VIONGOZI WA VURUGU KITUO CHA MABASI MOSHI WATIWA MBARONI

Posted in
No comments
Saturday, July 7, 2012 By danielmjema.blogspot.com

 Na Mary Mosha, MOSHI .
 
7 July 2012
 
JESHI la polisi  mkoani Kilimanjaro, linawashikilia watu 18 wenye umri kati ya miaka 18-20 kwa kosa la kuhusika na vurugu  zilizotokea kwenye mgomo wa madereva wa magari madogo kwa lengo la kupinga ongezeko la ushuru.  
 
Akizungunzia  hali halisi ya mgomo huo ,kaimu kamanda wa mkoa wa Kilimanjaro  Koka  Moita  alisema,   watu hao wanasadikiwa kuwa ni vibaka  waliojitokeza wakati mgogogoro huo  kwa lengo la kujipatia  masilahi yao binafsi  
 
Kaimu kamanda  alisema,  kutokana na vurugu hizo,  vilizosababishwa na vijana wanaosadikika kuwa ni vibaka , magari mawili yaliharibika na watu watatu waliokuwa kwenye gari  yenye nanba za usajili  AGQ T 703 walijereuliwa  na kupelekwa kwa  hospitali ya  Mkoa Mawenzi kwa ajili ya matidabu na waliweza kuruhusiwa.
 
Aidha vijana hao walikuwa wakifanya  fujo mbali mbali zikiwemo kuwashusha abiri na kuwachapa viboko, waliokuwa wamebebwa na baadhi ya madereva waliokuwa wametii sheria iliyopitishwa na manispaa   ya  ongezeko la ushuru kwa kuwaswagome kama wezao.
 
Hata hivyo, Moita alisema , kabla ya ongezeko la ushuru  daladala zilikuwa zinalipa shilingi 1000, na  mabasi shilingi 1500  kama ushuru ya maegesho lakini kwa sasa katika  sheria iliyopitisha na manispaa  iliwataka  kulipa shilingi 1500 kwa daladala, na  shilingi 2000 kwa magari makubwa., jambo ambalo lilileta mgogo mkubwa  baina ya manispaa na wadau wa usafiri.
 
 Kwa upande mwingine , kaimu kamanda  alikiri kuwa, jeshi la polisi haliusiki na kitu chochote katika mgogoro unaoendelea  baina ya manispaa na wadau wa usafi, ila wataendelea kuweka dori ili kuwakikisha hakuna vurugu yoyote inayoendelea mpaka mwafaka utakapopatikana baina ya pande zote mbili, kwani matatizo yao yapo mezani.
 
 Kaimu kamanda  alitowa wito kwa wananchi kutojishughilisha mgogoro wowote usio wahusu unapotokea  kwani  wataishia kwenye matatizo  na badala yake kuziacha pande hizo mbili kutatua matatizo yao kwa nja ya amani.
 
  Pia alisema, baada ya uchunguzi zaidi watu hao watafikishwa mahakanani
 .
Hata hivyo hali ya  mgomo bado haikuwa shwari, kwani magari ya pasua na kiboroloni   yalikuwa bado hayaanza kufanya kazi ipasavyo, huku baadhi ya magari yakiwa  yanapokia lakini hayalipi ushuru

Habari Zingine

0 MAOINI :

Fadhili Athumani



EastAfrica Swahili Blogger, Journalist at Mwanaspoti Kenya, Nairobi Kenya, Call: +254705246475, whatsapp:+255654724337, Email: fadhiliathumani85@gmail.com

Proudly Powered by EAMG .