Showing posts with label Kitaifa. Show all posts
Showing posts with label Kitaifa. Show all posts

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA MKUTANO WA PILI WA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII

MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL AFUNGUA MKUTANO WA PILI WA MIFUKO YA HIFADHI YA JAMII

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua rasmi Mkutano Mkuu wa pili wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, uliofanyika Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, leo Feb 5, 2015.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Kamishina Mstaafu wa TRA, Harry Kitilya, wakati walipokutana baada ya kufungua rasmi Mkutano Mkuu wa pili wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, uliofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, leo Feb 5, 2015.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiagana na Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Burn Ltd, Malaczynski Burn, baada ya kufungua rasmi Mkutano Mkuu wa pili wa Mifuko ya Hifadhi ya Jamii, uliofanyika kwenye Hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam, leo Feb 5, 2015.

KATIBU MKUU KIONGOZI AFURAHISHWA NA UWEPO WA SACCOS MAKAZINI

KATIBU MKUU KIONGOZI AFURAHISHWA NA UWEPO WA SACCOS MAKAZINI

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue (kushoto) akimsikiliza Mshauri Mkuu na Mlezi wa Ikulu SACCOS Bw Joseph Sanga (wa pili kulia) akimuelezea mikakati ya ushirika huo wakati wa hafla fupi ya kumkabidhi kitabu chake cha uanachama wa ushirika huo Ikulu Dar es salaam. Wa pili kushoto ni Makamu Mwenyekiti wa Ikulu SACCOS, Bw. Deodatus Gaudio, akifuatiwa na Katibu wake Bw. Benedicto Damiano na kulia ni Mtunza Hazina Bi. Judith Medson.

Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akipokea kitabu chake cha uanachama toka kwa Makamu Mwenyekiti wa Ikulu SACCOS, Bw. Deodatus Gaudio (wa tatu toka kulia). Wengine ni Katibu wa wa ushirika huo Bw. Benedicto Damiano (wa pili kulia), Mtunza Hazina Bi. Judith Medson ( wapili kushoto) na Mshauri Mkuu na Mlezi wa Ikulu SACCOS Bw Joseph Sanga kulia,wakati wa hafla fupi ya kumkabidhi kitabu chake cha uanachama wa ushirika huo Ikulu Dar es salaam.
Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue akionesha kitabu chake cha uanachama baadas ya kukabidhiwa na Makamu Mwenyekiti wa Ikulu SACCOS, Bw. Deodatus Gaudio wakishuhudiwa na Katibu wa wa ushirika huo Bw. Benedicto Damiano, Mtunza Hazina Bi. Judith Medson ( wapili kushoto) Mshauri Mkuu na Mlezi wa Ikulu SACCOS Bw Joseph Sanga kulia,wakati wa hafla fupi ya kumkabidhi kitabu chake cha uanachama wa ushirika huo Ikulu Dar es salaam.KWA MSAADA WA MICHUZI BLOG

MAMA SALMA KIKWETE AKABIDHI MASHINE YA KUPIMIA SARATANI YA MATITI KWA AKINA MAMA HOSPITALI KUU YA JESHI LUGALO

MAMA SALMA KIKWETE AKABIDHI MASHINE YA KUPIMIA SARATANI YA MATITI KWA AKINA MAMA HOSPITALI KUU YA JESHI LUGALO

Posted in ,
No comments
By danielmjema.blogspot.com
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo,WAMA, Mama Salma Kikwete akitoa hotuba yake muda mfupi kabla ya kukabidhi mashine ya kupimia saratani ta matiti kwa akina mama kwenye Hospitali Kuu ya Jeshi Lugalo. Hafala hiyo ilifanyika kwenye Kitengo cha Uzazi na mtoto cha hospitali hiyo kilichoko eneo la Mwenge hapa Dar tarehe 27.2.2015.
Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania Luteni Jenerali Samuel Ndomba akitoa hotuba wakati wa hafla ya kukabidhi mashine ya kupima saratani ya matiti kwa akina mama katika Hospitali ya Lugalo tarehe 27.5.2015.
Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania Luteni Jenerali Samuel Ndomba akimpongeza Mama Salma Kikwete kwa hotuba yake aliyoitoa kwenye hafla ya kukabidhi mashine ya kupimia saratani ya matiti kwa akina mama kwenye hospitali Kuu ya Jeshi ya Lugalo tarehe 27.2.2015.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA Mama Salma Kikwete akikabidhi mashine ya kupimia saratani ya matiti kwa akina mama kwa uongozi kwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi Luteni Jenerali Samuel Ndomba (kulia). Hafla ya makabidhiano hayo ilifanyika kwenye Hospitani Kuu ya Jeshi Lugalo kwenye Kitengo cha Uzazi na Mtoto kilichoko Mwenge tarehe 27.2.2015. Aliyesimama pembeni kwa Mama Salma ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii Dkt. Donan Mmbando na aliyesimama kulia kwa Mnadhimu Mkuu wa Jeshi ni Mkuu wa Hospitali Kuu ya Jeshi ya Lugal Brigedia Jenerali Josia Mwita Makere.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akisalimiana na Bibi Mariam Omar aliyemshika mtoto wake Jane Winston aliyekuwa akisubirim kupata huduma hospitalini hapo wakati Mama Salma alipotembelea sehemu mbalimbali za Kitengo cha Uzazi na Mtoto mara baada ya kukabidhi mashine ya kupimia saratani ya matiti kwa akina mama tarehe 27.2.2015.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akimshauri Ndugu Peter Charles,28, baba mzazi wa binti Irene mwenye umri wa miezi 3 na mkazi wa Mikocheni kupunguza baadhi ya nguo alizomfunika mtoto wakati hali ya hewa ni ya joto. Mama Salma alimpongeza Ndugu Peter kwa kuambatana na mke wake kwenda kliniki. PICHA NA JOHN LUKUWI

PSPTB YAFANYA SEMINA YA UTAFITI KWA WANAFUNZI WA BODI YA WATAALAMU WA UNUNUZI NA UGAVI

PSPTB YAFANYA SEMINA YA UTAFITI KWA WANAFUNZI WA BODI YA WATAALAMU WA UNUNUZI NA UGAVI

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com

New Picture (88) 

Mr. Godfred Mbanyi, Mkurugenzi wa Mafunzo PSPTB akitoa neno katika ufunguzi wa semina ya utafiti iliyofanyika kwenye ukumbi wa TEC Kurasini Dar es Salaam tarehe 16/2/2015
New Picture (89)
Mkurugenzi wa mafunzo Mr. Godfred Mbanyi akimkaribisha Mkurugenzi mtendaji wa PSPTB Dr. Clemence TEsha kufungua semina ya utafiti katika ukumbi wa TEC Kurasini Dar es Salaam. Tarehe 16/02/2015
New Picture (90) 
Picha ya pamoja ya Mkurugenzi mtendaji wa PSPTB na washiriki wa semina ya Utafiti iliyofanyika Katika ukumbi wa TEC Kurasini Dar es Salaam tarehe. 16/2/2015.
New Picture (91)Mkurugenzi Mtendaji wa PSPTB Dr. Clemence Tesha(aliyeketi katikati), mwezeshaji wa semina Dr. Eli Tumsifu (aliyeketi kushoto) na Mr. Godfred Mbanyi Mkurugenzi wa mafunzo (aliyeketi kulia) katika picha ya pamoja na washiriki wa semina
New Picture (92) 
Washiriki wa Semina ya utafiti wakimsikiliza mwezeshaji Dr. Eli Tumsifu toka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kwenye semina ya utafiti iliyofanyika katika ukumbi waTEC Kurasini Dar es Salaam tarehe. 16-20 Februari 2015
New Picture (93) 
Dr. Eli Tumsifu akiwa na washiriki wa semina ya utafiti ya PSPTB ndani ya ukumbi wa TEC Kurasini Dar es Salaam tarehe 16-20 Februari 2015

Na Mwandishi wa Kijiwe Chetu, Dar es salaam
Bodi ya Wataalam wa Ununuzi na Ugavi PSPTB imeendesha mafunzo kwa wanafunzi wa fani ya ununuzi na ugavi wanaofanya tafiti kama sehemu ya mafunzo yao ya shahada ya Ununuzi na ugavi.

Mafunzo hayo yalifunguliwa tarehe 16 Februari 2015 na Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi Dr. Clemence Tesha, ambaye aliwaasa wanafunzi hao wazingatie mafunzo hayo ili kuongeza ubora wa kazi za utafiti watakazofanya kwa ajili ya kupata shahada ya juu ya ununuzi na ugavi. Aidha, alisisitiza kuwa wanapaswa kuzingatia maadili katika kufanya utafiti, jambo ambalo ndio msingi na matakwa ya Bodi. 

Wanafunzi wanatakiwa kufanya utafiti wao wenyewe na sio kuchukua kazi zilizofanywa na wanafunzi/watafiti wengine au kufanyiwa na watu wengine maana kufanya hivyo ni kuvunja sheria.

Pamoja na kuwajengea uwezo wa kufanya utafiti, pia wanafunzi wanajengewa uwezo wa kujiamini, kuandika ripoti na kujieleza na hata kuwasilisha ripoti katika sehemu zao za kazi. 

Hivyo lengo kuu la semina hii ni kuwajengea uwezo wa kuandika, kujieleza na kutoa huduma bora kwa taifa, kwani ufaulu wa mwanafunzi, unategemea sana uwezo wake wa kuitetea kazi yake, ambapo katika mtihani huo mwanafunzi atawasilisha kazi yake mbele ya wataalam, ili kupima uwezo wake.

BODI YA BARABARA MKOA WA DODOMA YAZITAKA HALMASHAURI ZA WILAYA DODOMA KUCHAGUA WAKANDARASI WENYE UWEZO WA KUFANYA KAZI WANAPOTOA KANDARASI

BODI YA BARABARA MKOA WA DODOMA YAZITAKA HALMASHAURI ZA WILAYA DODOMA KUCHAGUA WAKANDARASI WENYE UWEZO WA KUFANYA KAZI WANAPOTOA KANDARASI

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com
Mkuu wa Mkoa wa Dodoma na Mwenyekiti wa Bodi ya Barabara ya Mkoa wa Dodoma Mhe. Chiku Gallawa akifugua Mkutano wa bodi hiyo Feb. 17,2015 Mjini Dodoma.
Wajumbe wa Bodi ya barabara ya Mkoa wa Dodoma wakimsikiliza mwenyekiti wa Bodi Mhe. Chiku Gallawa wakati akifungua Mkutano wa kwanza wa Bodi hiyo kwa mwaka 2015 mjini Dodoma Feb. 17.
Meneja wa Wakala wa Barabara-TANROADS Mkoa wa Dodoma mhandisi Leonard Chimagu akiwasilisha taarifa ya utekelezaji wa miradi ya barabara inayotekelezwa na TANROADS kwenye Mkoa wa Dodoma wakati wa kikao cha Bodi ya Barabara Mkoani humo Feb 17, 2015.
Wajumbe wa Sekretarieti ya Bodi ya Barabara ya Mkoa wa Dodoma wakichukua kumbukumbu muhimu kutoka michango ya wajumbe wakati wa Kikao cha Bodi ya barabara ya Dodoma Feb. 17, 2015.
Mwenyekiti wa Halashauri ya Wilaya ya Kongwa Mhe. White Zuberi akichangia hoja wakati wa Kikao cha Bodi ya Barabara Moka wa Dodoma Feb.17, 2015.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Dodoma SACP David Misime aki akichangia hoja wakati wa Kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Dodoma Feb.17, 2015.
Naibu Waziri wa Habari Vijana Utamaduni na Michezo na Mbunge wa Kondoa Kusini Mhe. Juma Nkamia akichangia hoja wakati wa Kikao cha Bodi ya Barabara Mkoa wa Dodoma Feb.17, 2015.

WAZIRI MKUU AFUNGUA MKUTANO WA NNE WA WADAU WA MFUKO WA PENSHENI WA PSPF MJINI DODOMA

WAZIRI MKUU AFUNGUA MKUTANO WA NNE WA WADAU WA MFUKO WA PENSHENI WA PSPF MJINI DODOMA

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com
Waziri Mkuu,Mizengo Pinda (Kushoto) akizindua huduma mpya itolewayo na Mfuko wa Pensheni wa PSPF, ya Fao la Uzazi, mwanzoni mwa mkutano mkuu wa wadau na wanachama wa Mfuko huo mjini Dodoma jana. Wanaoshuhudia kutoka kulia, ni naibu waziri wa fedha, Adam Malima, Mwenyekiti wa bodi ya Mfuko huo, GHeorge Yambesi, Mkurugenzi Mkuu wa PSPF, Adam Mayingu, na mkuu wa mkoa wa Dodoma, Chiku Galawa.
Waziri Mkuu,Mizengo Pinda akihutubia wakati wa ufunguzi wa Mkutano mkuu wa Nne wa Wadau na Wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF ulioanza leo mjini Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF ,Adam Mayingu kihutubia wakati wa ufunguzi wa Mkutano mkuu wa Nne wa Wadau na Wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF ulioanza leo mjini Dodoma.
Waziri mkuu Mizengo Pinda (Kushoto) akipeana mkono na Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, Adam Mayingu, huku Mwenyekiti wa bodi ya Mfuko huo, George Yambesi, (Kulia), na Mkuu wa mkoa wa Dodoma, Chiku Galawa wakishuhudia, wakati wa ufunguzi wa mkutano mkuu wa 4 wa wanachama na wadau wa Mfuko huo mjini Dodoma, Jumatano Feb 18, 2015.
Waziri mkuu Mizengo Pinda, akimpongeza Zainab Khalid, mmoja kati ya wanachama wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, aliyefaidika na mkopo wa elimu ambapo sasa anasoma chuo kikuu Huria jijini Dar es Salaam. Tukio hilo lilikuwa sehemu ya ufunghuzi wa mkutano mkuu wan ne wa wadau na wanachama wa Mfuko huo mjini Dodoma Jumatano Februari 18, 2015.
Baadhi ya wajumbe wa bodi ya Mfuko wa Pensheni wa PSPF, waliopita na wa sasa, wakipiga makofi wakati waziri mkuu Mizengo Pinda, wakati akifungua mkutano mkuu wa Nne wa wadau na wanachama wa Mfuko huo mjini Dodoma, Jumatano Februari 18, 2015.
Baadhi wa washiriki wa mkutano mkuu wan ne wa wanachama na wadau wa Mfuko wa Pensheni wa PSPF, mjini Dodoma Jumatano Feb 18, 2015.

UZALENDO, UADILIFU NA MASLAHI YA TAIFA: WAJIBU WA VYOMBO VYA HABARI JAMII

UZALENDO, UADILIFU NA MASLAHI YA TAIFA: WAJIBU WA VYOMBO VYA HABARI JAMII

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com
DSC_0219
Mshehereshaji kwenye madhimisho ya siku ya redio duniani, Bi. Usia Nkhoma Ledama akizungumza machache kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufungua rasmi maadhimisho hayo Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha.(Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog).

Na Mwandishi wetu, Arusha
Vyombo vya habari hususan redio za jamii zimetakiwa kutanguliza uzalendo na kutetea maslahi ya taifa ili kuliepusha taifa katika migogoro na mitafaruku inayoweza kusababisha machafuko nchini hasa katika kipindi cha uchaguzi mkuu ujao.

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa wilaya ya Arumeru mkoani Arusha Nyerembe Munasa wakati wa kuadhimisha Siku ya Redio duniani iliyofanyika mwishoni mwa wiki. Akizungumza na watangazaji wa redio za jamii na wadau mbalimbali wa habari nchini katika ufunguzi wa maadhimisho hayo Munasa alisema redio ina nguvu kubwa kuchambua na kutengeneza mustakabali wa taifa na hasa vijana iwapo itatumika vizuri badala ya kuwa chanzo cha matatizo na uchochezi mambo ambayo yanaweza kulisambaratisha taifa.

Amewataka waandishi na watangazaji wa redio jamii kuzingatia maadili ya kazi zao kwa lengo la kuleta mabadiliko katika maisha ya Watanzania na kujenga taifa endelevu .
DSC_0255
Mkuu wa Wilaya ya Arumeru Mkoani Arusha, Nyerembe Munasa akizungumza katika ufunguzi wa kuadhimisha siku ya redio duniani iliyofanyika mwishoni mwa wiki jijini Arusha.

“Mnatakiwa kutafiti, kutathmini na kupeleka taarifa zenye tija na kuhamasisha vijana kujituma kufanya kazi kwa bidii ili kuondoa wimbi la umaskini kwa wananchi na hasa vijana, mkitekeleza wajibu wenu kwa kujua nini mnachofanya mtachochea mabadiliko kwa haraka katika jamii”.

Akizungumzia fursa zilizopo, Mkuu huyo wa Wilaya ya Arumeru ametoa wito pia kwa vyombo vya habari hususani radio za jamii kuwawezesha vijana wa Kitanzania kutambua na kutumia fursa zilizopo za uchumi wa gesi na mafuta ili kujiondoa katika umaskini unaolalamikiwa kusababishwa na ukosefu wa kazi.

“Pamoja na utengenezaji wa vipindi vyenye kuelimisha jamii redio jamii lazima ziwajibike kibinafsi na kijamii hadi ngazi ya taifa kwa kuwapa vijana taarifa zilizosheheni fursa zilizopo na namna ya kuzifanyia kazi, ili vijana waondokane katika migogoro na maandamano yasiyokuwa na tija kwa sababu watakuwa wanajua nini cha kufanya ndani ya sheria na utengamano wa amani”.

DSC_0242
Amesema vyombo vya habari jamii iwapo vitatumia vyema Katika kuwashirikisha vijana vina uwezo na nguvu kubwa kubadilisha fikra za wananchi kwa kutengeneza vipindi ambavyo vitachochea mawazo endelevu kwa kuzingatia mila na utamaduni wa taifa la Mtanzania kuwakomboa vijana kuepukana na utamaduni tegemezi unaosababisha kulemaa kwa vijana kutafuta njia za mkato na kutopenda kufanya kazi jambo ambalo linasababisha mwendelezo wa umaskini nchini.

Akizungumza kwa wakilishi wa redio za jamii, waandishi na wadau wengine wa habari mjini hapa, Munasa alisema majukumu matatu ya utangazaji wa redio, yamekuwa hayafikiwi inavyotakiwa kutokana na wengi wa wahusika kutofahamu vyema majukumu yao au kutowajibika kikamilifu.
“Utakuta mwandishi wa habari hasa watangazaji anaingia studio hajajiandaa kwa kufanya utafiti wa somo linalozungumziwa, hana mwongozo wa kipindi (script), hana mpango kazi wa kipindi (programme matrix) na wala mlolongo wa uendeshaji wa kipindi kinapoanzia na kuishia, hili ni tatizo sio utangazaji!”

DSC_0223
Baadhi ya washiriki kutoka redio mbalimbali za jamii nchini wakimsikiliza mgeni rasmi wakati akifungua rasmi sherehe za maadhimisho ya siku ya redio duniani.

Pamoja na kuwakumbusha watangazaji umuhimu wa kutangaza katika vyombo vya habari hususan redio mkuu huyo wa wilaya aliwataka washiriki kubadili mtazamo wa muziki kwa kupiga muziki wa asili kwa lengo la kupeleka ujumbe mzito na wenye manufaa kwa taifa badala ya muziki uliojaa mahadhi ya mapenzi na matusi.

“Muziki una nguvu kubwa katika maisha ya binadamu watangazaji lazima mfahamu na mjue namna ya kuupangilia kutokana na vipindi mnavyovitayarisha na muda wa aina ya muziki husika. Sio wakati wote ni wakati wa kusikiliza muziki wa mapenzi, kwa sababu redio husikilizwa na watu mbalimbali kwa sababu mbalimbali pia.”

Suala la mpangilio wa muziki, kuuelewa na thamani yake katika redio na umma lilielezwa kwa undani zaidi na nguli wa masuala ya muziki katika vyombo vya habari Masoud Masoud ambaye alisema kuwa watangazaji wa kisasa wamekuwa hawaelewi maana ya muziki na faida zake Katika kuendeleza taifa kitamaduni na kimaendeleo.

DSC_0012
“Vijana wengi wamekuwa wakitayarisha muziki wanaoupenda wao na sio unaopendwa na kufufaisha umma, wakati umefika kwa kutafuta mbinu au jitihada zozote za kuwafundisha muziki ni nini, unachezwa wakati gani na kwa manufaa ya nani.”

Sherehe hizo ambazo huandaliwa kila mwaka tarehe 13 Februari, ziliandaliwa na Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO) na ujumbe wa mwaka huu ni “Nguvu ya Redio na Ushiriki wa Vijana katika Maendeleo”.

Ujumbe kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa UNESCO, Irina Bokova katika kuadhimisha siku hiyo na kusomwa kwa niaba yake na mwakilishi wa UNESCO nchini Bokosha Spencer umesisitiza nguvu ya radio katika kujihusisha na masuala ya kijamii kwa vijana wenye umri chini ya miaka 30, ambao ni zaidi ya nusu ya idadi ya watu duniani.

DSC_0258
Afisa Habari wa kituo cha Habari cha Umoja wa Mataifa (UNIC), Usia Nkhoma Ledama akifurahi jambo na baadhi ya washiriki kutoka redio mbalimbali za jamii wakati Mkuu wa Wilaya ya Arumeru akibariki ufunguzi wa maadhimisho ya siku ya redio duniani yaliyofanyika jijini Arusha mwishoni mwa wiki.

“Vijana wanawake na wanaume hawashirikishwi vema katika vyombo vya habari - hutengwa mara nyingi kunakoashiria kusahaulika kwa mapana yake katika masuala ya kijamii, kiuchumi na kidemokrasia. Redio kama chombo cha mshikamano, kinachokuza elimu na utamaduni ushirikishwaji wa vijana ni muhimu”.

Bokova aliitaka jamii kuwasaidia vijana kwa kuwapa sauti kubwa zaidi na kujenga hisia ya jamii kwa njia ya usambazaji wa habari kwa kutayarisha na kusikiliza vipindi vya redio.

DSC_0007
Bw. Spencer Bokosha akisoma hotuba kwenye maadhimisho ya siku ya redio duniani kwa niaba ya Mkuu wa ofisi ya Shirika la UNESCO, Tanzania Zulmira Rodriguez.
DSC_0061
Mwenyekiti wa mkutano wa sherehe maadhimisho ya siku ya redio duniani ambaye pia ni Meneja wa Maadili wa Baraza la Habari Tanzania (MCT), Bw. Allan Lawa akiendesha akitoa mada chokonozi ni kwa namna gani radio inaweza kutumika kama jukwaa la ushiriki kwa vijana katika mabadiliko ya kidemokrasia? Utafiti unaogusa Watanzania wakielekea katika uchaguzi mkuu.
DSC_0158
Mwandishi mkongwe na mkufunzi wa tasinia ya habari kutoka chuo kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Ayub Rioba akitoa mada Je uwekaji huru wa mawimbi ya radio kumesababisha mambo mabaya zaidi kuliko mazuri: Mitazamo na matarajio kuhusiana na ushiriki wa vijana wakati wa sherehe za maadhimisho ya siku ya redio duniani.
DSC_0147
Makamu Mwenyekiti wa mtandao wa redio za jamii nchini (COMNETA) ambaye pia ni Meneja wa redio jamii Sengerema FM ya mkoani Mwanza Bw. Felician Ncheye, akiwasilisha mada inayohusu ushiriki wa vijana katika vipindi vya Redio, ambapo amesema kuwa kuna umuhimu mkubwa wa Redio za jamii kuhakikisha zinawafikia watu wote kwenye jamii huku wakiwalenga vijana ambao ndio wana idadi kubwa ambayo inaweza kuchochea mabadiliko ya kisiasa, kiuchumi na kitamaduni.
DSC_0091
Meneja wa Redio Kahama FM, Marco Mipawa akichangia mada ya kuonesha nguvu za vijana na vyombo vya habari vya jamii pamoja na kujadili kanuni bora zilizojitokeza katika utekelezaji wakati sherehe za maadhimisho ya siku ya redio duniani zilizofanyika mwishoni mwa wiki jijini Arusha.
DSC_0136
Mwandishi wa habari mkongwe, mzee Gervas Moshilo akitoa mada ya Uandishi wenye maadili na uwakilishi wa vijana kupitia vyombo vya habari wakati wa sherehe za maadhimisho ya siku ya redio duniani.
DSC_0054
Meza kuu ikifuatilia mada na michango mbalimbali iliyokuwa ikitolewa na washiriki.
DSC_0183
Pichani juu na chini ni watangazaji wa redio za kijamii walioshiriki kwenye sherehe za maadhimisho ya siku ya redio duniani wakichangia mada mbalimbali zilizokuwa zikiwasilishwa kwenye maadhimisho hayo.
DSC_0123

WAOMBA KITUO MAALUMU CHA WATOTO WALEMAVU BUHANGIJA KUSAIDIWA ZAHANATI

WAOMBA KITUO MAALUMU CHA WATOTO WALEMAVU BUHANGIJA KUSAIDIWA ZAHANATI

Posted in ,
No comments
By danielmjema.blogspot.com
DSC_0002
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Bi. Anne Rose Nyamubi mara baada ya kuwasili ofisini kwake kwa ajili ya mazungumzo kabla ya kuelekea kwenye kituo cha kulelea watoto wenye mahitaji maalum wakiwemo walemavu wa ngozi cha Buhangija Jumuishi kilichopo mkoani Shinyanga.

Na mwandishi wetu, Shinyanga
MKUU wa wilaya ya Shinyanga AnneRose Nyamubi ameomba jamii ya watanzania kusaidia kupatikana kwa zahanati katika kituo cha kulelea watoto walemavu cha Buhangija ili kupunguza adha wanazopata watoto hao katika huduma za afya.

Kauli hiyo ameitoa katika mazungumzo na mwandishi wa habari hizi ambaye alifika katika kituo hicho akiambatana na ujumbe wa Umoja wa Mataifa uliokuwa ukiongozwa na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez.

Nyamubi amesema kwamba ingawa hospitali ya mkoa ina dirisha kwa ajili ya matibabu ya watoto hao,wakati mwingine inakuwa shida daktari maalumu anayehusika anapokuwa hayupo. Aidha alisema kwa namna watoto hao walivyo wanahitaji huduma ya karibu ya kitiba ambayo inawezekana kama kituo hicho kingekuwa na zahanati yake.
DSC_0026
Mkuu wa Wilaya ya Shinyanga, Bi. Anne Rose Nyamubi akiwa kwenye mazungumzo na Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez aliyeambatana na Mshauri wa masuala ya haki za binadamu kutoka ofisi kwake, Bi. Chitralekha Massey ( wa pili kulia kwake) pamoja na Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania Hoyce Temu (wa pili kushoto). Wengine katika picha ni Afisa Elimu Sayansikimu, Beatrice Mbonea (wa kwa kulia), Afisa Elimu Msingi wa manispaa ya Shinyanga, Bi. Pudensiana Magnus (katikati kulia), Mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga, Festo Kang'ombe pamoja na Msaidizi wa Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Bw. Shadrack Kengese.

Kituo hicho kilichoanzishwa mwaka 2010 kwa ajili ya watoto walemavu wasiosikia na wasiiona kwa sasa kinapokea watoto wenye alibnizim ambao wanaokabiliwa na ujahiri dhidi ya maisha yao.
Kwa mujibu wa mkuu huyo wa wilaya kituo hicho ambacho serikali hutenga bajeti kwa ajili ya wanafunzi 50 wasiosikia na kuona, sasa kina watoto wenye albinism 247 ambao hawako katika bajeti na wanaishi kutokana na misaada ya watu mbalimbali.

Alisema kwamba watoto wenye albinism wanahitaji huduma za tiba za karibu zaidi kutokana na mazingira yanawazunguka na dirisha pekee katika hospitali ya mkoa halitoshi kwani wakati mwingine wanalazimika kukaa kwenye foleni kama wagonjwa wengine na hili halipendezi.
Aidha alisema kituo hicho cha Buhangija kwa sasa ni kidogo kuzingatia na uwingi wa wanaohitaji msaada na hivyo serikali inatafuta eneo jingine kwa ajili ya kujenga kituo.

DSC_0053
Mazungumzo yakiendelea ndani ya ofisi za Mkuu wa mkoa wa Shinyanga zinazokaimiwa na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Bi Anne Rose Nyamubi.
Kufurika kwa watoto hao wenye ulemavu kunatokana na tishio la maisha yao hasa ukanda wa Ziwa ambapo familia zao zimewakimbiza kituoni hapo kwa ajili ya usalama wao.
Aidha Mkuu huyo wa wilaya amesema kwamba kituo hicho hakina bajeti na kutaka wasamaria wema kuendelea kuchangia ili watoto hao waendeshe maisha ya kawaida.
Naye Mratibu wa Mashirika ya Umoja Mataifa yaliyopo nchini, Alvaro Rodrigues amesema kwamba Umoja wa Mataifa utaendelea kusaidia kituo hicho na kuwataka wanaotunzwa hapo kutoacha kuishi kama watoto kwani ndio tunu waliyonayo kwa sasa.
Aidha alisema kwamba anauchukua wimbo waliouimba ambao unazungumzia machungu ya maisha yao na kwenda kuwaeleza watu wengine ili nao washiriki katika kubadilisha hali ya kuogofisha na kuleta usalama.
DSC_0068
Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la UNDER THE SAME SUN, Vicky Ntetema alijumuika kwenye mazungumzo hayo. Pichani akifafanua jambo kwa Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (hayupo pichani) kuhusiana na changamoto mbalimbali zinazowakabili watu wenye ulemavu wa ngozi nchini.

Alisema wao (UN) wamefika katika kituo hicho kuona watoto wanavyoishi na watafanya nini kuwasaidia.
Aliwataka Watanzania kuhakikisha wanakomesha machungu ya albino hao na kuishi nao kama watu wengine wa kawaida.
Aidha Mratibu huyo alipata nafasi ya kuzungumza na Binti wa miaka 19 Masabu masuka ambaye amejifungua mwaka jana kituoni hapo bila msaada wa wauguzi baada ya kulazimika kuondoka kwao akiwa mjamzito kukwepa mauaji dhidi ya albino yaliyofanyika Mei mwaka jana wilayani Bariadi.
Binti huyo alifika kituoni hapo na kaka zake watatu ambao wote ni maalbino kama yeye.
DSC_0075
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Bi Anne Rose Nyamubi katika picha ya pamoja na ugeni kutoka ofisi za Umoja wa Mataifa Tanzania na Shirika la UNDER THE SAME SUN.

DSC_0120
Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Bi Anne Rose Nyamubi akiwasalimia watoto wenye ulemavu wa ngozi wanaolelewa kwenye kituo cha Buhangija Jumuishi kilichopo mkoani Shinyanga kabla ya kumtambulisha Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (hayupo pichani).

DSC_0150
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kulia) akizungumza na watoto wenye ulemavu wakiwemo wa ngozi (hawapo pichani) wanaolelewa kwenye kituo cha Buhangija Jumuishi kilichopo mkoani Shinyanga alipofanya ziara ya kutembelea kituo hicho. Katikati ni Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania Hoyce Temu na kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Bi. Anne Rose Nyamubi.

DSC_0167
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akitoa zawadi ya maziwa kwa watoto wenye ulemavu wa ngozi wanaolelewa kwenye kituo cha Buhangija Jumuishi kilichopo mkoani Shinyanga.
DSC_0174
Mtaalam wa Mahusiano na Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa (UN) Tanzania, Hoyce Temu akishiriki kwenye zoezi la kugawa zawadi kwa watoto hao.

DSC_0186
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez na Mshauri wa masuala ya haki za binadamu kutoka ofisi ya Mratibu huyo, Bi. Chitralekha Massey wakiendelea na zoezi la kugawa zawadi kwa watoto hao.

DSC_0203
Mratibu Mkazi huyo Bw. Alvaro Rodriguez akiwasaidia watoto hao kufungua biskuti alizowapekea kama zawadi alipotembelea kwenye kituo hicho.
DSC_0213
Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la UNDER THE SAME SUN, Vicky Ntetema akieleza jambo kwa Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kulia) alipokuwa akikagua mazingira ya kituo hicho na kuona ni jinsi atawasaidia kutatua changamoto mbalimbali zinazoikabili kituo hicho.
DSC_0235
Pichani ni jiko la kituo cha kulelea watoto wenye ulemavu wakiwemo wa ngozi cha Buhangija Jumuishi kilichopo mkoani Shinyanga.
DSC_0248
Wapishi wakiendelea na shughuli zao kuwapikia watoto wanaolelewa kwenye kituo hicho.
DSC_0261
Mwalimu Mkuu wa shule ya watoto wenye maalum ya Buhangija Jumuishi, Peter Ajali akitoa maelezo ndani ya moja ya mabweni kituoni hapo kwa Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez (kulia) na kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la UNDER THE SAME SUN, Vicky Ntetema.
DSC_0278
Mwalimu Mkuu wa shule ya watoto wenye maalum ya Buhangija Jumuishi, Peter Ajali akimwonyesha baadhi ya sehemu ambazo hazisakafiwa ndani ya mabweni kituoni hapo Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez.
DSC_0308
Baadhi ya matandiko wanayotumia watoto hao wenye mahitaji maalum kulali kwenye sakafu ambayo haijasakafiwa na pia kutokana na uhaba wa mabweni inawalazimu kubanana na kulala bila uhuru.
DSC_0311
Bweni lililojengwa na Miss Tanzania 2012, Brigitte Alfred linalohudumia watoto 48 ambalo linahitaji kumaliziwa ili watoto hao nao waweze kulala mahali pazuri.
DSC_0233
Mratibu wa mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini,Alvaro Rodrigues akizungumza na binti wa miaka 19 ambaye ni mlemavu wa ngozi na kutosikia, Masalu Masuka ambaye anaishi katika kituo cha watoto walemavu cha Buhangija baada ya kukimbia kwao Bariadi kukwepa wauaji wa albino. Binti huyo alijifungua mtoto wake akiwa kituoni hapo bila msaada wa muuguzi. Kituo hicho kinahitaji msaada wa kujengewa zahanati. (Picha na Zainul wa Mo Blog)
DSC_0331
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akicheza mpira ambao ni moja ya zawadi alizozitoa kwa watoto wenye ulemavu wa ngozi wanaolelewa kwenye kituo cha Buhangija Jumuishi kilichopo mkoani Shinyanga alipofanya ziara ya kukitembelea kituo hicho kinachokabiliwa na changamoto mbalimbali na kuwaahidi kuwasaidia huku akiwashirkisha na wadau wengine wa maendeleo. Kushoto mwenye kofia ni Khassan Khamis na kulia ni Emmanuel Deus.
DSC_0346
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akiendelea kucheza mpira na kufurahi na watoto hao wenye ulemavu wa ngozi.
DSC_0386
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akiwa amembeba mtoto mwenye ulemavu wa ngozi Ghoke Maliwa anayelelewa kwenye kituo cha Buhangija Jumuishi kilichopo mkoani Shinyanga alipofanya ziara ya kukitembelea kituo hicho juzi mkoani humo.
DSC_0351
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akisoma ujumbe unaosema "DREAM BIG" kwenye T-shirt ya mtoto Agnes Kabika mwenye ulemavu wa ngozi anayelelewa kwenye kituo cha Buhangija Jumuishi alipofanya ziara ya kutembelea kituo hicho.
DSC_0315
Mshauri wa masuala ya haki za binadamu kutoka ofisi ya Mratibu huyo, Bi. Chitralekha Massey akibadilishana mawazo na binti anayefanya shughuli za kujitolea Claire Grubbs kutoka nchini Marekani aliyepiga kambi kwenye kituo cha Buhangija Jumuishi kilichopo mkoani Shinyanga.
DSC_0428
Mratibu Mkazi wa mashirika ya Umoja wa Mataifa na mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini, Alvaro Rodriguez akiagana na Mkuu wa wilaya ya Shinyanga, Bi Anne Rose Nyamubi mara baada ya kuhitimisha ziara yake kwenye kituo hicho.

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .