Sahihisho La Habari Kuhusu Jerry Muro
Posted in
No comments
Sunday, June 10, 2012
By
danielmjema.blogspot.com
| Jerry muro akiongea na waandishi wa habari |
Jana
tuliweka hapa habari kuwa Jerry Muro anrudi TBC.Jerry mwenyewe ametupa
ufafanuzi wa ziada ambao hatukuwa tumeupata kabla na kuwa hatakuwa
mwajiriwa wa TBC bali atawauzia vipindi na atakuwa huru kuviuza TV
yeyote.Hapa chini ni maelezo ya Jerry Muro.Tunaomba radhi sana kwa
upungufu huo.
Msaidizi wa Mwenyekiti,Dar
UFAFANUZI WA JERRY MURO
Napenda
kuwajulisha wanamabadiliko kuwa kuanzia jumapili tarehe 10 mwezi
huu,saa tatu na nusu usiku nitaanza kurusha mfululizo wa vipindi vyangu
TBC,lengo la vipindi hivi ni kuonyesha kazi mbalimbali zilizofanywa na
serikali kwa kushirikiana na taasisi ya mkapa foundation haswa katika
masuala ya afya.
Vipindi
pia vitaonyesha changamoto mbalimbali tunazokabiliana nazo katika sekta
ya afya ili kwa pamoja tuweze kuzitatua haswa katika maeneo ya
pembezoni mwa nchi(vijijini).
Vipindi hivi nimefanya mwenyewe na kampuni binafsina vitarushwa TBC kwa ufadhili wa mkapa foundation.
Napenda ieleweke,mimi jerry muro sijaajiriwa TBC bali narusha vipindi vyangu pale kwa muda wa miezi miwili na nusu.
Mashabiki
na wapenzi wa kazi zangu karibu tutazame ili pamoja tuweze kukabiliana
na changamoto zinazolikumba taifa letu na hatimae tuweze kuleta maisha
bora kwa kila Mtanzania.
Naomba kuwasilisha,
Jerry muro.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako

0 MAOINI :