Mke wa Rais Obama, avutiwa na ubunifu wa Mbunifu kutoka Kenya
Posted in
Kimataifa
No comments
Friday, June 17, 2016
By
danielmjema.blogspot.com
Mkewe rais wa Marekani Michelle Obama amemsifu mjasiria mali kutoka Kenya mwanzilishi wa kampuni inayotengeza biadhaa za watoto bi Wanjiru Waithaka Waweru.
Katika dhifa ya jioni iliyoandaliwa kwa heshma ya wanawake bi Wanjiru Waithaka Waweru, ambaye ni mhandisi/Msanifu mijengo ambaye amegusa maisha ya wengi kwa njia yake ya kipekee ya ubunifu wake unaozingatia maslahi ya watoto.
Shirika lake la FunKidz, lilitajwa kama moja ya kupigiwa mfano na kuigwa kote duniani. Funkidz ilikuwa moja kati ya mashirika yanayongozwa na wanawake 10,000 kutoka Afrika Mashariki, mataifa ya Mashariki ya Kati na Kaskazini mwa Afrika yanayotambuliwa na Goldman Sachswhich kwa mchango wao.
Japo Bi Obama alikuwa ni mifano mingi tu ya kusimulia faida ya mikopo kwa wanawake inayotolewa na Goldman Sachs chini ya mpango maalum wa ''10000 Women'' bi Obama alichagua kusimulia kisa cha Wanjiru Waweru ambaye ubunifu wake wa kuunda bidhaa zinazozingatia hadhi ya mtoto mwafrika ni wa kuigwa.
''Ciru anatokea Kenya,,,kwa hivyo yeye ni kama familia kwangu'' Yeye ni mbunifu wa bidhaa za watoto zenye nembo ya Funkidz''''Najua kuwa alikuwa na matatizo mengi mno kupata mtaji wa biashara yake lakini bidhaa zake ziliwavutia wakenya wengi mbali na kina mama kutoka kote barani Afrika '' alisema bi Obama.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :