AFYACHECK: NJIA SAHIHI YA KUACHA SIGARA
Posted in
Afya
No comments
Tuesday, March 15, 2016
By
danielmjema.blogspot.com

Idara ya Afya ya Taifa Uingereza inasema njia bora zaidi ni kutenga siku fulani kuwa ya kuacha kuvuta sigara. Weka ahadi, tenga siku na uhakikishe umefanya hivyo siku hiyo, idara hiyo inashauri. Utafiti huo wa karibuni uliofadhiliwa na Wakfu wa Moyo wa Uingereza ulihusisha washiriki 700 wa kujitolea.
Waliwekwa kwenye makundi mawili, moja la kuacha kuvuta sigara mara moja na jingine la kuacha asteaste. Baada
ya miezi sita, ni 15.5% ya washiriki walioacha kuvuta sigara taratibu
taratibu waliokuwa bado hawavuti sigara wakilinganishwa na 22% kwenye
kundi la walioacha kuvuta sigara mara moja.
Kiongozi wa utafiti huo Dkt Nicola Lindson-Hawley, kutoka Chuo Kikuu
cha Oxford alisema: "Tofauti inaonekana ni kama inatokana na kutatizika
kwa watu katika kupunguza uvutaji sigara. Hili liliwapa jambo la ziada
la kufanya, ambalo huenda liliwafanya kuacha kabisa mpango wao wa kuacha
uvutaji sigara.”
Ingawa wengi wa washiriki walisema wangependelea
sana kuacha uvutaji sigara, bado wale waliofanikiwa zaidi kuacha kabisa
uvutaji sigara walikuwa wale walioacha Dkt Lindson-Hawley hata hivyo
alisema ni heri kupunguza uvutaji sigara kuliko kutochukua hatua yoyote. Washiriki wote walipewa ushauri pamoja na vitu vya kuwasaidia kukabiliana na makali ya kuacha uvutaji sigara.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :