IDADI YA WALIOFARIKI DUNIA NA WALIOOKOLEWA KWENYE AJALI YA BOTI ZANZIBAR JANA MCHANA.

Posted in
No comments
Thursday, July 19, 2012 By danielmjema.blogspot.com

Inawezekana taarifa za ajali ya boti ya Seagul iliyotokea leo (July 18) mchana Zanzibar ukawa umezisikia au kuzisoma sehemu mbalimbali lakini kauli hii ya Waziri wa mambo ya ndani imetoka kwenye taarifa ya habari ya saa mbili usiku.  

Waziri Emmanuel Nchimbi akiongea kwenye taarifa ya habari ya saa mbili usiku july 18 2012  TBC1 alisema “vikosi vya uokoaji vinaongozwa na mkuu wa jeshi la polisi Inspekta Jenerali Said Mwema vinaendelea na uokoaji”

Kuhusu watu waliopoteza maisha au kuokolewa Waziri Nchimbi amesema “Katika abiria wanaokadiriwa kuwa zaidi ya 250 waliokua wamebebwa na boti hiyo, wameokolewa 124 wakiwa hai na waliothibitishwa na jeshi la polisi kufariki dunia ni saba tu, juhudi kubwa za uokoaji zinaendelea”

.
Mwokoaji akiwa na mmoja wa maiti wa ajali hiyo
Waokoaji wakiokoa moja ya maiti. wakiwa katika boti ya Kilimanjaro.
Majeruhi wakiwa katika mgongo wa boti hiyo wakisubiri kuokolewa.
Baadhi ya Abiria wakiwa katika moja ya chombo cha kuokolea wakielea baharini wakisubiri kuokolewa.
Boti ya KMKM ikiwa katika zoezi la kuokowa majeruhi.

Majeruhi alieokolewa katika meli ya Star Gate iliozama huko katika bahari ya Chumbe Zanzibar na ikiwa na abiria 250.
Daktari akitowa huduma ya kwanza kwa mmoja wa majeruhi wa boti iliozama ikiktokea Dar-es-Salaam
Majeruhi wa ajali ya Meli wakiwa katika Hospitali ya Mnazi Mmoja wakipata huduma baada ya kuokolewa.
Majeruhi wakiwa katika hospitali ya Mnazi Mmoja
Picha/Ramadhan Othman - Ikulu

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .