MBUNGE WA BAHI APANDISHWA KIZIMBANI KWA MASHITAKA YA KUPOKEA RUSHWA
Posted in
No comments
Tuesday, June 5, 2012
By
danielmjema.blogspot.com
Mbunge Badwel, akiongozwa na askari baada ya kufikishwa mahakamani hapo.
Akirudishwa mahabusu baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana.
MBUNGE
wa Jimbo la Bahi, Mkoani Dodoma, Omar Badwel, leo amepandishwa
kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi, Kisutu jijini Dar es Salaam
na kusomewa mashitaka mawili ya rushwa.
Akimsomea
mashitaka yake, Mwendesha Mashitaka wa Taasisi ya Kupambana na Kuzuia
Rushwa (Takukuru), Ben Lincoln, amesema mnamo Mei 30 mwaka huu,
mshitakiwa akiwa Mbunge wa Jimbo la Bahi na Mjumbe wa Kamati ya Hesabu
za Serikali za Mitaa, alimuomba rushwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya
Mkuranga, Schola Jonathan, ili aweze kuwashawishi wajumbe wa kamati yake
waweze kuipitisha taarifa ya fedha ya halmashauri hiyo.
Shitaka
la pili alilosomewa ni kupokea rushwa, ambapo mwendesha mashitaka huyo
wa Takukuru amedai kuwa mnamo Juni 2 mwaka huu, mshitakiwa alinaswa
kwenye Hotel ya Peacock jijini Dar, akipokea rushwa ya shilingi milioni
moja kutoka kwa Schola.
Mbunge
huyo alikana mashitaka hayo mbele ya hakimu aliyekuwa akisikiliza kesi
hiyo, Faisar Kihamba, ambapo hakimu huyo aliiahirisha mpaka Juni18 mwaka
huu, itakapotajwa tena mahakamani hapo
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :