KICHANGA CHA SIKU MOJA CHAOKOTWA KIKIWA KIMETELEKEZWA BARABARANIMOSHI
Posted in
No comments
Thursday, June 28, 2012
By
danielmjema.blogspot.com
Na Mary Mosha,
Moshi.
WIMBI la matukio ya wanawake kujifungua na kuwatelekeza
watoto limekuwa likiongezeka nchini ambapo katika tukio la kusikitisha jeshi I la polisi mkoani Kilimanjaro, limemuokota kichanga kinacho dhaniwa kuwa ni cha siku
moja kikiwa kimetelekezwa kando
kando ya barabara ya kibosho , wilaya Moshi
vijijini mkoani Kilimanjaro.
Akidhibitisha ukweli wa tukio hilo, kamanda mwandamizi wa jeshi la polisi la mkoani wa Kilimanjaro Robert Boaz , alisema, majira ya asubuhi ya jana, walipata
taarifa kutoka kwa wananchi kuwa kuna kichanga kimettelekezwa katika barabara
ya kibosho.
Kamanda Boaz, alisema kichanga hicho chenye jinsia ya kiume,
kinakadiriwa kuwa ni cha siku moja, vijana wake walifika maeneo hayo na
kumchukua na kumkimbiza katika hospitali
ya rufaa ya KCMC kwa ajili ya uangalizi
wa madaktari wakati uchunguzi wa tukio hilo likiendelea.
“Tulimkuta mtoto huyo katika hali nzuri tu na kwa usalama
zaidi, tumempeleka katika hospitali ya KCMC, chini ya uangalizi wa madaktari
bingwa wa watoto,” alisema Boaz na kuongeza kuwa
“ Askari wangu kwa sasa wanafanya uchunguzi ili kuweza
kubaini ni nani aliyefanya kitendo hicho cha kinyama na tutakapofanikiwa
kumkata hatua za kisheria zitachaukua mkondo wake,” alisema kamanda Boaz.
Kamanda boaz, alitoa wito kwa wakazi wa maeneo hayo, kutoa taarifa ya mtu yeyote,
aliyekuwa mjamzito awali na kwa sasa haupo kwa hali za kutatanisha, kutoa
taarifa katika jeshi la polisi ili kuweza kumbaini mama wa mtoto huyo.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :