Mabaki ya ndege ya EgyptAir yapatikana
Posted in
Ajali
No comments
Thursday, May 19, 2016
By
danielmjema.blogspot.com
Duru za kampuni ya ndege ya EGYPTAIR zimesema kuwa wizara ya usafiri wa anga nchini humo imepokea barua rasmi kutoka kwa wizara ya maswala ya kigeni nchini Misri inayothibitisha kupatikana kwa mabaki ya ndege iliotoweka ya MS 804 karibu na kisiwa cha Karpathos.
Hivyobasi kampuni hiyo imetuma salamu za rambi rambi kwa familia za abiria na wafanyikazi waliokuwa wakiabiri ndege hiyo. Tayari familia za abiria hao pamoja na wafanyikazi wameelezewa kuhusu tukio hilo jipya.
Kwa sasa kundi la wachunguzi wa Misri wakishirikiana na wenzao wa Ugiriki wanaendelea kutafuta mabaki mengine ya ndege hiyo. Ndege hiyo ilikuwa imepaa kutoka uwanja wa ndege wa Charles de Gaulle, Paris ikiwa na raia 15 wa Ufaransa.
Ndege hiyo pia ilikuwa na raia 30 wa Misri, raia 2 wa Iraq na raia mmoja mmoja kutoka Uingereza, Canada, Ubelgiji, Kuwait, Saudi Arabia, Algeria, Sudan, Chad na Ureno.Awalia rais wa Ufaransa Francois Hollande alikuwa amesema kuwa ndege hiyo ilianguka.
Ugiriki imesema ndege hiyo ilifanya mizunguko miwili ya ghafla angani kabla ya kutoweka kwenye rada yao. Rais wa Ufaransa Francois Hollande amesema huenda ndege hiyo ilianguka. Shughuli za kutafuta manusura zaendelea.
Waziri wa ulinzi nchini Ugiriki Panos Kammenos amesema ndege hiyo aina ya Airbus ilifanya mizunguko miwili ya ghafla angani na kushuka ghafla kutoka futi 37,000 hadi futi 15,000 angani, kisha ikatoweka kutoka kwenye mtambo wao wa rada.
Rais wa Ufaransa Francois Hollande amesema huenda ndege hiyo ilianguka katika bahari Mediterenia katikati ya visiwa vya Ugiriki na Misri. Amekariri kuwa uchunguzi kamili unahitajika kubaini mkasa huo umesababishwa na nini.
Maafisa nchini Misri wamesema kuwa ndege ya taifa hilo iliyokuwa ikisafiri kutoka Paris Ufaransa kuelekea Cairo imetoweka na huenda imeanguka katika bahari ya Mediterrania. Ndege hiyo ya shirika la EgyptAir ilikuwa na jumla ya watu 66 miongoni mwao wahudumu wa ndege hiyo. Shughuli za kutafuta mabaki ya ndege na manusura imeanzishwa.
Ndege hiyo ilitoweka na kutoonekana tena kwenye mtambo wa rada dakika 45 kabla ya muda kamili ambao ilitarajiwa kutua katika uwanja wa ndege wa Cairo. Maafisa nchini Misri wanasema ndege hiyo ilianguka mwendo wa saa nane usiku majira ya Misri, jumla ya saa tatu na nusu tangu kupaa kutoka uwanja wa ndege wa Charles de Gaulle mjini Paris. Hii ni muda mfupi baada ya ndege hiyo kutoweka na kutoonekana tena kwenye mtambo wa rada maili kumi ndani ya anga ya Misri.
Sababu ya kutoweka ni gani?
Chanzo cha ndege hiyo kuanguka hakijabainika. Awali kulitokea ripoti kwamba idara ya jeshi la Misri ilipokea taarifa ya kuonyesha kuwa ndege hiyo ilikumbwa na hali ya dharura. Lakini baadaye maafisa wamesema hakukuwa na wito wa dharura kutoka kwa ndege hiyo. Hali ambayo imeibua mkanganyiko. Waziri mkuu wa Misri Sherif Ismail alipoulizwa uwezekano wa njama ya kigaidi katika mkasa huo amejibu kuwa hawapuuzilii sababu yoyote inayoweza kukisiwa kusababisha ndege hiyo kuanguka.
"Kile tunachoweza kusema kwa sasa ni kuwa tulipoteza mawasiliano kwa saa fulani na sasa tunatafuta eneo hili… jeshi limetangaza kuwa lilipokea ishara wala si wito wa dharura lakini hiyo pia inachunguzwa na kuna idara za jeshi na wanajeshi wa majini wanapekua kila eneo kwa ushirkiano na Wagiriki, zipo ndege za Ugiriki zimehusishwa kwenye msako… hatuwezi kuthibitisha au kukana chochocte kwa wakati huu kuwa ndicho kimesababisha, hadi uchunguzi dhidi ya suala ukamilike tunaweza kusema hali ni nini?"
Kwa sasa vikosi vya usalama vya Misri vikishirikiana na vikosi kutoka Ugiriki vinaendeleza shughuli za kutafuta manusura, ndege hiyo au mabaki yake katika bahari ya Mediterania. Jamaa za abiria waliokuwemo ndani ya ndege wamefika katika uwanja wa ndege wa Cairo wakisubiri habari zaidi kuhusu wapendwa wao. Miongoni mwa waliokuwemo ndani ya ndege hiyo aina ya MS804 ni raia 30 wa Misri, wafaransa 15, wairaqi 2, watoto wawili na mmoja mdogo, Uingereza, Kuwait, Ubelgiji, Saudi Arabia, Sudan, Chad, Ureno, Algeria na Canada wakiwa na raia mmoja mmoja.
Kulingana na shirika la ndege hiyo, nahodha wa ndege kwa jina Said Ali Shaqir ana tajriba ya kuendesha ndege kwa zaidi ya saa elfu sita, na miongoni mwa ndege hizo 2000 zikiwa kubwa aina ya Airbus.
Mwandishi: John Juma/APE/RTRE/AFPE/DPE
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :