Tanzania kinara unyanyasaji kwa watu wenye Ualbino
Posted in
afrika mashariki
,
Afya
No comments
Monday, June 20, 2016
By
danielmjema.blogspot.com
Na Mwandishi wetu, Dar es salaam
Pamoja
na juhudi ambazo serikali ya Tanzania. imekuwa ikizifanya ili kuhakikisha watu wenye ulemavu wa ngozi (albino) wanakuwa salama na amani lakini bado Taifa hilo, lililoko katika jumuiya ya Afrika mashariki, inaendelea
kuwa nchi ya hatari kwa watu hao kwa kuwa katika orodha ya nchi ambazo
zina kiwango kikubwa cha unyanyasaji.
Akizungumza na waandishi
wa habari katika kilele cha kongamano la kikanda kwa ajili ya hatua
kuhusu ulemavu wa ngozi Afrika lililofanyika Dar es Salaam, Mtaalam huru
wa Umoja wa mataifa kuhusu Ulemavu wa Ngozi, Ikponwosa Ero alisema kuwa
kwa ripoti ambazo wamekuwa wakizipokea inaonyesha Tanzania ni moja ya
nchi ambazo zina unyanyasaji kwa watu wenye ualbino.
"Tangu
nimeingia sijawahi kufanya uchunguzi hata katika matokeo ya uchunguzi wa
nchi 29 sijaujua sana lakini kwa taarifa ambazo nimekuwa nikipata
kutoka kwa taasisi mbalimbali inaonyesha Tanzania ni unyanyasaji wa hali
ya juu kwa watu walio na uablino," alisema Ero.
Nae
Mwenyekiti wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora, Bahame Nyanguga
alisema katika kongamano hilo wametoka na maazimio ambayo wanaiomba
serikali iweze kuyafanya ili kuwezesha watu wenye ualbino kuwa na
usalama wa uhakika.
"Tumejadili mambo mengi lakini tunaiomba
serikali ihusike moja kwa moja kupinga unyanyasaji, ukatili na ubaguzi
nia tunaiona kwahiyo tunaomba waendelee kuwa hivyo na pia waongeze
bajeti na zaidi katika matibabu kwa watu wenye ualbino," alisema
Nyanduga.
Kwa upande wa Shirika la Umoja wa Mataifa kupitia
Mratibu Mkazi wa mashirika hayo, Alvaro Rodriguez alisema ni wataendelea
kuwasaidia watu wenye ualbino ili kuwezesha kupunguza changamoto ambazo
zinawakabili.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :