Watoto waanza kupewa chanjo ya Rubella nchini Kenya

No comments
Monday, May 16, 2016 By danielmjema.blogspot.com

Wizara ya afya nchini imeanzisha kampeni ya kitaifa ya kutoa chanjo kwa watoto dhidi ya maradhi ya ukambi na rubella. Maafisa wa afya watakuwa wakiwalenga watoto wa umri wa miezi tisa hadi miaka 14.

Kampeni hiyo imeanzishwa baada ya kuongezeka pakubwa kwa visa vya maambukizi ya maradhi hayo yanayosababisha na virusi, hasa visa vya Rubella.
Wazazi wametakiwa kuwapeleka watoto wao walio umri wa na miezi 9 hadi miaka 14 katika vituo vya afya vya serikali kuanzia hii leo mpaka tarehe 24. Dkt Sultan Matendechero ni Mkuu wa mradi wa kitengo cha magonjwa ya kitropiki yaliyopuuzwa kutoka wizara ya Afya nchini Kenya.
Anaeleza umuhimu wa chanjo hii. Maafisa wa afya wanasema karibu Wakenya 400 wamekuwa wakipatikana na virusi vya rubella kila mwaka. Kwa kawaida, chanjo hiyo hupewa watoto wa umri wa kati ya miezi 9 na 18.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .