Chid Benz: Sijatoroka Rehab, niko Studio

Posted in ,
No comments
Friday, May 27, 2016 By danielmjema.blogspot.com

BAADA ya kuwepo kwa taarifa kwenye baadhi ya vyombo vya habari na mitandao kwamba, Rapa Chid Benz ametoroka Rehab, mjini Bagamoyo, nchini Tanzania, alikokuwa akipata tiba ya kuacha madawa ya kulevya, Rapa amekanusha vikali na kudai taarifa hizo ni za kupuuzwa.

Akiongea na East Africa Radio Chid Benz 'King Kong' amesema si kweli kwamba ametoroka, isipokuwa ameruhusiwa kutoka rehab.

“Wameongea uongo hao wajinga, nimeachana nao kwa sababu hatuwezi kubishana nao, mi nimetoka niko sawa, nipo fresh na siwezi kubishana na magazeti, na sasa hivi nipo studio nataka niingie kurekodi, kwa hiyo sio kweli kama nimetoroka rehab, nimetoka kwa sababu nimeruhusiwa”, alisema Chid Benz.


Hata hivyo East Africa Radio iliamua kumtafuta mtu wa karibu wa Chid Benz (Madee) ambaye naye yupo chini ya Babu Tale, na kuthibitisha taarifa hizo kuwa hajatoroka kweli.


Chid Benz alipelekwa rehab Bagamoyo mwezi wa 3 mwaka huu, baada ya meneja wa TipTop kujitolea kumsaidia kuacha matumizi ya madawa ya kulevya, ambayo yalikuwa yameshamuathiri.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .