiongozi huyo ameeleza kwamba Mungu ni mwenye huruma na anaweza kusamehe dhambi zote ikiwa mkosaji atatubu.
Kiongozi huyo wa kanisa katoliki duniani amesema anaelewa jinsi suala la utoaji wa mimba linavyoweza kuwa tatizo kimaadili kwa mwanamke.
Chanzo: BBC

Obama: Sitanyamaza wakati wa utawala wa Trump

Obama: Sitanyamaza wakati wa utawala wa Trump

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com
Rais wa Marekani anayeondoka Barack Obama amesema huenda akazungumza, kinyume na utamaduni wa siasa Marekani, iwapo mrithi wake Donald Trump atatishia "maadili muhimu" ya Marekani.
Huwa desturi kwamba marais wa zamani wa Marekani huwa hawajiingizi sana katika siasa baada ya kuondoka madarakani na huwa hawazungumzi kuhusu warithi wao.
Akiongea katika kikao na wanahabari wakati wa mkutano wa nchi za Asia na Pasifiki (Apec) mjini Lima, Peru, Bw Obama amesema anakusudia kumsaidia Bw Obama na kumpa muda wa kueleza maono yake. Lakini amesema kwamba, kama raia, huenda akalazimika kuzungumza kuhusu baadhi ya mambo.
"Ninataka kuiheshimu afisi na kumpa rais mteule fursa ya kueleza msimamo wake na mipango yake bila mtu kujitokeza kumkosoa," Bw Obama alisema. Lakini akaongeza, kwamba iwapo suala "litagusa maadili muhimu ya Marekani na imani yetu, na nafikiri kwamba inahitajika au itafaa kwangu kutetea maadili hayo, badi nitalitathmini wakati huo". Kisha, amejieleza kama "raia wa Marekani anayejali sana taifa".
Akiongea katika kikao cha wanahabari wakati wa kufungwa kwa mkutano mkuu wa viongozi wa Apec, Bw Obama amesisitiza kwamba ataonyesha utaalamu kwa kundi la Bw Trump wakati wa mpito sawa na ilivyofanyika kwa kundi lake wakati wa kuondoka kwa mtangulizi wake George W Bush.
Bw Bush, tangu aondoke madarakani, amejizuia kuzungumzia utawala wa Bw Obama. "Sidhani hilo linasaidia kwa vyovyote," aliambia CNN mwaka 2013, baada ya Obama kuchaguliwa kwa mara ya pili.
"Ni kazi ngumu. Ana mambo mengi ya kushughulikia kwenye ajenda yake. Rais wa zamani hafai kuyafanya mambo kuwa magumu zaidi kwake. Marais wengine wa zamani wamechukua uamuzi tofauti; huu ni wangu."
Msimamo wa Bw Bush unafuata desturi, ambapo maras wa Marekani huwa wanajiepusha kuwakosoa watangulizi au warithi wao. Bw Obama alisema wazi kwamba hataingilia msimamo wa Bw Trump kabla ya muhula wake kumalizika Januari mwakani.
Lakini ufafanuzi wake kwamba, atakapokuwa raia wa kawaida, atatettea "maadili muhimu", ameutoa huku kukiendelea kuwa na wasiwasi miongoni mwa makundi ya kutetea haki za kiraia kuhusu watu wanaoteuliwa na Bw Trump kushikilia nyadhifa kuu katika serikali yake.
Mwanamikakati mkuu wa Bw Trump, Steve Bannon, alikuwa awali mkuu wa Breitbart, tovuti ambayo imetuhumiwa kwa kuendeleza ubaguzi wa rangi na chuki dhidi ya Wayahudi. Na mshauri mkuu wa masuala ya usalama wa taifa wa Bw Trump, Jenerali Michael Flynn, alikuwa awali amefananisha Uislamu na "saratani" ambayo inaenea Marekani.
Mwanasheria mkuu aliyeteuliwa na Bw Trump, Jess Sessions, alizuiwa kuhudumu kama jaji wa dola mwaka 1986 kwa sababu ya kutoa matamshi ya ubaguzi wa rangi. Bw Obama amesema anaamini majukumu makuu ya urais yatamlazimu Bw Trump kulegeza baadhi ya sera zake kali ambazo alizitetea wakati wa kampeni.
'Kushindwa kwa Democratic'
Alipoulizwa kuhusu kushindwa kwa chama cha Democratic chini ya Hillary Clinton, Bw Obama alikosoa kampeni zilizolenga "makundi fulani", badala ya kukumbatia taifa lote.
Bi Clinton amekosolewa kwa kuangazia sana watu wa jamii fulani, wakiwemo Walatino na wanawake, ambao waliaminika kumuunga mkono badala ya watu wote.
Njia kama hiyo "haitakusaidia kushinda uungwaji mkono wa watu wengi kama inavyohitajika," Bw Obama alisema na kuongeza kwamba chama hicho kilihitaji "ujumbe bora zaidi".

Chanzo: BBC

Afrika imefikia hapa katika mpango wake wa kutumia passport moja kwa nchi zake zote

Afrika imefikia hapa katika mpango wake wa kutumia passport moja kwa nchi zake zote

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com
pass
Wazo hili limezaliwa ndani ya ule mfumo huru wa safari za ndani ya bara la Ulayaambapo nchi zake zote hufanya safari bila visa ndani ya bara hilo. Mpaka sasa nchi 13 za Afrika zina mikataba ya safari za bila visa kwa nchi nyingine za ndani yaAfrika, ambapo raia wake usafiri bila ya visa ama kupokea visa wanapowasili.
Viongozi wa nchi za Afrika watakapokutana Kigali Rwanda July 2016 watakuwa miongoni mwa watu wa kwanza kutumia passport hizo za kielektroniki. Lengo ni kurahisisha safari za ndani ya Afrika na inaaminika pia biashara za ndani zitaimarika na kukuza uchumi kwa ujumla pia kuimarisha ujamaa na mahusiano mazuri baina ya nchi hizo.

Mke wa Rais Obama, avutiwa na ubunifu wa Mbunifu kutoka Kenya

Mke wa Rais Obama, avutiwa na ubunifu wa Mbunifu kutoka Kenya

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com
Mkewe rais wa Marekani Michelle Obama amemsifu mjasiria mali kutoka Kenya mwanzilishi wa kampuni inayotengeza biadhaa za watoto bi Wanjiru Waithaka Waweru.
Katika dhifa ya jioni iliyoandaliwa kwa heshma ya wanawake bi Wanjiru Waithaka Waweru, ambaye ni mhandisi/Msanifu mijengo ambaye amegusa maisha ya wengi kwa njia yake ya kipekee ya ubunifu wake unaozingatia maslahi ya watoto.
Shirika lake la FunKidz, lilitajwa kama moja ya kupigiwa mfano na kuigwa kote duniani. Funkidz ilikuwa moja kati ya mashirika yanayongozwa na wanawake 10,000 kutoka Afrika Mashariki, mataifa ya Mashariki ya Kati na Kaskazini mwa Afrika yanayotambuliwa na Goldman Sachswhich kwa mchango wao.
Japo Bi Obama alikuwa ni mifano mingi tu ya kusimulia faida ya mikopo kwa wanawake inayotolewa na Goldman Sachs chini ya mpango maalum wa ''10000 Women'' bi Obama alichagua kusimulia kisa cha Wanjiru Waweru ambaye ubunifu wake wa kuunda bidhaa zinazozingatia hadhi ya mtoto mwafrika ni wa kuigwa.
''Ciru anatokea Kenya,,,kwa hivyo yeye ni kama familia kwangu'' Yeye ni mbunifu wa bidhaa za watoto zenye nembo ya Funkidz''''Najua kuwa alikuwa na matatizo mengi mno kupata mtaji wa biashara yake lakini bidhaa zake ziliwavutia wakenya wengi mbali na kina mama kutoka kote barani Afrika '' alisema bi Obama.

Obama ampinga Trump kuhusu kuwazuia Waislamu kuingia Marekani

Obama ampinga Trump kuhusu kuwazuia Waislamu kuingia Marekani

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com
Rais wa Marekani, Barack Obama, ameshutumu vikali matamshi ya mgombea urais kwa tiketi ya chama cha Republican, Donald Trump, kwamba waislamu wasiruhusiwe kuingia Marekani. Obama amesema hiyo 'si marekani wanayohitaji.'
''Kuwabagua Waislamu wa Marekani kutasababisha nchi hiyo kukosa usalama,na kuongeza tofauti iliopo kati ya nchi za magharibi na zile za kislamu'', Obama alisema
Siku ya Jumatatu bwana Trump, aliongezea kuhusu mpango wa kupiga marufuku nchi zote ambazo zina historia ya kutekeleza mashambulizi dhidi ya Marekani.
Alisema shambulio la ufyatuliaji risasi la Orlando linathibitisha yote.
Watu 49 waliuawa, baada ya Omar Mateen raia wa Marekani ambaye wazazi wake ni raia wa Afghan kufyatua risasi katika kilabu ya wapenzi wa jinsia moja huko Orlando.
Bwana Trump amesema pendekezo lake litatekelezwa kupitia (uamuzi wa pamoja ) iwapo rais atapewa mamlaka ya kupiga marufuku uingizaji wa watu wenye daraja lolote katika nchi hiyo jambo ambalo rais ataliona kuleta madhara ya kiusalama kwa Marekani.
Lakini siku ya Jumanne katika wizara ya fedha mjini Washington,Obama aliyekuwa amekasirishwa na matamshi hayo ya Trump alimshambulia mgombea huyo anayetarajiwa kuthibitishwa kuwa mteuzi wa urais wa chama cha Republican mwezi ujao.

waliomtukana Rais uturuki wafikia 2010, Mahakam yamhukumu Miss wa zamani.

waliomtukana Rais uturuki wafikia 2010, Mahakam yamhukumu Miss wa zamani.

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com
turkey 2
Hata nchi ya Tanzania imeshuhudia baadhi ya watu wakipelekwa Mahakamani kwa kumtusi Rais au kuandika habari za uongo kuhusu viongozi wengine wa nchi na hii ni baada ya sheria mpya ya makosa ya mitandao kuanza kufanya kazi.
Huko Uturuki habari nyingine kubwa ni hii ya Mahakama kwenye mji wa Istanbul kumhukumu mshindi wa zamani wa shindano la urembo nchini Uturuki kwa kosa la kumtukana rais wa nchi hiyo Recep Tayyip Erdogan.
Kwa mujibu wa BBC Swahili , Merve Buyuksarac mwenye umri wa miaka 27 alipatikana na hatia ya kumtukana hadharani President wa Uturuki hivyo amehukumiwa kifungo kilichoahirishwa cha miezi 14 gerezani.
Inasemekana pia mrembo huyu aliandika kwenye mtandao wake wa kijamii pamoja na kuwatumia watu shairi lenye matusi katika mtandao wake wa Instagram lakini Wakili wake amesema wamepinga hukumu hiyo katika Mahakama kuu ya bara la Ulaya na Buyuksarac amekanusha madai yote dhidi yake.
uturuki 3
Wanaharakati wa kupigania haki za Binadamu wanasema hiyo kesi ni njia ya serikali ya rais Erdogan kukandamiza uhuru wa kujieleza ambapo hadi sasa watu 2000 wengi wao wakiwa ni Wasanii nyota na hata wanafunzi wameshtakiwa kwa kumkejeli au hata kumtusi Rais huyu tangu mwaka wa 2014.
BBC wameripoti kwamba hukumu hiyo iliahirishwa ilimradi tu asirudie makosa hayo katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

Mabaki ya kiumbe “Naledi”yagunduliwa nchini Afrika Kusini.

Mabaki ya kiumbe “Naledi”yagunduliwa nchini Afrika Kusini.

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com
Wanasayansi nchini Afrika Kusini kwa ushirikiano na Chuo kikuu cha Wits University (University of Witwatersrand) na Taasisi ya utafiti wa anga na viumbe hai (The National Geographic Society) wamebaini mabaki ya mifupa ya kiumbe kinachofanana kwa kiasi kikubwa na binadamu, ambayo yalifukiwa chini ya ardhi zaidi ya miaka milioni iliyopita.
Naledi 00003 SA.Mabaki ya kumbe hicho kilichopewa jina la NALEDI, yamepatikana karibu na Mji wa Johannesburg ambapo Kiumbe hicho kina mikono na miguu kama ya binadamu, ingawa maungo yake ni makubwa.
NALEDI 002
Ukubwa ya ubongo wa kiumbe hicho unashabihiana kabisa na wa binadamu, huku hatua za miguu yake zikionekana kuwa kubwa kidogo kuliko za binadamu.

Mataifa yakutana kuijadili IS nchini Libya

Mataifa yakutana kuijadili IS nchini Libya

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com

Mataifa kadhaa yenye nguvu duniani yanakutana leo katika mji mkuu wa Austria, Vienna kujadili kuongezeka kwa ushawishi wa kundi linalojiita Dola la Kiislamu, IS nchini Libya, ambako ni kitisho kwa Ulaya.

Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, John Kerry (kulia) na mwenzake wa Urusi Segei Lavrov
Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani, John Kerry (kulia) na mwenzake wa Urusi Segei Lavrov
Mkutano huo unaongozwa kwa pamoja na Marekani pamoja na Italia ambayo ni mkoloni wa zamani wa Libya, na ambayo imekuwa ikitaabika kutokana na idadi kubwa ya wahamiaji wanaoingia kwenye ardhi yake, wakitokea Afrika Kaskazini.
Msemaji wa wizara ya mambo ya nchi za nje ya Marekani John Kirby, amesema mkutano huo wa leo utatakafari msaada ya jumuiya ya kimataifa kwa Serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Libya, kwa kuangazia zaidi masuala ya kiusalama.
Wenyekiti wa mkutano huo ni waziri wa mambo ya nchi za nje wa Marekani John Kerry, na mwenzake wa Italia Paolo Gentiloni. Gentiloni amesema kabla ya mkutano huo, kuwa nguvu za pamoja zinahitajika kusaidia mchakato wa kurejesha utulivu nchini Libya.
Uungwaji mkono nje, upinzani ndani
Serikali ya Umoja wa Kitaifa Libya inakabiliwa na upinzani mkubwa ndani ya nchi.
Serikali ya Umoja wa Kitaifa Libya inakabiliwa na upinzani mkubwa ndani ya nchi.
Serikali hiyo inayoongozwa na mfanyabiashara Fayez al-Sarraj inaungwa mkono kimataifa katika juhudi za kuiunganisha tena nchi, lakini inakabiliwa na upinzani wa ndani.
Bado haiungwi mkono na bunge lililochaguliwa nchini humo, na mtu aliyetangaza kuwa mkuu wa majeshi Khalifa Haftar, mshirika wa bunge hilo ambaye ameapa kuyaangamiza makundi ya kiislamu nchini Libya.
Hata serikali kinzani yenye makao mjini Tripoli imekataa kuitambua serikali hiyo ya umoja wa kitaifa.
Katika mazingira hayo ya mgawanyiko, IS imejiimarisha katika eneo linalouzunguka mji wa Sirte kwenye ufukwe wa Mediterania, ambao imeugeuza kituo cha mafunzo kwa wanajihadi kutoka maeneo yote ya karibu na ya mbali.
Tumbo joto kwa Ulaya na Marekani
Wapiganaji wa IS wamejiimarisha katika mji wa Sirte
Wapiganaji wa IS wamejiimarisha katika mji wa Sirte
Ulaya ina wasiwasi kwamba wanajihadi hao ambao wamekuwa wakijikusanya upya, watautumia uwanja wa ndege wa Sirte na bandari ya mji huo, kuanzisha mashambulizi dhidi ya bara la Ulaya.
Hivi karibuni ripoti ya bunge la Uingereza ilisema kuwa operesheni ya Umoja wa Ulaya baharini kupambana na magenge yanayosafirisha watu kimagendo imeshindwa.
Wasiwasi huo unakwenda sambamba na hofu ya Marekani, ambako maafisa wa serikali na wanadiplomasia wamesema ipo mipango ya kufikiria jinsi ya kuiondolea Libya vikwazo vya kuagiza silaha kutoka nje, ambavyo iliwekewa na Umoja wa Mataifa miaka mitano iliyopita.
Afisa mmoja wa ngazi ya juu wa Marekani ameliambia shirika la habari la AFP, kwamba washirika wako tayari kuisaidia serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Libya, ikiwa itatoa maelezo ya kutosha na yenye kueleweka, juu ya namna inavyopanga kupambana na kundi la Dola la Kiislamu.
Maelezo hayo ndio yanayotarajiwa kuzungumziwa na Kerry na wenzake katika mkutano wa Vienna, lakini kuna mashaka ikiwa serikali ya Umoja wa Kitaifa ya Libya itawasilisha mpango kamili wa kutaka usaidizi.
Nguvu zilizotawanywa
Mgawanyiko nchini Libya ulizidi makali hivi karibuni, pale pande mbili zinazopingana, serikali ya Umoja wa Kitaifa, na vikosi vinavyoongozwa na Khalifa Haftar, zilipotangaza mipango ya kupambana na IS, kila upande kivyake.
Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi katika baraza la seneti la Italia Nicola Latorre alisema hali hiyo ni kosa linalopaswa kuzuiliwa, na kuongeza kuwa hawataendelea kuukubali mgawanyiko huo.
Suala jingine litakalojadiliwa katika mkutano wa Vienna ni la wahamiaji haramu wanaoendelea kumiminika Ulaya, na mkuu wa sera za nje wa Umoja wa Ulaya Federica Mogherini amesema atajadili uwezekano wa kurefusha operesheni ya kupambana wa wasafirishaji haramu wa watu hao.
Mwandishi: Daniel Gakuba/afpe
Source: DW Kiswahili

OBAMA KUZURU UJERUMANI LEO (24.04.2016)

OBAMA KUZURU UJERUMANI LEO (24.04.2016)

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com

Rais wa Marekani Barack Obama anatarajiwa kuwasili mjini Hanover, nchini Ujerumani leo Jumapili (24.04.2016) na kuwa na mazungumzo na kansela wa Ujerumani Angela Merkel. Merkel, ni mmoja kati ya washirika wa karibu wa rais Obama katika kupambana na uchumi wa dunia unaoyumba pamoja na mizozo ya kiusalama katika mashariki ya kati na Ukraine.
England Besuch US Präsident Obama beim Town Hall Meeting Rais wa Marekani Barack Obama
Kitakuwa kituo chake cha mwisho katika ziara ya siku sita katika mataifa ya kigeni ambako Obama ametaka kuimarisha ushirika wa Marekani na mataifa washirika mataifa anayoyaangalia kuwa ni muhimu kukuza uchumi, kulishinda kundi la dola la Kiislamu, na kudhibiti mabavu ya Urusi nchini Ukraine na Syria.

Deutschland Barack Obama und Angela Merkel in Baden-BadenBarack Obama na kansela Angela Merkel(kulia)
Obama, ambaye yuko katika miezi yake tisa ya mwisho katika muhula wake wa mwisho wa urais, amekuwa kwa siku tatu mjini London ambako amewataka Waingereza kuchagua kubakia ndani ya Umoja wa Ulaya katika kura ya maoni itakayofanyika mwezi Juni, kura ambayo inaweza kuleta msituko katika uchumi wa dunia.

Maonesho ya biashara
Mapema wiki hii, alikutana na viongozi wa mataifa ya ghuba mjini Riyadh kujaribu kupunguza hofu kwamba Marekani imepunguza msisitizo wake kuhusiana na usalama wao. Mjini Hanover, atazuru na kuzungumza katika maonesho makubwa ya biashara na Merkel. Viongozi hao wanataka kuweka uhai katika makubaliano kati ya Marekani na Umoja wa Ulaya ya biashara huru ambayo wale wanaoyaunga mkono wanasema yataweza kuongeza uwezo wa uchumi wa kila upande kwa kiasi cha dola bilioni 100.

Msukumo wake unakuja katika wakati ambapo watu wengi wa Ulaya na Marekani kwa pamoja wanatia shaka kwamba makubaliano hayo yanaweza kugharimu kazi zao na kuathiri viwango.Deutschland Hannover Proteste gegen TTIP
Waandamanaji wakiingia mitaani mjini Hanover

Makubaliano ya kibiashara
"Lakini muda haumsubiri yeyote katika wakati huu," amesema Heather Conley, afisa wa zamani wa wizara ya mambo ya kigeni ya Marekani katika enzi za utawala wa rais George W. Bush, hivi sasa akiwa katika kituo kwa ajili ya mikakati na mitaala ya kimataifa mjini Washington.
Viongozi wanajaribu kukamilisha mazungumzo tata kuhusu ushirika wa uwekezaji na biashara katika eneo la mataifa hayo yanayotenganishwa na bahari ya Atlantic yaani TTIP kabla Obama, kutoka chama cha Democratic, kuondoka madarakani Januari 20. 

Obama anatokea Uingereza kuja Ujerumani ambako amesema katika mahojiano yaliyotangazwa leo Jumapili na shirika la utangazaji la BBC kwamba makubaliano ya kibiashara kati ya Uingereza na Marekani yanaweza kuchukua miaka mitano hadi kumi kujadili iwapo Uingereza itapiga kura kujitoa katika Umoja wa Ulaya katika kura ya maoni itakayofanyika Juni 23.

Deutschland G7 Gipfel Barack Obama und Angela Merkel Schloss Elmau Obama(kushoto) akizungumza na kansela Merkel(kulia)

Ziara ya Obama na uamuzi ya kuingilia kati katika majadala wa Umoja wa ulaya umeukasirisha upande wa kampeni ya kujitoa, ambayo imekuwa ikidai mara kwa mara kwamba Uingereza inaweza kirahisi kujadili makubaliano na kupata masharti mazuri zaidi ikiwa nje ya Umoja huo.
Mwandishi: Sekione Kitojo / rtre

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .