HUU NDIO MCHANGANUO WA GHARAMA ZA UJENZI WA BARABARA YA MAGARI YAENDAYO KASI
Posted in
No comments
Saturday, July 7, 2012
By
danielmjema.blogspot.com
Waziri wa ujenzi John Magufuli
wakati akisoma bajeti ya wizara yake bungeni July 5 2012 amesema kiasi
cha shilingi milioni 577 kimetengwa kwa ajili ya ukarabati wa barabara
ya Ubungo Maziwa, External, Tabata, Dampo na Kigogo.
Milioni 1000 ni kwa ajili ya
ujenzi wa barabara ya lami Kimara, Kilungule na External, ambapo milioni
elfu 2 zimetengwa kwa ajili ya barabara ya Mbezi, Maramba Mawili pamoja
na barabara iendayo shule ya msingi Maramba mawili, Kinyerezi na
Banana.
Milioni nyingine elfu mbili mia
moja ni kwa ajili ya barabara ya Tegeta Kibaoni, Wazo Hill, Goba, Mbezi
na Morogoro, Milioni elfu moja imetengwa kwa ajili ya barabara ya tangi
bovu goba na Goba ambapo milioni 573 ni kwa ajili ya ukarabati wa
barabara ya kimara Baruti, Msewe, Changanyikeni ambapo pia Magufuli
amesema Wizara yake pia kupitia TANROADS imetenga bilioni 18 kwa ajili
ya mkoa wa Dar es salaam.
Kuhusu ujenzi wa barabara za
juu kwenye jiji la Dar es slaam, Waziri Magufuli amesema umetengewa
bilioni elfu mbili, daraja la kigamboni limetengewa milioni elfu mbili
na mia saba, barabara ya Dar es salaam Mbagala imetengewa shilingi
milioni elfu nane na mia tano, kiasi cha shilingi milioni elfu sita na
mia sita kimetengwa kwa ajili ya upanuzi wa sehemu ya bendera tatu
gerezani ambapo pia ujenzi wa maegesho ya vivuko yametengewa zaidi ya
shilingi milioni 2000.
Kwenye line nyingine, Magufuli
amesema barabara za mikoa zimetengewa shilingi milioni 20 na 410 zote
zikiwa fedha za ndani ambapo kilichopangwa kutekelezwa ni kufanya
ukarabati wa jumla ya ukarabati wa jumla ya kilomita 337 kwa kiwango cha
changarawe na kujenga kilomita 23.7 kwa kiwango cha lami.
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :