Ukivuta sigara kwenye maeneo ya umma, mighahawa na maeneo ya burudani faini dola 60 nchini Uganda
Posted in
afrika mashariki
,
Afya
No comments
Thursday, May 19, 2016
By
danielmjema.blogspot.com
Sheria mpya kali dhidi ya uvutaji na mauzo ya bidhaa za tumbaku zimeanza kutekelezwa nchini Uganda. Watu wanaovuta sigara wakiwa maeneo ya burudani na migahawa sasa watapigwa faini ya dola 60 au kifungo cha hadi miezi miwili jela.
Pia wavutaji sigara watahitajika kuwa umbali wa takriban mita 50 kutoka maeneo ya umma kama vile shule na hospitali.Sheria hizo pia zinapiga marufuku kuuzwa kwa sigara za elektroniki pamoja na shisha ambavyo ni maarufu kwenye maeneo ya burudani mjini Kampala.
Serikali pia imepiga marufuku kuuzwa kwa sigara moja na kudhibiti zaidi matangazo ya sigara na kuzwa kwa bidhaa za tumbaku kwa watu walio chini ya umri wa miaka 21.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :