UKIMWI ya Paka yagundulika nchini Kenya

Posted in
No comments
Friday, June 3, 2016 By danielmjema.blogspot.com

Wanasayansi humu nchini wamegundua virusi hatari aina ya FIV vinaavyofanana kabisa na virusi vya HIV vinavyosababisha UKIMWI vimegunduliwa katika paka mmoja ikiwa ni baada ya uchunguzi wa kina wa damu ya paka huyo kuthibitisha uwepo wa viini vinavyofanana kabisa na vile vinavyoathiri binaadamu.
Wafugaji wa paka na wanyama wa nyumbani wametakiwa kuwapeleka wanyama wao kufanyiwa uchunguzi wa afya wanapowashuku wanyama wao wanaugua, virusi hivyo vinaitwa FIV (Feline Immunodefficiency Virus) na wanasema ugonjwa huu sio mgeni kwa wanyama.
kwa mujibu wa BBC Swahili, Mwaka wa 1986 madaktari wa Marekani waligundua virusi vilivyofanana kwa karibu na vile vinavyoambukiza binadamu vya HIV lakini hii ndio mara ya kwanza kwa virusi hivyo kugunduliwa nchini Kenya.
Madaktari wa maabara ya Lancet Nairobi waligundua kuwa virusi hivyo vinasababisha ukosefu wa kinga mwilini na kudhoofisha afya ya wanyama hao wanaopendwa na kuishi majumbani lakini hata hivyo waliwahakikishia wafugaji wa paka kuwa hakuna ushuhuda wowote wa maambukizi kutoka kwa paka hao kwenda kwa binadamu.
Daktari Dhaval Shah badala yake amewashauri wafugaji wa paka kuwafungia paka wao ndani ili kuwazuia wasijamiiane na wale paka wanaorandaranda mitaani ambao huenda wameambukizwa UKIMWI wa paka ambao unaambukizwa kupitia mate na mkwaruzano paka wanapopigana.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .