WILFRED MOSHI AMERUDI NCHINI LEO BAADA YA KUWEKA REKODI YA KUFIKA KATIKA KILELE CHA EVAREST
Posted in
No comments
Wednesday, May 30, 2012
By
danielmjema.blogspot.com

KIJANA Wilfred moshi(33), mkazi wa moshi mjini, wilaya ya
moshi, mkoani Kilimanjaro ambaye ni mtanzania wa kwanza kufika katika kilele
cha mlima Evarest amerejea nchini na kupokelewa na umati mkubwa ya watanzania
waliofurika katika uwanja wa kimataifa wa Kilimanjaro KIA, kumpokea shujaa
aliyeandika historia kwa kufika kilele cha mlima huo mrefu zaidi duniani.
Wilfred ambaye ni mfanyakazi wa kampuni ya kitalii cha
Nature Discovery amerejea nchini ikiwa ni siku chache tu tangu alipofanikiwa kufika katika kilele cha
mlima Evarest tarehe 19 ya mwezi huu. Wilfred alipokelewa uwanjani hapo na
ndugu jamaa na marafiki wakiwemo baba yake mzazi Ceryl Moshi, mama yake mzazi
Martina moshi, mke wake Agness Wilfred pamoja na watoto wake wawili Martina
Wilfred na Martin Wilfred.
Akiongea na waandishi wa habari mara baada ya kutua katika
ardhi ya Tanzania, Wilfred aliyeondoka hapa nchini Machi 28 mwaka huu akielekea
Newzealand alisema baada ya kufika Newzealand aliungana na marafiki zake na
kufunga safari kuelekea Nepal ambako ndiko iliko mlima Evarest. alisema katika safari yao walikumbana na vikwazo
vingi sana akitaja tatizo la hewa kuwasumbua sana hadi kulazimika kutumia hewa
ya oksijeni.
“namshukuru sana Mwenyezi kwa kufanikisha ndoto yangu ya kuwa mtanzania wa kwanza kuingia
katika kumbukumbu za vitabu kufika katika kilele cha mlima evarest, siri ya
mafanikio siku zote ni kujituma na kuwa na imani katika kile unachokifanya
.naiomba serikali, adau wote wa katika sekta ya utalii, wizara ya utamaduni,
waangalie ni kwa namna gani tunaweza kufanya katika kuhakikisha tunaitangaza
vyema nchi yetu pamoja na rasilmali zake zote pamoja na kuenzi mlima wetu,
mlima kilimanjaro,” alisema Wilfred.
Wakiongea na MTANZANIA kwa nyakati tofauti, baadhi ya
wananchi waliofika uwanjani hapo kumpokea shujaa wao, waliitaka serikali na
wahusika katika idara zake zote kuhakikisha
kwamba kile kilichofanywa na mzalendo Wilfred hakipotei hivihilivi. walisema
kwa kulipeperusha bendera ya Tanzania ni vyema wizara ya utalii pamoja na ile
ya utamaduni kumtangaza kijana Wilfred moshi kuwa balozi wa kulitangaza mlima
Kilimanjaro katika anga la kimataifa.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :