MZEE CHILO: SIJALAZWA KCMC HATA SIKU MOJA

Posted in
No comments
Saturday, July 7, 2012 By danielmjema.blogspot.com

maktaba
Msanii na nguli wa bongo movies nchini Ahmed Olotu, maarufu kama Mzee Chilo, amekana taarifa zilizoripotiwa na gazeti moja maarufu nchini kwa kuripoti habari za udaku iliyoripoti katika gazeti lake toleo la Jumamosi kuwa msanii huyo amelazwa katika hospitali ya KCMC, kuwa ni uongo na uzushi unaolenga kumyumbisha katika gemu la bongo movie.

maktaba
Mzee Chilo alisema hayo katika studio ya Hmedia alipoitembelea studio kwa lengo la kujionea kazi zinazofanywa na studio hiyo.

maktaba
" nataka wapenzi wangu waelewe kwamba taarifa za hivi zilizoandikwa zikidai kuwa nimelazwa KCMC ni uongo na nataka niwaondoe hofu mashabiki wangu kwamba niko fiti na siku ya jumatatu nitarudi Dar kumalizia filamu yangu na Ray," alisema Mzee Chilo.



maktaba

Mzee Chilo alisema kuwa siku hiyo ni kweli aliugua Ghafla akiwa safarini akiwa njiani kuja ambako ndiko asili yake iliko.

alisema kuwa alilazimika kwenda KCMC lakini kutokana na mgomo unaondelea hivi sasa nchi nzima alilazimika kuenda katika hospitali ya Dkt. Mbwambo iliyoko mjini Moshi na kutibiwa akaondoka na kuongeza kwamba ya yeye kulazwa sio kweli.

Mzee Chilo ambaye yuko mjini hapa kutembelea familia ataondoka keshokutwa kuelekea Dar es Salaam tayari kwa shughuli ya kukamilisha filamu aliyoshirikishwa na msanii mwenzake katika gemu hilo, Ray.

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .