Moses Kuria na wenzake 7 wafikishwa Mahakamani kwa kutoa matamshi ya Uchochezi

No comments
Friday, June 17, 2016 By danielmjema.blogspot.com

WABUNGE nane , ambao walikamatwa hivi majuzi kwa kosa la kutoa kauli za uchochezi na chuki, wamefikishwa Mahakamani leo, katika mahakama ya Milimani na kusomewa mashitaka yanayowakabili.

Wabunge hao kutoka Chama cha Jubilee, kinachoongozwa na Rais Uhuru Kenyatta pamoja na wenzao kutoka Muungano wa vyama vya Upinzani, kinachoongozwa na Waziri Mkuu wa zamani, Raila Odinga, walifikishwa Mahakamani hapo majira ya saa 11:45 asubuhi katika gari la Polisi lengo la kuwafikisha Mahakamani Alfajiri yote hiyo ikiwa ni kuepuka vurugu za wafuasi wao.


Wabunge waliofikishwa Mahakamani ni pamoja na Moses Kuria (Gatundu Kusini), Kimani Ngunjiri (Bahati), Ferdinand Waititu (Kabete), Junet Mohamed (Suna Mashariki), Timothy Bosire (Kitutu Masaba), Aisha Jumwa (Mwakilishi wa wanawake-Kilifi), Florence Mutua (Mwakilishi wa Wanawake-Busia) na Seneta Johnstone Muthama (Machakos), walifungiwa katika Maabusu ya Mahakama ya Mlimaniwere wakisubiri muda wa shughuli za Mahakama zifike.
Wabunge wamekuwa wakishikiliwa katika kituo kidogo cha Polisi cha Pangani na Muthaiga kwa takribani siku tatu sasa tangu walipokamatwa siku ya Jumanne ya Juni 14, mwaka huu kwa kosa la kutoa matamshi ya chuki.


Siku ya jana (Alhamisi), viongozi wa CORD walitishia kuendelea na maandamano iwapo wabunge wao hawataachiwa huru ndani ya masaa 24 bila masharti. Kiongozi wa CORD, Raila Odinga aliituhumu Serikali kwa kukiuka haki za wabunge wanaoshikiliwa kwa kuwanyima fursa ya kuonana na mawakili wao, kuwanyima chakula na badhi ya mataji muhimu.

Kwa upande wake Rais Uhuru Kenyatta, akizungumza kutoka Brussels, Ubelgiji aliko kwa ziara ya siku tatu, alisema serikali haitomvumilia mtu yeyote anayeeneza siasa za chuki bila kujali chama chake.


“Ujumbe wangu ni kwamba, Nikiwa kama Rais wa Kenya, kauli za uchochezi, kutoka kwa yeyote yule, bila kujali ni wa chama gani, haiwezi kuvumiliwa na Serikali yangu na yeyote atakayekutwa akitoa kauli za chuki, sheria itamshughulikia," alisema Rais Kenyatta na kuendelea.

“Nitafanya chochote ndani ya uwezo wangu kama Rais, kuhakikisha taifa la Kenya haliporomoki na wala halielekezwi katika njia hiyo wanayotaka wao, bila kujali wewe ni nani, hakuna Mkenya atakayemshambulia mwenzake kwa misingi ya kikabila au Udini, Kenya inahitaji kusonga mbele," alisema Rais Kenyatta.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .