Showing posts with label Afya. Show all posts
Showing posts with label Afya. Show all posts

Fahamu nchi zinaongoza kwa matumizi ya Bangi

Fahamu nchi zinaongoza kwa matumizi ya Bangi

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com
Lesotho
Matumizi ya bangi nchini Lesotho yanaruhusiwa tu kwa matumizi ya dawa , kwa kiasi kikubwa bangi hulimwa nchini humo.Miaka ya 2000 ilikadiriwa kuwa asilimia 70 ya bangi nchini Afrika Kusini inatoka nchini Lesotho.
Wakulima nchini Lesotho wanalima bangi kwa ajili ya matumizi yao nyumbani na kusafirisha nje ya mipaka, kutokana na hali ya umasikini waliyonayo, wakulima wadogo nchini humo wanalima bangi miongoni mwa mazao yao mengine kama vile mahindi kwa ajili ya kusafirisha nchini Afrika Kusini.
Afrika Kusini
Afrika Kusini ni nchi ambayo ilitarajiwa kuwa ya kwanza kuhalalisha bangi.Mwezi Aprili mwaka jana, ilihalalisha bangi kwa matumizi binafsi nyumbani, lakini haikuruhusiwa kuzalishwa au kuuzwa.
Tangu mwezi machi mwaka 2017, baada ya mahakama kuu ya Western Cape kuhalalisha matumizi ya bangi majumbani bado matumizi yake ni kinyume cha sheria, mpaka pale sheria itakapobadilishwa kuruhusu wafanyabiashara walime na kuwekeza kwenye kilimo cha bangi, vivyo hivyo kwa makampuni kutengeneza bidhaa zitokanazo na bangi na mawakala kusambaza bidhaa.
katika kipindi cha miezi kadhaa nyuma, wale walioonyesha nia ya kuwekeza kwenye kilimo cha bangi wameleta maendeleo makubwa kufungua milango katika uzalishaji wa bangi kwa ajili ya dawa.
Ghana
Kwa mujibu wa Umoja wa mataifa, Ghana ni mtumiaji wa tatu wa bangi duniani, asilimia 21.5 ya raia wake wenye umri wa kati ya miaka 15 mpaka 64 wanajihusisha na uvutaji wa bangi .
kulikuwa na mjadala wa kitaifa kuhusu kuhalalishwa kwa bangi, mjadala ambao uligonga mwamba wakati wa siku ya kimataifa ya kupambana na dawa za kulevya.
Mamlaka nchini humo zinasema kuwa bangi ni hatari zaidi kuliko kinywaji chenye kilevi, na iwapo itahalalishwa madhara yake hayatahimilika.
pamoja na hayo Ghana inashirikiana na mataifa mengine ya Afrika Magharibi kuhakikisha kuwa wanapambana kukomesha matumizi ya bangi na usafirishaji katika ukanda wao.
Korea Kaskazini
Bangi hukua kwa wingi sana nchin Korea Kaskazini hata mashirika ya kiserikali yamekuwa yakisafirisha kuuza nje ili kupata fedha za kigeni.
wachambuzi wa mambo wanasema haiko wazi kama kuna sheria inayopinga matumizi ya bangi, nchi hiyo haitazami kama matumizi ya bangi ni kinyume cha sheria.
Bangi imekuwa ikiuzwa kwenye maduka ya vyakula na hata maeneo mengine watu wakivuta bila kificho.

Kuwa na mpenzi na afya nzuri huchangia furaha

Kuwa na mpenzi na afya nzuri huchangia furaha

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com
Afya nzuri ya akili na kuwa na mpenzi huwafanya watu kuwa kwenye furaha kuliko hata kuongezwa mshara mara dufu, kwa mujibu utafiti mpya.
Utafiti huo uliofanywa na chuo cha masuala ya uchumi cha London ulitokana na majibu kutoka kwa watu 200,000, kuhusu ni kwa njia ipi masuala tofauti huchangia maisha yao.
Kwa vipimo kutoka namba moja hadi kumi, kuongezwa mara dufu mshahara wa mtu hukumonga furaha alama ilisyo chini ya 0.2.
Hata hivyo kuwa na mpenzi kulichangia furaha kuongezeka kwa alama 0.6 na kumpoteza mpenzi kwa kutengana au kifo nako kulisababisha furaha kupungua kwa alama kama hiyo.
Madhara zaidi yalisababishwa na msongo wa mawazo ambayo ilisababisha viwango vya furaha kudidimia kwa alama 0.7. Ukosefu wa ajira pia kulichangia kushuka kwa alama sawa na hizo.
Mmoja ya waandishi wa ripoti hiyo Prof Richard Layard, anasema kuwa matokeo hayo yana maana kuwa, nchi zinastahili kuelekeza majukumu mapya kuboresha furaha kwa watu wake badala ya kuangazia njia za kukuza utajiri.
Aliongeza kuwa vitu ambavyo huchangia katika furaha zetu na kwa hatma yetu ni mahusiano na hali zetu kiafya.

Mji wa Dodoma, nchini Tanzania yakumbwa na ugonjwa usiojulikana

Mji wa Dodoma, nchini Tanzania yakumbwa na ugonjwa usiojulikana

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com
Hofu na wasi wasi umezidi kutanda huko mkoani Dodoma katikati mwa Tanzania baada ya kuibuka kwa ugonjwa usiojulikana.
Hadi sasa jumla ya watu saba wamefariki na wengine 21 kulazwa katika hospital ya mkoa mjini Dodoma baada ya kuzuka ugongwa huo ambao hadi sasa madaktari haujui tiba yake.
Dalili za ugonjwa huo ni pamoja na kutapika, kuharisha, ngozi na macho kuwa ya njano pamoja na kuumwa na tumbo.
Kufuatia kuibuka kwa ugonjwa huo tayari kumetengwa wodi maalum katika hosptali ya taifa ya rufaa ya Dodoma katikati mwa Tanzania ambapo pia karantini imewekwa na hakuna anayeruhusiwa kukaribia mahali hapo zaidi ya madaktari ambao nao pia wanaingia kwenye wodi kuwaona wagonjwa kwa tahadhari kubwa.

Tanzania kinara unyanyasaji kwa watu wenye Ualbino

Tanzania kinara unyanyasaji kwa watu wenye Ualbino

No comments
By danielmjema.blogspot.com
Mtaalam huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu Ulemavu wa Ngozi, Ikponwosa Ero akizungumza na waandishi wa habari. Kushoto ni Shirika la Kimataifa la Under The Same Sun, Vicky Ntetema na kulia ni Mkuu wa Mawasiliano wa Shirika la Standing Voice, Sam Clarke.
Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini (UN), Alvaro Rodriguez akielezea jinsi UN waevyojipanga kuwasaidia watu wenye ualbino. Kushoto ni Mtaalam Huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu Ulemavu wa Ngozi, Ikponwosa Ero.
Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Bahame Nyanduga. Kushoto ni Mtaalam Huru wa Umoja wa Mataifa kuhusu Ulemavu wa Ngozi, Ikponwosa Ero  na kulia ni Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini (UN), Alvaro Rodriguez.
Na Mwandishi wetu, Dar es salaam
Pamoja na juhudi ambazo serikali ya Tanzania. imekuwa ikizifanya ili kuhakikisha watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) wanakuwa salama na amani lakini bado Taifa hilo, lililoko katika jumuiya ya Afrika mashariki, inaendelea kuwa nchi ya hatari kwa watu hao kwa kuwa katika orodha ya nchi ambazo zina kiwango kikubwa cha unyanyasaji.
 
Akizungumza na waandishi wa habari katika kilele cha kongamano la kikanda kwa ajili ya hatua kuhusu ulemavu wa ngozi Afrika lililofanyika Dar es Salaam, Mtaalam huru wa Umoja wa mataifa kuhusu Ulemavu wa Ngozi, Ikponwosa Ero alisema kuwa kwa ripoti ambazo wamekuwa wakizipokea inaonyesha Tanzania ni moja ya nchi ambazo zina unyanyasaji kwa watu wenye ualbino.
"Tangu nimeingia sijawahi kufanya uchunguzi hata katika matokeo ya uchunguzi wa nchi 29 sijaujua sana lakini kwa taarifa ambazo nimekuwa nikipata kutoka kwa taasisi mbalimbali inaonyesha Tanzania ni unyanyasaji wa hali ya juu kwa watu walio na uablino," alisema Ero.
Nae Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Bahame Nyanguga alisema katika kongamano hilo wametoka na maazimio ambayo wanaiomba serikali iweze kuyafanya ili kuwezesha watu wenye ualbino kuwa na usalama wa uhakika.
"Tumejadili mambo mengi lakini tunaiomba serikali ihusike moja kwa moja kupinga unyanyasaji, ukatili na ubaguzi nia tunaiona kwahiyo tunaomba waendelee kuwa hivyo na pia waongeze bajeti na zaidi katika matibabu kwa watu wenye ualbino," alisema Nyanduga.
Kwa upande wa Shirika la Umoja wa Mataifa kupitia Mratibu Mkazi wa mashirika hayo, Alvaro Rodriguez alisema ni wataendelea kuwasaidia watu wenye ualbino ili kuwezesha kupunguza changamoto ambazo zinawakabili.

Je Wajua Samaki Wabichi ni Dawa?

Je Wajua Samaki Wabichi ni Dawa?

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com
samaki insia

Huu umekuwa utamaduni wao wa muda mrefu huku wakiamini kuwa njia hii inaweza kurahisisha upumuaji kwa watoto na pia kwa wagonjwa wa Pumu  hii ndio tiba sahihi. Kila June familia mbalimbali hujumuika kwa pamoja ili kushiriki katika zoezi hili.
Mdomoni mwa samaki hao wanaweka dawa za asili zenye rangi ya njano na kuhakikisha anayepokea anameza vyote. Zoezi hili limekuwa likifanyika kwa miaka 170 ikiwa mwaka huu inakadiriwa zaidi ya watu laki moja walipokea tiba hiyo.

UKIMWI ya Paka yagundulika nchini Kenya

UKIMWI ya Paka yagundulika nchini Kenya

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com
Wanasayansi humu nchini wamegundua virusi hatari aina ya FIV vinaavyofanana kabisa na virusi vya HIV vinavyosababisha UKIMWI vimegunduliwa katika paka mmoja ikiwa ni baada ya uchunguzi wa kina wa damu ya paka huyo kuthibitisha uwepo wa viini vinavyofanana kabisa na vile vinavyoathiri binaadamu.
Wafugaji wa paka na wanyama wa nyumbani wametakiwa kuwapeleka wanyama wao kufanyiwa uchunguzi wa afya wanapowashuku wanyama wao wanaugua, virusi hivyo vinaitwa FIV (Feline Immunodefficiency Virus) na wanasema ugonjwa huu sio mgeni kwa wanyama.
kwa mujibu wa BBC Swahili, Mwaka wa 1986 madaktari wa Marekani waligundua virusi vilivyofanana kwa karibu na vile vinavyoambukiza binadamu vya HIV lakini hii ndio mara ya kwanza kwa virusi hivyo kugunduliwa nchini Kenya.
Madaktari wa maabara ya Lancet Nairobi waligundua kuwa virusi hivyo vinasababisha ukosefu wa kinga mwilini na kudhoofisha afya ya wanyama hao wanaopendwa na kuishi majumbani lakini hata hivyo waliwahakikishia wafugaji wa paka kuwa hakuna ushuhuda wowote wa maambukizi kutoka kwa paka hao kwenda kwa binadamu.
Daktari Dhaval Shah badala yake amewashauri wafugaji wa paka kuwafungia paka wao ndani ili kuwazuia wasijamiiane na wale paka wanaorandaranda mitaani ambao huenda wameambukizwa UKIMWI wa paka ambao unaambukizwa kupitia mate na mkwaruzano paka wanapopigana.

Virusi vya ZIKA tishio Olimpiki, Wataalamu wa Afya washauri mashindano yaondlewe Brazil

Virusi vya ZIKA tishio Olimpiki, Wataalamu wa Afya washauri mashindano yaondlewe Brazil

Posted in ,
No comments
By danielmjema.blogspot.com
Zaidi ya wataalamu 100 wa afya, wanazuoni na wanasayansi Ijumaa (27.05.2016) wametoa wito kuahirishwa michezo ya olimpiki mjini Rio kwa kuwa tukio hilo linaweza kuharakisha kusambaa kwa virusi vya Zika duniani.


Tathmini yao inapingana na mawazo ya baadhi ya wataalamu waandamizi wa magonjwa ya kuambukiza ambao wanasema iwapo patachukuliwa hatua za tahadhari hakuna sababu ya kufuta michezo hiyo. 
Siku ya Alhamis, Dr. Tom Friedeb, mkurugenzi wa kituo cha Marekani kwa ajili ya udhibiti wa magonjwa na kuzuwia, alitangaza kwamba hakuna sababu ya kiafya kwa jamii hata kufuta ama kuchelewesha michezo hiyo inayotarajiwa kufanyika majira ya kiangazi.
Katika barua ya wazi iliyowekwa katika mtandao wa internet, kundi hilo la wa wataalamu wa afya 150 , wengi wao wakihusika na masuala ya bakteria amesema kitisho cha maambukizi kutokana na virusi vya Zika ni cha juu kabisa.
Barua hiyo ilitumwa mwa Dr. Margaret Chan, mkurugenzi mkuu wa shirika la afya ulimwenguni WHO, na kushauri kuwa michezo hiyo, ambayo inatarajiwa kufanyika mjini Rio de Janeiro mwezi Agosti , ihamishiwe sehemu nyingine ama icheleweshwe.
"Hatari bila sababu ipo wakati watalii wa kigeni 500,000 kutoka nchi zote ambazo zinahudhuria michezo hiyo,wakipata virusi hivyo, na kurejea nyumbani kwao ambako mgonjwa huo unaweza kuwa maafa," barua hiyo imesema.
Wataalamu hao wa tabia za uhai ,Bioethicists, wanajifunza kuhusu matatizo ya kimaadili kutoka katika utafiti wa kibiolojia ama kiganga. Profesa Arthur Caplan, mkurugenzi wa kitengo cha maadili ya utabibu katika chuo kikuu cha mjini New York cha udaktari na mmoja kati ya wataalamu wanne ambao wameandika barua hiyo, amesema ana shaka iwapo Brazil ina vifaa vya kuweza kuulinda umma na wakati huo huo ana shaka ya "uhakika wa jumla " kutoka maafisa wa afya ya umma.

Hatari ni kubwa Ikidokeza kuhusu "wasiwasi mkubwa kwa ajili ya afya duniani", barua hiyo pia imesema , "Virusi vya Brazil vya Zika vinaathiri afya kwa njia ambayo sayansi haijachunguza hapo kabla." 

Akizungumza katika chakula cha mchana katika klabu ya taifa ya waandishi habari mjini Washington siku ya Alhamis, Frieden amesema hakuna sababu ya kuchelewesha michezo ya Olimpiki.

Barua hiyo imetoa wito kwa shirika la afya WHO kuunda kundi huru litakalotoa ushauri kwa shirika hilo na kamati ya kimataifa ya olimpiki. "Naamini kuhusu kuridhia baada ya kupata habari," Caplan amesema katika mahojiano. "Tuwe na kikundi cha wanasayansi huru watakaoangalia kuhusu hili na kumpa kila mtu nafasi ya kusikia mawazo tofauti."
Alikuwa akitoa maelezo kuhusu kujibu waraka wa profesa mmoja wa Canada uliochapishwa mapema mwezi huu katika mapitio ya afya ya jarida la Harvard ambao umetoa wito wa michezo hiyo kufutwa ama ihamishiwe kwingine kwasababu inaweza kuwa chombo cha kusambaza virusi vya Zika.
"Hatari sio lazima kuwa iko juu kuliko kwa mwanamke mjamzito," Frieden amesema. Maambukizi ya Zika kwa mwanamke mjamzito yameonesha kuwa ni sababu ya kuzaliwa watoto wenye athari pamoja na watoto wenye matatizo makubwa ya ubongo.
Chanzo:DW Kiswahili

Chid Benz: Sijatoroka Rehab, niko Studio

Chid Benz: Sijatoroka Rehab, niko Studio

Posted in ,
No comments
By danielmjema.blogspot.com
BAADA ya kuwepo kwa taarifa kwenye baadhi ya vyombo vya habari na mitandao kwamba, Rapa Chid Benz ametoroka Rehab, mjini Bagamoyo, nchini Tanzania, alikokuwa akipata tiba ya kuacha madawa ya kulevya, Rapa amekanusha vikali na kudai taarifa hizo ni za kupuuzwa.

Akiongea na East Africa Radio Chid Benz 'King Kong' amesema si kweli kwamba ametoroka, isipokuwa ameruhusiwa kutoka rehab.

“Wameongea uongo hao wajinga, nimeachana nao kwa sababu hatuwezi kubishana nao, mi nimetoka niko sawa, nipo fresh na siwezi kubishana na magazeti, na sasa hivi nipo studio nataka niingie kurekodi, kwa hiyo sio kweli kama nimetoroka rehab, nimetoka kwa sababu nimeruhusiwa”, alisema Chid Benz.


Hata hivyo East Africa Radio iliamua kumtafuta mtu wa karibu wa Chid Benz (Madee) ambaye naye yupo chini ya Babu Tale, na kuthibitisha taarifa hizo kuwa hajatoroka kweli.


Chid Benz alipelekwa rehab Bagamoyo mwezi wa 3 mwaka huu, baada ya meneja wa TipTop kujitolea kumsaidia kuacha matumizi ya madawa ya kulevya, ambayo yalikuwa yameshamuathiri.

Ukivuta sigara kwenye maeneo ya umma, mighahawa na maeneo ya burudani faini dola 60 nchini Uganda

Ukivuta sigara kwenye maeneo ya umma, mighahawa na maeneo ya burudani faini dola 60 nchini Uganda

No comments
By danielmjema.blogspot.com
Sheria mpya kali dhidi ya uvutaji na mauzo ya bidhaa za tumbaku zimeanza kutekelezwa nchini Uganda. Watu wanaovuta sigara wakiwa maeneo ya burudani na migahawa sasa watapigwa faini ya dola 60 au kifungo cha hadi miezi miwili jela.
Pia wavutaji sigara watahitajika kuwa umbali wa takriban mita 50 kutoka maeneo ya umma kama vile shule na hospitali.Sheria hizo pia zinapiga marufuku kuuzwa kwa sigara za elektroniki pamoja na shisha ambavyo ni maarufu kwenye maeneo ya burudani mjini Kampala.
Serikali pia imepiga marufuku kuuzwa kwa sigara moja na kudhibiti zaidi matangazo ya sigara na kuzwa kwa bidhaa za tumbaku kwa watu walio chini ya umri wa miaka 21.

Watoto waanza kupewa chanjo ya Rubella nchini Kenya

Watoto waanza kupewa chanjo ya Rubella nchini Kenya

No comments
By danielmjema.blogspot.com
Wizara ya afya nchini imeanzisha kampeni ya kitaifa ya kutoa chanjo kwa watoto dhidi ya maradhi ya ukambi na rubella. Maafisa wa afya watakuwa wakiwalenga watoto wa umri wa miezi tisa hadi miaka 14.

Kampeni hiyo imeanzishwa baada ya kuongezeka pakubwa kwa visa vya maambukizi ya maradhi hayo yanayosababisha na virusi, hasa visa vya Rubella.
Wazazi wametakiwa kuwapeleka watoto wao walio umri wa na miezi 9 hadi miaka 14 katika vituo vya afya vya serikali kuanzia hii leo mpaka tarehe 24. Dkt Sultan Matendechero ni Mkuu wa mradi wa kitengo cha magonjwa ya kitropiki yaliyopuuzwa kutoka wizara ya Afya nchini Kenya.
Anaeleza umuhimu wa chanjo hii. Maafisa wa afya wanasema karibu Wakenya 400 wamekuwa wakipatikana na virusi vya rubella kila mwaka. Kwa kawaida, chanjo hiyo hupewa watoto wa umri wa kati ya miezi 9 na 18.

DAWA YA KUREFUSHA MAISHA YAGUNDULIKA

DAWA YA KUREFUSHA MAISHA YAGUNDULIKA

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com
Dawa inayotumika kwa matibabu ya kawaida huenda ikategua kitendawili cha kurefusha maisha na kuzuia uzee. Hii ni kwa mujibu wa utafiti mpya, ambao ulibainisha kwamba viwango vya chini vya dawa aina ya Lithium vilisaidia kurefusha maisha ya nzi waliowekwa kwenye maabara.

Wanasayansi wamesema utafiti huu unatoa matumaini ya kutoa dawa kuwasaidia watu kuishi maisha marefu na yenye afya. Lithium inatumika katika matibabu ya matatizo ya akili, kama mfadhaiko, na kusongwa na mawazo.

Hata hivyo ina madhara makubwa ikiwa itatumika kwa viwango vya juu. Haijulikani jinsi Lithium inavyotibu matatizo ya akili, lakini alipopewanzi, dawa hiyo ilisaidia kurefusha maisha yao.

Hata hivyo watafiti wamesisitiza lazima dawa hii kutumiwa kwa viwango vya chini zaidi, kwani viwango vya juu vinaweza kuleta maafa. Dkt Ivana Bjedov mmoja wa watafiti kutoka taasisi ya matibabu ya saratani amesema dawa hii itasaidia afya kwa wazee sawa na kuzuia magonjwa kama vile ugonjwa wa kutetemeka 'Parkinson'.

Kando na matatizo ya akili Lithium imetumika kutibu maumivu makali ya kichwa 'Migraines' na ugonjwa wa jongo unaomfanya mtu kuvimba viungo hasa wakati wa baridi.

AFYACHECK: NJIA SAHIHI YA KUACHA SIGARA

AFYACHECK: NJIA SAHIHI YA KUACHA SIGARA

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com
Utafiti wa karibuni zaidi umeonesha kwamba njia bora zaidi ya kuacha uraibu wa kuvuta sigara ni kuacha mara moja. Utafiti ambao matokeo yake yamechapishwa katika jarida la kimatibabu la Annals of Internal Medicine unasema washiriki walioacha mara moja walikuwa na uwezekano mara 25% zaidi ya kutovuta sigara nusu mwaka baada ya kuachana na uraibu huo wakilinganishwa na walioacha uvutaji sigara taratibu taratibu.

Idara ya Afya ya Taifa Uingereza inasema njia bora zaidi ni kutenga siku fulani kuwa ya kuacha kuvuta sigara. Weka ahadi, tenga siku na uhakikishe umefanya hivyo siku hiyo, idara hiyo inashauri. Utafiti huo wa karibuni uliofadhiliwa na Wakfu wa Moyo wa Uingereza ulihusisha washiriki 700 wa kujitolea.

Waliwekwa kwenye makundi mawili, moja la kuacha kuvuta sigara mara moja na jingine la kuacha asteaste. Baada ya miezi sita, ni 15.5% ya washiriki walioacha kuvuta sigara taratibu taratibu waliokuwa bado hawavuti sigara wakilinganishwa na 22% kwenye kundi la walioacha kuvuta sigara mara moja.

Kiongozi wa utafiti huo Dkt Nicola Lindson-Hawley, kutoka Chuo Kikuu cha Oxford alisema: "Tofauti inaonekana ni kama inatokana na kutatizika kwa watu katika kupunguza uvutaji sigara. Hili liliwapa jambo la ziada la kufanya, ambalo huenda liliwafanya kuacha kabisa mpango wao wa kuacha uvutaji sigara.”

Ingawa wengi wa washiriki walisema wangependelea sana kuacha uvutaji sigara, bado wale waliofanikiwa zaidi kuacha kabisa uvutaji sigara walikuwa wale walioacha Dkt Lindson-Hawley hata hivyo alisema ni heri kupunguza uvutaji sigara kuliko kutochukua hatua yoyote. Washiriki wote walipewa ushauri pamoja na vitu vya kuwasaidia kukabiliana na makali ya kuacha uvutaji sigara.

KINGA YA MWILI KUTIBU SARATANI?

KINGA YA MWILI KUTIBU SARATANI?

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com
Wanasayansi wanaamini wamegundua njia ya kuimarisha kinga ya mwili kuangamiza saratani. Watafiti katika chuo kikuu cha London wamepata njia ya kutafuta alama katika uvimbe,na kuiruhusu kinga ya mwili kuulenga ugojwa huo.

Lakini mbinu hiyo ya kibinafsi ilioripotiwa katika jarida la sayansi ni ghali mno na haijajaribiwa miongoni mwa wagonjwa. Wataalam wamesema kuwa mpango huo ni mzuri lakini huenda ni mgumu kutekeleza.

Lakini watafiti ambao kazi yao imefadhiliwa na kituo cha utafiti nchini Uingereza ,wanaamini ugunduzi wao huenda ukawa uti wa mgongo wa tiba mpya na inataraji kuijaribu mbinu hiyo katika wagonjwa katika kipindi cha miaka miwili. Wanaamini kwa kuchunguza chembe chembe za vinasaba vya DNA,wataweza kubuni tiba.

UNFPA WAKABIDHI MSAADA WA GARI LA WAGONJWA, JENGO NA VIFAA VYA UPASUAJI GEITA

UNFPA WAKABIDHI MSAADA WA GARI LA WAGONJWA, JENGO NA VIFAA VYA UPASUAJI GEITA

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com
DSC_0048
Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa (wa pili kulia) akisalimiana na Meneja Biashara Idara ya Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Grace Lyon mara baada ya kuwasili kwenye maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kutokomeza Fistula yaliyofanyika kitaifa katika Wilaya Mbogwe, Geita. Kulia ni Kaimu Mkuu wa wilaya ya Mbogwe, Amani Mwenegoha na Kushoto ni Naibu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT, Haika Mawalla na wa pili kushoto ni Mwakilishi msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu duniani (UNFPA) nchini Tanzania, Dkt.Rutasha Dadi.(Picha zote na Zainul Mzige wa modewjiblog)

Na Zainul Mzige wa modewjiblog
Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu Duniani(UNFPA) limekabidhi msaada wa gari la wagonjwa lenye thamani ya shilingi milioni 80 katika kituo cha afya cha Masumbwe kilichopo katika Wilaya mpya ya Mbogwe Mkoani Geita.

Shirika hilo limetoa vifaa vya kutoa huduma ya upasuaji vyenye thamani ya shilingi milioni 250 katika kituo hicho mbali na kutumia shilingi zaidi ya shilingi milioni 100 kusadia ujenzi wa jengo la upasuaji katika kituo hicho.

Misaada hiyo kwa pamoja ilikabidhiwa Jumamosi iliyopita katika halfa ambaye mgeni rasmi alikuwa ni Naibu Waziri wa Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa.

Majaliwa alishuruku UNFPA kwa msaada huo na kutaka utumike vizuri ili kuboresha huduma za afya kwa wananchi. “ Nimeona vifaa vya hospitali vingi na vya gharama kubwa, sasa ni wajibu wetu kuvitunza na kuvitumia vizuri. Mfano gari tu limegharimu shilingi milioni 80. Huu ni msaada mkubwa sana na kwa niaba ya serikali nawashukuru sana UNPFA, tutaendelea kushirikiana”, alisema Majaliwa .

Hata hivyo Naibu Waziri huyo aliwaagiza vingozi wa Halmashuri ya Wilaya ya Mbogwe kuhakikisha kuwa gari hilo linatumika kusafirisha wagonjwa tu na sio vinginevyo.
DSC_0062
Naibu Ofisa Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT, Haika Mawalla (kushoto) na Mwakilishi msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu duniani (UNFPA) nchini Tanzania, Dkt.Rutasha Dadi wakipitia ratiba ya sherehe za maadhimisho ya siku ya kimataifa ya kutokomeza Fistula ambapo kitaifa yamefanyika katika Wilaya Mbogwe, Geita.

“ Gari hili litumike kwa matumizi ya wagonjwa tu. Sitegemei kusikia kuwa linapeleka wafanyakazi sokoni kununua nyanya. Na Mkurugenzi atenge bajeti ya mafuta ya gari hili muda wote”, aliagiza Majaliwa.

Hafla ya makabidhiano ya misaada hiyo ilienda sambamba na maadhimisho ya siku ya kutokomeza tatizo la ugonjwa wa Fistula duniani yaliyofanyakia kitaifa katika viwanja vya shule ya msingi Masumbwe katika Wilaya ya Mbogwe , Mkoani Geita.

Akizungumuza katika hafla hiyo Mwakilishi msaidizi wa Shirika la UNFPA, Dkt. Rutosha Dadi alisema msaada wa vifaa walivyotoa utasadia kumaliza tatizo la Fistula na kuboresha huduma zingine za afya. “ Tumefanya ukarabati mkubwa sana katika jengo la upasuaji na kutoa vifaa vya kisasa kama vile Ultrasound”, alisema Dkt. Dadi.
DSC_0072
Kaimu Mkuu wa wilaya ya Mbogwe, Amani Mwenegoha (wa nne kulia) akitoa salamu na kumkaribisha mgeni rasmi kuzungumza na umati wa wakazi wa Mbogwe waliokusanyika kwenye maadhimisho hayo. Kutoka kushoto ni Meneja wa miradi ya AMREF, kanda ya ziwa Dkt. Awene Gavyole, Makamu Afisa Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT, Bi. Haika Mawalla, Mwakilishi msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu duniani (UNFPA) nchini Tanzania, Dkt. Rutasha Dadi, Katibu Tawala wa mkoa wa Geita, Charles Palanjo, mgeni rasmi Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa, Mganga Mkuu wa mkoa wa Geita, Joseph Kisalla, Meneja Biashara Idara ya Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Grace Lyon pamoja na Mbunge wa jimbo la Mbogwe, Mh. Augustino Masele.
DSC_0204
Mwakilishi msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu duniani (UNFPA) nchini Tanzania, Dkt. Rutasha Dadi akitoa salamu za Umoja wa Mataifa kwenye maadhimisho ya siku ya Kimataifa ya Fistula ambapo kitaifa yamefanyika wilayani Mbogwe mkoa wa Geita.
IMG_1150
Mwakilishi msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu duniani (UNFPA) nchini Tanzania, Dkt. Rutasha Dadi akisisitiza jambo wakati wa kutoa salamu za Umoja wa Mataifa.
DSC_0149
Makamu Afisa Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT, Bi. Haika Mawalla akizungumza na wakazi wa Mbogwe ambapo aliwataka kufika katika vituo vya afya vilivyokaribu na makazi yao kufanyiwa uchunguzi wa ugonjwa wa Fistula pindi wanaonapo dalili na moja kwa moja kuwasiliana na Hospitali yake inayotoa huduma za matibabu bure ikiwemo usafiri na malazi mpaka mgonjwa anapopona na kumrejesha anakoishi.
IMG_1089
Meneja Biashara Idara ya Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Grace Lyon akitoa salamu za Vodacom ilivyobega bega katika kupamba na ugonjwa wa Fistula kabla ya kukabidhi hundi yenye thamani ya shilingi Milioni 100/- kutoka Taasisi ya Vodacom Foundation kwa ajili ya kutokomeza ugonjwa Fistula nchini wakati wa maadhimisho yanayofanyika kila mwaka Mei 23.
DSC_0248
Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)Mh. Kassim Majaliwa (kulia) akikabidhiwa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 100/- na Meneja Biashara Idara ya Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Grace Lyon, kwa niaba ya hospitali ya CCBRT kwa ajili ya kampeni ya kutokomeza Fistula nchini wakati wa maadhimisho ya Kimataifa ya Fistula yaliyofanyika kitaifa katika wilaya ya Mbogwe mkoani Geita mwishoni mwa wiki, Katikati ni Makamu Afisa Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT, Bi. Haika Mawalla.
DSC_0254
Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)Mh. Kassim Majaliwa akikabidhi hundi yenye thamani ya shilingi milioni 100/- kwa Makamu Afisa Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT, Bi. Haika Mawalla (kushoto) na anayeshuhudia tukio hilo ni Meneja Biashara Idara ya Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Grace Lyon.
DSC_0182
Bi. Esther Ernest akitoa ushuhuda wake baada ya kuteseka na ugonjwa wa Fistula kwa takribani miaka 8 na jinsi jamii ilivyomnyanyapaa akiwemo mume wake hadi alipopatiwa matibabu na kupona kabisa hali iliyompelekea kurudisha furaha na nuru katika uso wake wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya Fistula ambapo kitaifa imefanyika wilayani Mbogwe mkoani Geita.
IMG_0928
Kikundi cha maigizo cha Mrisho Mpoto kikitoa elimu kwa njia ya maigizo jinsi Wanawake wanaosumbuliwa na ugonjwa wa Fistula wanavyonyanyapaliwa na waume zao na kudhalilishwa kwa jamii ikiwemo kuitwa majina ya kila aina kutoka na kutokwa na haja ndogo muda wote bila breki.
IMG_0947
Mwigizaji wa kikundi cha sanaa za maigizo cha Mrisho Mpoto akilia kwa uchungu kutokana na kuugua ugonjwa wa Fistula na kunyanyapaliwa na mumewe wakati wa maadhimisho ya siku ya kimataifa ya Fistula ambapo kitaifa imefanyika wilayani Mbogwe mkoani Geita.
IMG_0969
Msanii mahiri wa sanaa ya kughani mashairi nchini Mrisho Mpoto akimliwaza Mwanamke anayenyanyapaliwa na mumewe kutokana na kuugua ugonjwa wa Fistula ambao unatibika bure kabisa bila gharama yoyote na Hospitali ya CCBRT.
IMG_1006
Mume wa mwanamke anayeumwa Fistula wakisoma vipeperushi vya CCBRT vinavyotoa elimu, dalili na nini cha kufanya pindi unapojigundua ni Fistula pamoja na jirani yake wakati wa mchezo wa maigizo kwenye maadhimisho hayo.
IMG_1009
Mrisho Mpoto akiendelea kutumia sanaa ya maigizo kuelemisha umati wa wakazi wa wilaya ya Mbogwe waliohudhuria maadhimisho hayo.
IMG_1030
Meneja Biashara Idara ya Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Grace Lyon (kushoto) na Mganga Mkuu wa wilaya ya Geita, Dkt. Joseph Kisalla wakifuatilia igizo la unyanyapaa kwenye jamii kwa wanawake wanaougua Fistula wakati wa maadhimisho hayo.
DSC_0170
Mgeni rasmi Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa akifurahi jambo kwenye maadhimisho hayo.
DSC_0235
Mgeni rasmi kwenye maadhimisho ya siku ya kimataifa ya Fistula Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa akimpongeza Balozi wa Fistula CCBRT, Elizabeth Jacob na kumkabidhi pesa taslimu Sh. 20,000/- kama motisha ya kazi anazofanya za kuwasafirisha wagonjwa wa Fistula jijini Dar es Salaam kwa matibabu.
DSC_0238
Balozi wa Fistula CCRT, Elizabeth Jacob akionyesha pesa alizokabidhiwa kama zawadi kutoka kwa mgeni rasmi Mh. Kassim Majaliwa.
DSC_0241
Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa akimpongeza na kumkabidhi pesa taslimu sh. 100,000/ kama motisha ya kazi anazofanya za kuelimisha jamii kwa kutumia sanaa na maigizo Mrisho Mpoto aliyekuwa akisheresha sherehe hizo.
DSC_0023
Makamu Afisa Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT, Bi. Haika Mawalla ( kushoto) na Meneja Biashara Idara ya Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Grace Lyon (kulia) wakimuangalia mtoto Nyambole Kulubone mwenye tatizo la mdomo wa Sungura akiwa amebebwa na mama yake Mariam Sanda (22) Mzazi huyo aliyehudhuria katika maadhimisho ya siku ya kimataifa ya Fistula aliahidiwa na Bi. Haika Mawalla (kushoto) mtoto wake atatibiwa bure katika hospitali CCBRT baada ya kusikia matangazo jirani na eneo liliofanyika sherehe hizo ambapo kitaifa katika Wilaya Mbogwe Geita.
DSC_0025
Mariam Sanda (22) akiwa amembeba mwanae mwenye mdomo wa Sungura.
DSC_0098
Baadhi ya umati wa wakazi wa Mbongwe waliohudhuria maadhimisho hayo.
IMG_0958
DSC_0101
IMG_0897
IMG_0891
IMG_1359
Burudani kutoka kwenye kikundi cha Mrisho Mpoto.
IMG_1393
DSC_0272
Mganga mfawidhi wa kituo cha Afya Masumbwe wilayani Mbogwe, Dkt. Petr Shilogile (kushoto) akisoma taarifa fupi ya ujenzi wa jengo la upasuaji katika kituo hicho kwa Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa uliofadhiliwa na Shirika linaloshughulikia Idadi ya Watu duniani (UNFPA) nchini Tanzania na ujenzi kusimamiwa na AMREF kabla ya kuzinduliwa rasmi. Kulia ni Mbunge wa jimbo la Mbogwe, Mh. Augustino Masele.
DSC_0275
Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa akifunua kitambaa kuzindua cha jiwe la msingi huku Mwakilishi msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu duniani (UNFPA) nchini Tanzania, Dkt. Rutasha Dadi (kulia) akishuhudia tukio hilo.
DSC_0277
Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa akisoma maneno yaliyoandikwa kwenye jiwe la msingi.
DSC_0281
Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa akikata utepe kuzindua jengo la upasuaji huku Mwakilishi msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu duniani (UNFPA) nchini Tanzania, Dkt. Rutasha Dadi akishuhudia tukio hilo.
DSC_0282
Sasa limezinduliwa rasmi.
DSC_0287
Mganga mfawidhi wa kituo cha Afya Masumbwe wilayani Mbogwe, Dkt. Peter Shilogile (kulia) akitoa maelezo kwenye chumba cha kujifungulia kina mama kilichowekwa vifaa vyote muhimu kwa Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa (wa tatu kushoto). Kutoka kushoto ni Kaimu Mkuu wa wilaya ya Mbogwe, Amani Mwenegoha, Mwakilishi msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu duniani (UNFPA) nchini Tanzania, Dkt. Rutasha Dadi.
DSC_0289
Mganga mfawidhi wa kituo cha Afya Masumbwe wilayani Mbogwe, Dkt. Peter Shilogile akitoa maelezo ya mashine ya kisasa ya kuongezea damu wakina mama watakaokua wakijifungulia kwenye kituo hicho kwa Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa.
DSC_0318
Wafadhali wa ujenzi na vifaa kwenye kituo hicho Mwakilishi msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu duniani (UNFPA) nchini Tanzania, Dkt. Rutasha Dadi akifafanua jambo kwa mgeni rasmi Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa baada ya kuzinduliwa kituo hicho cha afya. Kulia ni Mganga mfawidhi wa kituo cha Afya Masumbwe wilayani Mbogwe, Dkt. Peter Shilogile.
DSC_0340
Mganga mfawidhi wa kituo cha Afya Masumbwe wilayani Mbogwe, Dkt. Peter Shilogile akielezea changamoto waliozokuwa nazo hapo awali za kipimo cha "Ultra sound" kilichonunuliwa na UNFPA ambacho hivi sasa kitapatikana kituoni hapo kwa Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa.
DSC_0360
Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa akikata utepe kuzindua gari la wagonjwa (Ambulance) lenye thamani ya Tsh. Milioni 80 kwa ajili ya kubebea wakinamama wajawazito na watoto wanaohitaji huduma za dharula za upasuaji kutoka vituo vyote vya kutolea huduma za afya katika wilaya ya Mbogwe kwa ufadhili wa Shirika la UNFPA. Kushoto anayeshuhudia tukio hilo ni Mwakilishi msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu duniani (UNFPA) nchini Tanzania, Dkt. Rutasha Dadi.
DSC_0362
Mh. Kassim Majaliwa na Dkt. Rutasha Dadi wakipiga makofi.
DSC_0373
Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa akijaribu gari hilo.
DSC_0386
Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa akitoa angalizo la matumizi mabovu kwa DED wa Mbogwe na wafanyakazi wa kituo hicho cha afya.
DSC_0388
Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa akikabidhi funguo za gari hilo la kubebea wagonjwa (Ambulance) kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya Mbogwe, Abdala Idd Mfaume.
DSC_0411
Mgeni rasmi Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa katika picha ya pamoja na wafanyakazi wa kituo hicho cha afya na uongozi wa halmashauri ya wilaya ya Mbogwe mara baada ya makabidhiano hayo.
DSC_0421
Mgeni rasmi Naibu Waziri ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mh. Kassim Majaliwa katika picha ya pamoja na Muhanga wa Fistula, Bi. Ester Ernest (walioketi kulia), Balozi wa Fistula CCBRT, Bi. Elizabeth Jacob (wa pili kushoto), Katibu Tawala mkoa wa Geita, Charles Palanjo (kushoto) na waliosimama kutoka kushoto ni Makamu Afisa Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya CCBRT, Bi. Haika Mawalla, Mwakilishi msaidizi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu duniani (UNFPA) nchini Tanzania, Dkt. Rutasha Dadi, MC pamoja na Meneja Biashara Idara ya Uhusiano wa Vodacom Tanzania, Grace Lyon.

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .