Showing posts with label Sanaa. Show all posts
Showing posts with label Sanaa. Show all posts

SALAMU YA DIAMOND KWA WASANII KATIKA KUSHEREHEKEA SIKU YA UHURU......NI SHEEEEDAH

SALAMU YA DIAMOND KWA WASANII KATIKA KUSHEREHEKEA SIKU YA UHURU......NI SHEEEEDAH

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com

Instead of artists being role models and agents of unity, bringing our countries together to build a strong, prosperous peaceful continent, Africa. We are the first to instigate hate and regionalism. 

In this manner are we really building Africa? What is our fate? Continuing divide and rule inherited from the colonial era... Anyway, Happy Independence day Tanzania..

( Badala ya wasanii kuwa ndio Mfano bora wa kuweka karibu Nchi zao na kujenga Africa yenye upendo na Amani...eti wao ndio Wanakua chanzo cha Kutenganisha nchi zao...Namna hii kweli tutajenga Africa? Anyway, Happy Independence day Tanzania....)

MWANAAFA MWINZAGO AIBUKA KINARA WA SHINDANO LA TANZANIA MOVIE TALENTS (TMT) 2014 NA KUONDOKA NA KITITA CHA SHILINGI MILIONI 50 ZA KITANZANIA

MWANAAFA MWINZAGO AIBUKA KINARA WA SHINDANO LA TANZANIA MOVIE TALENTS (TMT) 2014 NA KUONDOKA NA KITITA CHA SHILINGI MILIONI 50 ZA KITANZANIA

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com


Host Wa TMT 2014 Joti akimpongeza Baba wa Mwanaafa Mwizago kwa Mwanae kuibuka Mshindi wa Fainali ya Tanzania Movie Talents (TMT) na kuibuka na kitita cha Shilingi Milioni 50 za Kitanzania
Mwenyekiti wa Makampuni ya Proin, Bw Johnson Lukaza akitoa neno kwa wadau waliojitokeza kushuhudia fainali ya Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) lililokuwa pia likirushwa live kupitia Kituo Cha Runinga cha ITV
Mwanaafa Mwinzago (katikati) akishangilia Mara baada ya kutangazwa Mshindi wa Kitita Cha Milioni 50 za Kitanzania katika Fainali ya Kumsaka Mshindi wa Shindano la Tanzania Movie Talents (TMT) 2014 lililofanyika usiku wa kuamkia leo katika Ukumbi wa Mlimani City na Kuhudhuriwa na Mamia ya Watanzania.
Mwanaafa Mwinzago (katikati) akiwa katika picha ya Pamoja na wazazi wake na timu ya wafanyakazi wa TMT na washiriki wenzie mara baada ya kukabidhiwa mfano wa Hundi ya Shilingi Milioni 50 za Kitanzania Mara baada ya Kuwabwaga Washiriki wenzie tisa na Kuibuka Mshindi wa Kitita Cha Milioni 50 za Kitanzania katika Fainali ya Kusaka Vipaji Vya Kuigiza Nchini lijulikanalo kama Tanzania Movie Talents (TMT) ambalo limefikia Ukingoni Jana Katika Ukumbi wa Mlimani City.
Washiriki wa Tanzania Movie Talents (TMT) 2014 waliofanikiwa kuingia Kumi Bora wakiwa wanasubiri mshindi atangazwe 

Mwanaafa Akiwa amembeba Mdogo wake mara baada ya kutangazwa Mshindi wa Fainali ya Tanzania Movie Talents (TMT) 2014 na kuibuka na kitita cha Shilingi milioni 50.
Lulu akionyesha Bahasha iliyokuwa na JIna la Mshindi wa Tanzania Movie Talents (TMT) ambae ni Mwanaafa Mwinzago na Kumfanya kujishindia Shilingi Milioni 50 za Kitanzania
Baadhi ya wakazi wa Jiji la Dar waliojitokeza kushuhudia fainali ya TMT ambayo ilikua ikirushwa live kupitia ITV.
Malaika Band wakitoa Burudani wakati wa fainali ya TMT 2014 katika Ukumbi wa Mlimani City Usiku wa Kuamkia leo.
Christian Bella Akitoa burudani kwa kuimba wimbo wa Nani kama Mama ambao uliamsha Shamra Shamra katika Ukumbi wa Mlimani City Usiku wa Kuamkia leo na Mwanaafa Mwinzago Kuibuka Mshindi.
Majaji wa Tanzania Movie Talents (TMT) 2014 
Joti akitoa Suprize ya ukweli haswa katika fainali ya Tanzania Movie Talents (TMT) katika ukumbi wa Mlimani City usiku wa Kuamkia Leo
 Mkurugenzi wa Kampuni ya Proin Promotions, Geofrey Lukaza akiwa na Mkewe katika Red Carpet Kabla ya Show Kuanza katika Ukumbi wa Mlimani City usiku wa Kuamkia leo

 Mc Pilipili Akifanya Yake
 Wadau wa Kampuni ya Proin Promotions Limited wakiwa katika Picha ya Pamoja mara baada ya MShindi wa Tanzania Movie Talents (TMT) kupatikana na kila Mmoja kusherehekea Ushindi huo

MTEMVU ATOA MKONO WA IDD WA VYOMBO NA SH. 10,000 KWA VIONGOZI 912 WA MATAWI YA CCM TEMEKE

MTEMVU ATOA MKONO WA IDD WA VYOMBO NA SH. 10,000 KWA VIONGOZI 912 WA MATAWI YA CCM TEMEKE

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com

Mbunge wa Jimbo la Temeke, Abbas Mtemvu (kulia), akimkabidhi boksi la vyombo na zawadi ya sh. 10,000 mmoja wa viongozi 912 wa matawi wa ya CCM na jumuiya zake wa jimbo hilo, katika hafla ya kutoa mkono wa Idd el Fitr Dar es Salaam jana. Kila mmoja alipata zawadi kama hiyo. Katika boksi hilo kuna vikombe, birika, vijigo, sahani na chupa ya chai. Katikati ni mke wa mbunge huyo, Mariam Mtemvu. PICHA ZOTE NA RICHARD MWAIKENDA;KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Mtemvu akimkabidhi Mwenyekiti wa UWT CCM tawi la Mji Mpya Kata ya Buza, Temeke.

Baadhi ya viongozi wakiondoka na vyombo vyao huku wakiwa na sh. 10,000 kibindoni.
Shehena ya vyombo vilivyokuwa vinagawiwa
Sehemu ya umati wa viongozi wa CCM wa matawi waliofika kupata zawadi hizo. Wengi walimpongeza Mtemvu kwa moyo wake wa kujitolea.
Ni furaha tele kwa mama huyo

        Mary wa Yombo Kilakala akifurahia zawadi yake na kitita cha sh. 10,000
Mwenyekiti wa CCM Tawi la Mlimani, Kata ya Kilakala, Temeke, Dar es Salaam, Omar Kichapwi huyoooo na vyombo vyake . ndani ya vyombo hivyo kuna vikombe, birika vijiko na chupa ya chai
Mke wa Mbunge wa Jimbo la Temeke, Mariam Mtemvu akimkabidhi zawadi ya vyombo na sh. 10,000 mmoja wa viongozi wa CCM wa Jimbo hilo.
Naibu Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Temeke,  akimkabidhi vyombo na sh. sh. 10,000 mmoja wa viongozi wa matawi wa CCM wa Jimbo hilo. Zawadi hizo zilitolewa na Mbunge wa Jimbo hilo, Abbas Mtemvu (kulia).
Wakifurahia kupata zawadi hizo

MSANII WA BONGO MOVIE ESTER KIAMA AFUTURISHA WASANII WENZAKE JIJINI DAR

MSANII WA BONGO MOVIE ESTER KIAMA AFUTURISHA WASANII WENZAKE JIJINI DAR

Posted in
No comments
By danielmjema.blogspot.com
Msanii chupukizi wa Bongo Movie, Ester Kiama leo alifuturisha wasanii, ndugu,jamaa na marafiki zake ikiwa ni ishara ya kumkumbuka marehemu mama yake mzazi ambaye alishatangulia mbele ya haki. Akitoa shukrani zake kwa waalikwa, alisema ameona vyema kuandaa chakula cha pamoja ili waweze kumuenzi mama yao mzazi kwa vile alipenda sana watu hasa kukutana na kupata chakula pamoja.
Msanii chupukizi wa Bongo Movie, Ester Kiama akiendelea kutoa shukrani zake za pekee.

Mjomba wa Msanii chipukizi wa Bongo Movie, Ester Kiama akitoa shukrani zake za pekee.

Msanii wa runinga, Michael Deodatus Sango ‘Mike’ akitoa shukrani kwa niaba ya rais wa Bongo Movie Steve Nyerere ambaye hakuweza kufika.
Wasanii, ndugu jamaa na marafiki waliofika wakipata futari.
Kila mmoja hakuwa nyuma kupata futari.
Huduma zikiendelea kutolewa.
Kumbu Kumbu.
Picha ya pamoja na wasanii wenzake mara baada ya kupata futari.
Msanii chupukizi wa Bongo Movie, Ester Kiama (kati) akiwa na Dada yake kushoto na mdogo wake wakipata ukodak.
Msanii chupukizi wa Bongo Movie, Ester Kiama akiwa na wajomba zake.

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .