KIONGOZI WA MBIO ZA MWENGE AMFAGILIA MBUNGE FILIKUNJOMBE KWA KUFANUIKISHA MAENDELEO LUDEWA , AMPONDA DIWANI KWA KUUKWEPA MWENGE
Posted in
Matukio
No comments
Friday, July 4, 2014
By
danielmjema.blogspot.com
Mwenge wa Uhuru ulipowasili wilaya ya Ludewa eneo la Madope mpakani mwa Njombe na Ludewa |
Watoto wea kijiji cha Mlangali wakifurahi kushika mwenge wa Uhuru |
Kiongozi wa mbio za Mwenge kitaifa Rachel Kassanda akimpongeza mwanamke mwenye ulemavu wa macho Bi Regina Kayombo kwa ujenzi wa nyumba ya kisasa |
Kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru taifa Rachel Kassanda akionya utumiaji wa madawa ya kulevya huku mmoja kati ya askari akichochea bangi iliyoteketezwa na kiongozi huyo wilayani Ludewa |
Mwananchi wa Ludewa mjini akishiriki kukimbiza Mwenge baada ya kuzindua ujenzi wa barabara ya lami mjini Ludewa |
Vijana wakimbiza mwenge kitaifa wakiondoka eneo la Manda leo asubuhi |
kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru Kitaifa Rachel Kassanda wa tatu kulia akiruka kwa ukakamavu na askari wengine wakati wa mbio hizo wilayani Ludewa |
Mwenge wa Uhuru ukikimbizwa katika barabara inayojengwa kwa kiwango cha lami mjini Ludewa |
Bi Ragena Kayombo akiwa ameshika mwenge wa Uhuru |
Bw Khamis Kayombo akiwa ameshika mwenge wa Uhuru |
Mtoto Sabina Kayombo wa Mlangali Ndani akiwa ameshika mwenge wa Uhuru
.............................. .............................. .............................. ..........................
Na Francis Godwin Blog -Ludewa
KIONGOZI wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa Rachel Kassanda amempongeza mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe kwa jitihada mbali mbali za kimaendeleozinazofanyika katika jimbo hilo na huku akimshambulia diwani wa kata la Mlangali Faraja Mlelwa (Chadema) kwa kushindwa kushiriki mbio za mwenge katika kata yake.
Alisema kuwa miradi 7 yenye thamani ya zaidi ya Tsh bilioni 3 ambayo mwenge wa Uhuru mwaka 2014 unaipitia katika jimbo la Ludewa na wilaya ya Ludewa kuwa ni miradi mikubwa ambavyo ni wazi mbunge wa jimbo hilo Filikunjombe amefanya kazi kubwa hasa ukilinganisha na majimbo mengine ambayo miradi yake haifikii thamani hiyo .
Kiongozi huyo alitoa pongezi hizo leo wakati wa kuzindua nyumba ya bora ya mkazi wa Mlangali Ndani Khamis Ignas Kayombo .
Kiongozi wa mbio za mwenge kitaifa Rachel Kassanda akimpongeza mbunge wa jimbo la LudewaDeo Filikunjombe kwa kanzi nzuri ya kuwaletea wana Ludewa maendeleo |
Alisema kuwa mbio za mwenge wa Uhuru zimekuwa zikihamasisha maendeleo katika maeneo mbali mbali na viongozi wapenda maendeleo wakiwemo wabunge na madiwani hawana budi kushiriki mbio hizo kama ambavyo wananchi wana wamekuwa wakifanya .
Kwani alisema hata kama diwani huyo alikuwa na majukumu yake binafsi hakupaswa kuwakimbia wananchi wake ambao wamejitokeza kuupokea mwenge na kuwa kitendo cha diwani kushindwa kushiriki ni wazi kuwa ni diwani asiyependa maendeleo katika eneo lake.
Mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe kulia akimtazama mwandishi wa TBC Bw Msigwa wakati akiendelea kukusanya habari za mwenge |
“Ndugu zangu watanzania na wananchi wa Mlangali wilaya ya Ludewa kwanza napenda kumpongeza mbunge wenu Deo Filikunjombe natambua jitihada mbali mbali za kimaendeleo ambazo amekuwa akizifanya ndani ya jimbo la Ludewa na nje ya jimbo kwa maana ya mchango wake mkubwa katika bunge la jamhuri ya muungano wa Tanzania ila ninapenda kuwaeleza wazi kuwa ni viongozi wachahe wa kisiasa ambao wamekuwa wakiacha posho bungeni na kushiriki mbio za mwenge kama ilivyo kwa Filikunjombe ninampongeza sana ila kama kiongozi wa mbio za mwenge sijapendezwa na kitendo cha diwani wenu kushindwa kufika hapa leo “
Hata hivyo alisema wananchi hawana sababu ya kuendelea kuwasikiliza viongozi wa vyama vya siasa ambao wamekuwa wakipinga mbio za mwenge kwani mwenge wa Uhuru si mwenge wa chama cha siasa ila upo kwa ajili ya watanzania wote na ni sehemu ya kudumisha mshikamano wetu na kuenzi amani yake pamoja na kuhamasisha maendeleo miongoni mwetu.
Kiongozi wa mbio za mwenge wa Uhuru kitaifa Rachel Kassanda akiwa na Bw Khanmis Kayombo na mkewe baada ya kuzindua nyumba yao ene la Mlangali Ndani |
Hivyo kiongozi yeyote wa kisiasa ni lazima kuendelea kuenzi mshikamano wetu na kushiriki katika mbio hizo ambazo zilihasisiwa na baba wa Taifa hayati Julius Nyerere ambae kwa sasa kanisa la RC limepata kumtangaza kuwa miongoni mwa watakatifu kutokana na mchango wake mkubwa wa kuliletea taifa hili uhuru wake.
Pia alisema kuwa wapinzani wanaosema Mwenge wa Uhuru umepitwa na wakati na wakiingia madarakani watauweka katika jumba la makumbusho hawana nia njema na nchi hii na kuwataka watanzania kuwapuuza watu hao na ikibidi watu hao kwenda kumwomba radhi mjane wa baba wa Taifa Maria Nyerere ambae kitendo cha wao kuusemea vibaya mwenge huo ni sawa na kumtukana baba wa Taifa
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :