utulivu warejea DR Congo
Posted in
Kimataifa
No comments
Wednesday, December 21, 2016
By
danielmjema.blogspot.com
Hali ya utulivu imerejea katika barabara za mji mkuu wa Kinshasa pamoja na zile za miji mingine muhimu nchini DR Congo kufuatia maandamano. Kiongozi wa upinzini nchini humo Etienne Tshisekedi , amewataka wafuasi wake kuipinga serikali ya rais Joseph Kabila .
Zaidi ya watu 20 wameuawa katika ghasia baada ya muhula wa Kabila kukamilika siku ya Jumatatu usiku huku uchaguzi ukiwa umeahirishwa hadi 2018. Kanisa katoliki linatarajiwa kuendeleza mazungumzo kati ya upinzani na muungano wa kitaifa.
Mwandishi wa BBC mjini Kinshasa anasema kuwa kanisa linaheshimiwa sana nchini humo kwa miongo kadhaa na kwamba mazungumzo hayo huenda yakatuliza hali ya wasiwasi iliopo iwapo upinzani na serikali hawataafikiana
BBC
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :