KAMPENI YA MLIMA KILIMANJARO DHIDI YA MAAMBUKIZI MAPYA YA UKIMWI YAKUSANYA DOLA LAKI SITA!
Posted in
No comments
Saturday, July 7, 2012
By
danielmjema.blogspot.com
Kampeni
iliyopewa jina la mlima kilimanjaro dhidi ya maambukizi mapya ya ukimwi
iliyozinduliwa na Rais mstaafu wa awamu ya pili, Alhadji Ali Hassan
Mwinyi limefanikiwa kukusanya jumla ya kiasi cha dola 600,000 sawa na
shilingi 960,000,000.
kampeni
hiyo ambayo iliandaliwa na Mgodi wa dhahabu wa Geita, Geita Gold Mine
kwa kushirikiana na wadau wengine wakiwemo na Barrick Gold Corporation
pamoja na wanaharakati wengine wa mapambano dhidi ya janga la ukimwi.
Wakizungumza
na kijiwe blog baada ya kumaliza safari ya siku 7 na kufanikiwa kufika
kileleni baadhi ya washiriki wa kampeni hiyo walisema kuwa katika safari
zote ambazo wamekuwa wakishiriki kupanda mlima huo mrefu zaidi barani
afrika, walisema kuwa safari ya kupanda mlima mwaka huu ulikuwa mgumu
kuliko kipindi cha nyuma.
Human
Resource Manager wa Ustawi wa Jamii wa kampuni ya Barrick Gold
Corporation, bw. Simon Sanga, ambaye alifanikiwa kufika kileleni mwa
mlima huo, alisema tofauti na safari zilizopita, mwaka walikumbana na
vikwazo moja wapo akitaja mvua zinazoendelea kunyesha katika mlima huo
pamoja na hali ya hewa zisizotabirika.
"Namshukuru
Mungu tumerudi salama pamoja na safari kuwa ngumu, tulifika mahali
nikahisi siwezi kuendelea tena lakini namshukuru Mungu nimerudi mzima,"
alisema Sanga.
Akizungumza
katika sherehe ya kuwapokea wanahakati hao, mkuu wa wilaya ya Moshi,
Dkt.Ibrahim Msengi, aliyemwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro,
Leonidas Gama, alisema serikali inaunga mkono kwa dhati kampeni zote
zinazolenga kuelimisha jamii juu ya athari ya janga la Ukimwi.
Msengi alitoa wito kwa jamii zote zinazozunguka mlima wa
Kilimanjaro, kujikita katika harakati ya kukarabati mazingira ya
mzunguko wa mlima huo
Kaimu
mkurugenzi mkuu wa mgodi wa dhahabu wa Geita ( GGM) Steven Robin,
ambaye naye alikuwa mmoja wa wanaharakati hao alisema kuwa kiwango
kilichopatikana katika kampeni hiyo kimeshinda viwango vyote
vilivyokusanywa katika kampeni zilizopita na kuongeza kuwa kiwango hicho
kimevunja rekodi kwa kuvuka lengo lao la kukusanya shs. 750,000.
Bw.Robin, alisema kuwa wanajivunia matokeo mazuri yaliyopatikana
kwenye kampeni ya “Mlima Kilimanjaro dhidi ya maambukizi mapya ya virusi
vya UKIMWI" na kuongeza kuwa wamehamasika kuanda kampeni hiyo mwakani na miaka mingine mingi.
Alidokeza kwamba fedha hizo zitatumika kwa uwiano mzuri kwa welengwa na kusimamiwa vema.
jumla
ya wanaharati wapatao 50 walipanda mlima kilimanjaro, ambapo 49 kati
yao wakifanikiwa kufika kileleni huku mmoja akipata matatizo na
kulazimika kurudi kituoni.
wanaharakati hao walipokewa katika Geti la Mweka Kibosho, wilaya ya Moshi, Mkoani kilimanjaro
Habari Zingine
Mjulishe Mwenzako
0 MAOINI :